Kwanini hakukuwa na haja ya mwanadamu kuwa na uwezo wa kunusa kama wanyama?

mathsjery

JF-Expert Member
Sep 26, 2015
2,207
1,755
Nimekuwa nikisikia watu wanasema kuwa wanyama wanaitambua harufu ya mwanadamu, kwa kuwa nilishindwa kujigeuza kuwa kama mnyama, imekuwa ngumu kuielewa hii hadithi, naitaji ufafanuzi kama kuna tafiti ziliofanyika kulitambua hili nizifahamu, lakini pia kama ni kweli kwanini wana uwezo huo na kwanini mwanadamu hawezi tambua harufu ya wanyama wengine.

Mfano kufahamu kuwa kuna simba hapa kichakani au mtaani, ni mpaka nimwone au nisikie sauti yake, ila sijui harufu yake inanukiaje.
 
Mbona tunanusa na kutambua uwepo wa beberu? au mwenzetu huna uwezo huo.
 
Mbona tunanusa na kutambua uwepo wa beberu? au mwenzetu huna uwezo huo.
chukulia haujawahi kutana simba au chui, ila yupo maeneo ulipo utafahamu kuwa ni simba au chui?
 
MNYAMA
_Simba hanaitaji kunusa ili kujua swala yupo wapi apate mlo wake hivyohivyo chui, Duma, fisi, chatu, mbwamwitu.
_Swala/nyumbu/nyati...wanahitaji kunusu simba yupo wapi aweze jihami.

BINADAMU
Binadamu, haitaji kunusa ili kuuza Azamukwaju ili ajipatie mlo ni suala la kwenda stendi nakuuza / haitaji kunusa ili kujihami ni suala la kujua tu huyu mjeda ana Ak47 inabidi niwe na despline.
 
Nadhani sababu kubwa ni uwezo wa mwanadamu kuona kwa macho zaidi kuliko hisia... Macho ya wanyama wengi yana uono hafifu usiokamili

Sent using Jamii Forums mobile app
Naamini mlango mmoja wa fahamu ukiwa haufanyi kazi kabisa/vizuri basi ubongo unaupa nafasi na uwezo kwa viungo vingine kufanya kazi zaidi
 
Nimekuwa nikisikia watu wanasema kuwa wanyama wanaitambua harufu ya mwanadamu, kwa kuwa nilishindwa kujigeuza kuwa kama mnyama, imekuwa ngumu kuielewa hii hadithi, naitaji ufafanuzi kama kuna tafiti ziliofanyika kulitambua hili nizifahamu, lakini pia kama ni kweli kwanini wana uwezo huo na kwanini mwanadamu hawezi tambua harufu ya wanyama wengine.

Mfano kufahamu kuwa kuna simba hapa kichakani au mtaani, ni mpaka nimwone au nisikie sauti yake, ila sijui harufu yake inanukiaje.
MNYAMA
_Simba hanaitaji kunusa ili kujua swala yupo wapi apate mlo wake hivyohivyo chui, Duma, fisi, chatu, mbwamwitu.
_Swala/nyumbu/nyati...wanahitaji kunusu simba yupo wapi aweze jihami.

BINADAMU
Binadamu, haitaji kunusa ili kuuza Azamukwaju ili ajipatie mlo ni suala la kwenda stendi nakuuza / haitaji kunusa ili kujihami ni suala la kujua tu huyu mjeda ana Ak47 inabidi niwe na despline.
Jibu zuri. Binadamu ana uwezo mkubwa wa akili kupambana na mazingira yake.
 
Ingekuwa hivyo hata maumbile ya pua zetu yangekuwa mabaya hebu fikiri pua yenye uwezo wa kunusa hata kilometa moja ingekuwaje kama hizi tu za mita kadhaa tunaziona mbaya hizo ingekuwa ni mashambulizi ya harufu tungepata na upungufu wa hewa😂😂

Natania tu mkuu ila nafikiri nature inahitaji kuwa balanced viumbe wote tukiwa na uwezo huo hao simba watakula nini..?
Kwanza ni heri maana hata magerezani kungekosekana wateja maana polisi wakija kukukamata unahisi harufu yao kabla hawajafika
Hata kukimbia mikopo isingekuwa tabu dawa kalili harufu ya anaekudai😂😂
Ingekuwa patashika nguo kuchanika.
 
Back
Top Bottom