Kwanini haki nchini ipatikane kwa njia tofauti na hali tunasema binadamu wote ni sawa katika katiba? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini haki nchini ipatikane kwa njia tofauti na hali tunasema binadamu wote ni sawa katika katiba?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by haki na usawa, Jun 30, 2012.

 1. h

  haki na usawa JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 476
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Naomba kuuliza wanajamii kwanini ndani ya nchi hii moja kuna utofauti wa kupata haki!
  Kwanini Mbunge mshahara wake ni maamuzi tu ya Spika?
  Kwanini Mshahara wa mfanyakazi (mahakimu/majaji/watumishi wengine) lazima kesi mahakamani au majadiliano?
  Je kuna utofauti gani kati ya anayeitikia NDIYOOO! kutoka usingizini/katika kusinzia na asiyelala usiku kuhudumia miili ya watu?
  Je kuna utofauti gani wa kujitolea na kazi ya wito?
  Je wabunge waliombwa na nani kugombea mbona wanazunguka kuomba kura zetu katika majimbo yetu?
  Je uwepo wao unatusaidia nini?
  Je kama mbuge anataka pesa yote ya nchi hii alipwe yeye vizuri bila kujali mwananchi na mfanyakazi anafaa kuwepo?
  Je kama tunakopa pesa nje ili tuwalipe wanasiasa vizuri na kudharau watalaam je kuna haja ya kukopa?
  Je kama hatuwekezi katika utalaam je tutaacha lini kuomba misaada na kuwa wa kwanza kusalimiana na mnyonyaji/bepari?
  Je ni anaweza asiwepo na kazi zikaendelea kama kawaida?
  Je ukiajiriwa ndo ujue kuwa umeolewa na serikali na hurusiwi kumsema vibaya mme wako hata kama anakunyanyasa?
  Je ni nani bora kati ya wawekezaji na watumishi wa nchi hii?
  wawekezaji wanalipa wanapoamua na wafanyakazi wanakatwa wapende wasipende je ni nani wa muhimu zaidi?
  Je mbona mweusi akiuawa wauaji hawapatikani? ila mweupe muaji anapatikana kwa gharama yeyote?
  Je ni sahihi kwa mweusi kuawa bila wauaji kutafutwa na helicopta za polisi?
  Je bado tumetawaliwa na wazungu, kisha wakoloni weusi(vibaraka) wa wazungu?
  Je nani anaweza kunipa takwimu za gharama za watumishi (wanaopata haki kwa kesi au majadiliano) na gharama za mawaziri, nawaibu waziri, makatibu wakuu, wasaidizi wao, naibu katibu mkuu, akurugenzi na wakuu wa tasisi za umma na wabunge?
  Je akina nani wengi? mawaziri/ naibu waziri/katibu mkuu/naibu katibu mkuu/wakurugenzi na wakuu wa tasisi za umma ukilingalisha na wanaodai haki kwa majadiliano na wananchi wanyonge?
  Je keki ya taifa (GDP) wanakula nani zaidi? viongozi au wanyonge?
  Je kama keki itagawanwa na wafanyakazi na viongozi wananchi watapata nini?
  Kwanini Mbuge anaweza kulipwa mshahara wa kiwango hicho na wengine mshahara wao ni sawa na mbunge ugawe kwa hamsini na mbili wakati wanaenda soko moja?
  Je watu wote wakiamua kuingia bungeni patatosha?
  "NAOMBA KILA ALIYE NA UWEZO WALAU JIBU MOJA KATI YA HAYA NA ANISAIDIE SEHEMU YAKE ILI KUNITOLEA MAWAZO NA MASONONEKO MOYONI"
   
Loading...