Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Jiulize - askari wetu wa FFU, pamoja na Raisi wetu Magufuli, wanaona kwamba wana uwezo mkubwa sana wa kuzuia maandamano na ghasia nchini. Wanajisifia kwa hilo.
Sasa angalia kwamba askari wa Ufaransa kwa wiki nzima wamekuwa wakipambana na waandamaji wenye ghasia bila kuwa na mafanikio kwa kiasi cha kutosha.
Unaweza kuwaza - ina maana FFU wa Tanzania wana ujuzi zaidi ya askari wa Ufaransa katika kutuliza maandamano na ghasia mitaani? Je unaweza kuwazia kwamba Raisi Macron wa Ufaransa anampigia simu Rais Magufuli na kumwambia "Raisi Magufuli, naona askari wako wa FFU wana uwezo sana wa kutuliza maandamano na ghasia, naomba unisaidie waje huku Ufaransa"
Haiwezekani. Kwa nini? Sio tu kwa sababu si kawaida kwamba majeshi ya polisi kuvuka mpaka wa nchi yao kwenda kutuliza nchi nyingine,
Kwa nini haiwezekani basi? Ni kwa sababu mafanikio ya FFU kutuliza mandamoano au ghasia nchini hayatokani na ujuzi wao zaidi ya askari wa Ufaransa - yanatokana na wao kutumia njia za kinyama na kikatili ambazo nchi kama Ufaransa haiwezi hata kufikiria kuzitumia kwa wananchi wake.
Kwa hiyo kama FFU au Rais Magufuli watajisifu juu ya uwezo wa askari Tanzania kutuliza maandamano na ghasia si kwa kuwa FFU Tanzania wana uwezo zaidi ya aksri wa Ufaransa, bali ni kwa kuwa FFU Tanzania wanatumia njia za kinyama na ukatili ambazo askari wa Ufaransa kamwe hawawezi kuzikubali zitumike katika nchi yao. Huo ndio ukweli.