Kwanini guta lina breki ya kukanyaga?

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
May 25, 2015
6,617
21,353
Habari zenu wadau wa JF garage,mbarikiwe sana.
Niko kwenye harakati za kuagiza guta kutoka Dar kulileta hapa Dodoma ili liweze kurahisisha usafiri na pia katika shughuli zangu ndogo ndogo za kijasiriamali.
Swali langu ni moja kwa nini aina hii ya usafiri inakuwa na breki ya kukanyaga wakati aina nyingine za usafiri kama huu zinakuwa na breki za kubinya kwa mikono (kama baiskeli) pia nitashukuru kama nitapata maelezo ya wapi naweza pata mafundi wa kubadilisha hii braking system ya hii kitu maana hii ya sasa inanikwaza sana.
 
Mkuu, breki ya "kubinya" na mkono ina disadvantage ukifananisha na ya kukanyaga.

Ma engineer walienda Lab ndio wakaamua iwe hivyo. Usijione Vin Disel uka customize hiyo brake, ikawa ya mkono kama Bajaji, trust me utapata Ajali.

Kwanini?

Brake ya mkono pressure yake ndogo na ata nguvu za anae apply ni ndogo. Ndio maana inatumika kwenye baiskeli na bajaji sana sana ambavyo havibebi mzigo mkubwa na havina speed kali sana.

Guta na Pikipiki zinaweza beba mzigo mkubwa na/au vinaweza kua katika speed kali. Ndio maana wanaweka option ya brake ya mguu kwakua inatoa pressure kubwa.
 
Back
Top Bottom