Kwanini geti la idete -ifakara limekuwa kero kwa sisi wakulima?

miti

Senior Member
Jun 16, 2012
136
23
Jamani ndugu zangu watanzania na viongozi, wakazi wa ifakara wanakelekwa sana na geti la idete kwakuona viongozi wamegeuza sehemu yao ya kutafutia pesa za kubadirisha magari nk. Na kikubwa kinachochosha kwamba gunia moja tsh. 6000/= hatamwenye gunia moja. Kinachosikitisha kwamba mkulima analima hekali 5 au zaidi anategemea muda wa mavuno apate gunia ishilini au zaidi, na hapo hapo kagharamia pesa nyingi kwa huduma ya shamba hilo, kwa bahati mbaya muda wa mavuno anakosa kabisa, au mwingine anapata kidogo labda kama gunia 1-5 kashaingia hasara hapo, bado anahitaji asafirishe kutoka shambani hadi barabarani, na mwingine anakolima kunakuwa mbali zaidi na barabara hivyo anahitaji atafute watu wa kusomba hadi barabarani awalipe, bado ghalama za usafiri kutoka barabarani hadi mjini/nyumbani /ghalani huu si uonevu jamani? Haya ndo maisha bora kwa kila mtanzania? Au maisha bora kwa kila kiongozi aliye ngazi ya juu wa (.........) nduguzangu geti hilo limewewa 2010 baada ya uchaguzi tu, muda wote walikuwa wapi kuweka? Wananchi wenye hasira kali walibomoa hata hjivyo hawakulizika waliona sehemu ya kula hakuna wakajenga tena na kuliimalisha zaidi pia na kuweka ulinzi wa hali ya juu, je kwa hali hii umaskini utaisha? Mkulima ataweza kujikwamua kwa mtindo huo? Nawatakia majadiliano mema
 
kwa sababu hamjitambui, hamjui nguvu ya umoja, hamjui hatma yenu ipo mikononi mwenu, mmechagua kulala hadi muda huu wa saa nane mchana.
Blame God?
 
Back
Top Bottom