Kwanini gazeti la Mwanahalisi halioni mazuri ya serikali ya JPM? Muda wote ni kuponda tu?

MTV MBONGO

JF-Expert Member
Feb 18, 2016
1,261
1,222
Natafakari kwanini kila nikisoma gazeti la Mwanahalisi naona mabaya tu ya serikali. Najiuliza kwani gazeti hili ni la chama fulani cha upinzani?

Kwanini wasiponde pabaya na kusifia mazuri ya serikali ya JPM? Enzi za JK waliponda ufisadi, sasa Magufuli anatumbua wanamponda yeye kulikoni?

Au wanatumiwa na watu wa nje kumdhoofisha Mh. Rais? Kwanini wasiwe kama gazeti la Jamhuri, mabaya yanaanikwa na mazuri pia?
 
Mwanahalisi usipowahonga fedha hawawezi kukusifia.
waliandika JK kaangusha na kuua Uchumi lakini jana Juma tatu wana sema Magu kazorotesha Uchumi, sasa cha kujiuliza Uchumi uliokufa unazorota vipi? Hicho kipeperushi ni kama Mwanamke Kahaba thamani ya Mwaume ni fedha sio umbo wala Mapigo
 
Mazuri gani unayotaka yasifiwe? Watanzania wanataka Huduma afya elimu ajira n.k.sio kutumbua watu kwani hawapati faida ulitaka gazeti lisifie hivyo badala ya kuelimisha mambo muhimu Kwa wananchi
 
wewe huna lolote , nano ambaye hakujui kwamba unaisho kwa kudra za ccm , kijana mdogo unakuwa mnafiki , ukizeeka si utaloga watu ? Sukari hakuna uchumi haujadondoka hapo ?

Mlisema JK kaua Uchumi sasa Magu anadondoshaje uchumi uliokufa? Uongo wenu muwe mnauhifadhi kwenye Memory card maana vichwa vyenu ni vya kunyolea Mapanki tu hamna kumbukumbu ya Uongo mlioongea jana
 
Mwanahalisi si Gazeti la kuaminika tena.....Liliandika maovu ya Lowasa kwa miaka 8 hao hao wakaja kumsafisha ..

Wasakatonge hao.
 
Acha kukurupuka na kuandika pumba. Kusema kweli kuhusu utendaji wa Magufuli hakuna uhusiano wowote na kutumiwa na watu wa nje. Kwani Watanzania hatuna uwezo wa kuona mwenendo wa nchi na kukosoa utendaji wa Serikali?

Hivi Rais anapoonyesha kuelemewa na cheo cha Urais kwa kuweweseka na kudai anajuta kuchukua form ya Urais au atarudi kijijini kwenda kuchunga ng'ombe au kudanganya umma eti kajitoa kafara ya kupambana na ufisadi wakati huo huo akiwakwepa mafisadi wa Lugumi, UDA, Escrow, Pride, Boti la Bagamoyo kisha kudai eti katoa sadaka mwili wake ili kuwatetea wanyonge halafu anawamwaga polisi wenye silaha kali na mbwa kuwafukuza wanafunzi 7802 na kuwapa masaa 24 tu. Tumia akili yako acha kukurupuka na kuandika pumba.

Wewe tuwekee mazuri ya huyu mwenye sera za kukurupuka na dikteta.

Natafakari kwanini kila nikisoma gazeti la Mwanahalisi naona mabaya tu ya serikali. Najiuliza kwani gazeti hili ni la chama fulani cha upinzani?

Kwanini wasiponde pabaya na kusifia mazuri ya serikali ya JPM? Enzi za JK waliponda ufisadi, sasa Magufuli anatumbua wanamponda yeye kulikoni?

Au wanatumiwa na watu wa nje kumdhoofisha Mh. Rais? Kwanini wasiwe kama gazeti la Jamhuri, mabaya yanaanikwa na mazuri pia?
 
Kama unadhani ana mapya mazuri ungechukua nafasi kuyataja kuliko kulalamika inaonyesha hata wewe huyajui hayo mazuri Ila unategemea hayo mazuri ya abunuasi ya "kusadikika" uyakute kwenye gazeti
 
Natafakari kwanini kila nikisoma gazeti la Mwanahalisi naona mabaya tu ya serikali. Najiuliza kwani gazeti hili ni la chama fulani cha upinzani?

Kwanini wasiponde pabaya na kusifia mazuri ya serikali ya JPM? Enzi za JK waliponda ufisadi, sasa Magufuli anatumbua wanamponda yeye kulikoni?

Au wanatumiwa na watu wa nje kumdhoofisha Mh. Rais? Kwanini wasiwe kama gazeti la Jamhuri, mabaya yanaanikwa na mazuri pia?
Gazeti linafadhiliwa na mafisadi waliotemwaq CCM.
Siku hizi topic zao ni kumponda Magufuli na kueneza uongo juu ya Ask Malasusa.
Walio nyuma ya hayo yote ni watu fulani CHADEMA.
 
Back
Top Bottom