SoC01 Kwanini fursa ya ufadhili wa kimasomo nje ya nchi ni kwa ngazi za juu tu za elimu?

Stories of Change - 2021 Competition

cilla

JF-Expert Member
Jul 15, 2011
369
296
KWANINI FURSA YA UFADHILI WAKIMASOMO NJE YA NCHI NI KWA NGAZI ZA JUU TU ZA ELIMU?

UTANGULIZI.

Katika nchi yetu ya Tanzania na afrika kuna wimbi kubwa la wasomi ambao wanawaza kwenda nje ya nchi kwa mgongo wa scholarship zinazotolewa na nchi za marekani,ulaya na asia.Katika namna yakutafuta elimu ni jambo zuri na halina tatizo kabisa wala si walaumu wanaokwenda huko kutafuta elimu. Lakini jambo la kujiuliza ni kwamba kwanini fursa za ufadhili ni nadra kwa vijana wanaohitaji kusoma astashahada na stashahada?

ELIMU YA MSINGI NI ILE ANAYOIPATA MTOTO AU KIJANA KATIKA MAKUZI YAKE.


Kisaikolojia maarifa na ujuzi wa mtu hujengwa katika hatua za awali za ukuaji wake na sio katika umri mkubwa.Kwa maana nyingine msingi wa mabadiliko yoyote katika jamii msingi wake ni uwekezaji wa elimu na maarifa katika ngazi za chini za kielimu ambako ndiko watoto na vijana walipo.

Wenzetu wameona kutupatia scholarship za uzamili na uzamivu hatuwezi kufanya mabadiliko yoyote ya maana katika nchi zetu kwasababu msingi wetu tangu utotoni ni mbaya.

Wanaelewa kuwa elimu yao ni bora na msingi wao unajengwa kwenye ngazi ya chini ya elimu.Huko ndiko wanapotengenezwa wanasayansi na wabobezi wa teknolojia.

TUMENYIMWA TEKNOLOJIA

Katika ngazi hizi za chini za elimu(diploma na cheti) ndiko teknolojia mpya na ujuzi wa kisasa unapojengwa kwa kijana.Kila siku wenzetu wanaji update katika mitaala yao na kozi zao tofauti na hapa kwetu.Mfano kuna kozi nyingi tu ambazo wenzetu wamezianzisha ambazo sisi hatuna mpaka leo na wenzetu wana karibu miaka kumi tangu wamezianzisha.Kozi kama Robotics and mechanical, drone Pilot, 3D printing wenzetu wako mbali.

Ubora wao upo katika vifaa vya kufundishia, technolojia kama simulation na zingine nyingi zinamfanya mwanafunzi kuwa bora katika taaluma yake tofauti na sisi.

HODARI WA VYETI KULIKO UJUZI

Wazungu wanaelewa kuwa tunatukuza sana vyeti kuliko ujuzi.Wako tayari kukupatia cheti cha uzamivu katika mambo ya kijamii uongozi na utawala lakini sio elimu yakujikomboa na kupiga hatua kwenye teknolojia.

KUTENGENEZWA ILI KUFIKIRIA KAMA WAO

Mara nyingi elimu hizi za juu hazitujengi kwenye ubunifu.Siku zote zinatujengea kufikiri sawa na wengine.Sehemu kubwa unajifunza kuhoji kwa kufanya rejea ya kutoka sehemu Fulani.Mawazo mengi ya wasomi wa namna hii ni kulinganisha mambo na sehemu Fulani au takwimu Fulani.Hakuna wazo jipya analoweza kuwaza msomi wa namna hii isipokuwa lile aliloona katika nchi Fulani au kusoma katika vitabu Fulani.Tunakuwa watumwa wa mawazo ya watu wengine ambao mazingira na utashi wa watu wao ni tofauti kabisa.

Tumekuwa tunalinganisha mambo ndio maana tunakwama.Tuna copy na ku paste kila kitu kwa usemi wananchi Fulani walifanya hivi na vile wakafanikiwa.Hili ndio linaloharibu hata mifumo ya elimu yetu kwa kuingiza mambo ambayo kwa uhalisia mazingira ,uelewa na miundo mbinu haisapoti.

Mfano baadhi wanasema tuachane na kiingereza kama somo la kufundishia tuende na Kiswahili hadi chuo kikuu kwa sababu eti wachina mbona wanatumia kichina na wameendelea.Hii ni kukopi na kupesti.Hali ya siasa za china na historia yao mpaka kufika hapo walipita katika wakati mgumu wa kijamaa wakati ambapo utandawazi haukuwa kama hivi sasa.

Ndio maana watu walioleta mapinduzi katika nchi zao kwa sehemu kubwa hawakukopi mawazo ya wengine .walitengeneza mifumo yao ya kiutawala na kielimu kulingana na nchi zao na kama walikopi kutoka kwingine basi waliiboresha ili iendane na nchi zao.lakini wasomi wetu wanaokwenda kusoma nje nakupata vyeti vikubwa vikubwa tumeshindwa hata kuandika vitabu vyenye kuleta chachu katika nchi yetu.

SCOLARSHIP NI UTALII

Kitendo cha kwenda kusoma kwenye mataifa yao ni kuongeza utalii.Utalii wa kimasomo ni maarufu kwa wenzetu kwasababu wanajua kitendo cha wewe kuwepo katika nchi yao wananufaika kwa pesa yao kubaki kwao lakini pia ni njia yakuwaleta wengine katika nchi yao na uchumi wao kuendelea kukua.
TUBORESHE ELIMU YETU KATIKA MISINGI YA CHINI KWA VIJANA NA WATOTO HAO NDIO WANAMAPINDUZI WA BAADAYE
 
Back
Top Bottom