Kwanini Fulana za CCM Zinavaliwa na Walalahoi tu huku mtaani kwetu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Fulana za CCM Zinavaliwa na Walalahoi tu huku mtaani kwetu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ng'wanangwa, Dec 29, 2010.

 1. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  sote tunakumbuka vile ccm walikuwa wakijipamba kwa mafulana yao ya kijani na makofia kipindi cha uchaguzi. tena wale wenye uwezo kifadha. ndiyo yalikuwa mavazi yao ya kuvaa hata maofisini.

  baada ya uchaguzi kuisha sasa naona huku mtaani kwetu watu wanaovaa mavazi haya ya chama ni wale wenzangu-na-mimi wasiojua hata watakula nini. yaani wale wanaoishi maisha ya kila kukicha ni afazali ya jana.

  sioni tena watu wenye magari yao na majumba ya mamilioni huku mtaani wakijipamba na mavazi haya ya chama tawala.

  hii ina maana gani?
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  kwa mfano:

  mama mmoja nilipanda naye daladala alikuwa amefunga kiremba cha ccm kichwani lakini nauli ilikuwa haitosh.

  akaanza kuzozana na konda. mtu wa chama tawala anazozana na konda.

  ndiyo maisha bora?
   
 3. L

  LAT JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  that is a great observation..... hata makada wakubwa wa CCM hawavai hizo T-Shit .... its a symbol of shame and cowardliness..
   
 4. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wanaondelea kuvaa hizo tshirt na kofia waangalie wote wanaonekana wana akili mbovu
   
 5. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2010
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280  Mimi kwenye facebook status yangu ya leo nimetoa angalizo, asije mtu akathubutu kuja kunikopa pesa eti ili amlipie mtoto wake ada ya shule, maana Dr Slaa aliahidi elimu bure na matibabu bure, na utafiti wangu unaonesha wanawake waswazi na majuha ndio mtaji muhimu wa ccm, sasa mimi nasubili mwezi January nione wanavyohadhirika na naapa mwaka ujao sina msaada na majitu mazezeta. mimi binafsi nimeshafunga mkanda na nitapambana na hiki kibano cha mkwere na genge la wahuni wenzake. siku zote kwenye vita vya haki ushindi ni lazima its a matter of time.
   
 6. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #6
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 852
  Trophy Points: 280
  Hawana uwezo wa kununua nguo ila wanauwezo wa kuchagua ccm kweli wa tz tuna safari ndefu! Na hizo nguo zitawagharimu for 5 yer...lol
   
 7. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #7
  Dec 29, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,649
  Likes Received: 4,751
  Trophy Points: 280
  Mtaji wa CCM ni umasikini na ujinga wa watanzania.
   
 8. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #8
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  hahahahahahah! umenichekesha sana hapa nilipo sina mbavu wangu! halafu uzuri wa hawa jamaa bakora zao zinatunyuka wote kuazia aliyekuwemo na asiyekuwemo.
   
 9. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #9
  Dec 29, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,795
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  GreatThinkers,

  Umaskini wa watanzania ni Mtaji wa CCM na ndiyo maana hawataki kusikia wa utawala wa majimbo.

  Ujinga kwa watanzania ni Capital ndani ya CCM hivyo ndo maana hadi leo kuna shule za kata bila walimu

  Ona hata leo, wajinga na Maskini hawajui athari gani watapata iwapo umeme utapanda bei, kisa wanaishi vijijini hawatumiii umeme. Wamesahau bei ya kiberiti nayo itapanda au itabaki pale pale!

  Ndo maaana nasema kila siku "Tanzania ni Shamba la Bibi la Mafisadi"
   
 10. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #10
  Dec 29, 2010
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  Naona huu uzi ni wa watu wenye hasira kali. Hebu niwape ushauri. Hao walalahoi wanaoendelea kuvaa hizo fulana, vitenge, kofia, n.k. wamefikishwa hapo baada ya miaka mingi ya kudumazwa kifikra. Hawajui au hawaamini kama kuna namna mbadala ya kuboresha maisha yao zaidi ya kutegemea fadhila za msimu za wenye nchi. Hivyo kuweni na imani kidogo; wapeni elimu tartiibu, huenda wakazinduka siku moja! :bounce:
   
 11. M

  Mnyalu wa Kweli JF-Expert Member

  #11
  Dec 29, 2010
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 233
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Matola umenifurahisha sana. Siku moja nilikuwa napata moja baridi moja moto katika bar moja na jamaa yangu.Ghafla akapita ombaomba ambaya hana kasoro yoyote, hapa namaanisha hana ulemavu wowote. Lakini cha kushangaza ombaomba yule alikuwa kavaa T.shirt ya CCM. Basi baada ya yule beggar kufika kwenye meza yetu yule jamaa yangu akamwambia yule ombaomba kuwa aende akaombe kwa mtu aliyempatia ile T'shirt. Was that the correct act Comrade Matola?
   
 12. n

  nyantella JF-Expert Member

  #12
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  It is true common sense is not always common!

  Hivi unafikiri kama nauli tu hana, huoni kwamba anaweza asiwe na uwezo kuwa na nguo nzuri zaidi and the best clothes zinaweza kuwa hizo alizovyaa? mwache avae ana uhuru wa kuvaa nguo yoyote inayo msitiri maungo wewe kina kuuma nini na kwani yeye ndiye aliyetoa hiyo slogan? think good before unaleta threads za rangi hii!
  kumbuka hata US kuna masikini wa kutupa.
   
 13. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #13
  Dec 29, 2010
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280


  Hii nadhani ilikuwa ni difference kesi, wengi wanaovaa hizo fulana ni kwa ajili ya kujisitili tu, kwa hiyo yeye kama huwa ana kawaida ya kuwasaidia ombaomba pesa basi angewapa tu. ila mimi binafsi sina huo utamaduni wa kuwapa pesa omba omba.
   
Loading...