Kwanini friji langu limepungua uwezo wa kugandisha au kupoza haraka? Naombeni msaada

Tupa nunua jingine, sikuhizi yapo mpaka ya laki 3, usilipeleke kwa fundi tafadhali maana likipona lutaongeza hewa ukaa angani.
Huu ndio ushauri mzuri, safi sana, tupa au mbabatize mtu hata kwa alf 50, nunua lingine..yako mpaka laki 2 na nusu...
 
Kwa hiyo litafanya kazi yake kama zaman au inakuwaje hapo bosi? Je kuhusu matumizi makubwa ya umeme yanaweza pungua? Au
Natumahi matumiz yatapungua kwan nami ilikuwa hivyo nilikuwa natumia 3 units kwa SAA 24.means 90 units kwa mwezi
 
Kujaza gesi ni suala jepesi sn na gharama ni kuanzia 20 but nilipokuambia 50 nilimaanisha ni funding ambaye ataanza na kutafuta tatizo then atajaza na kukupa dhamana na hata ushauri muafaka.
 
Sijaona mtu aliyetoa jibu la kukata kiu yako ya kufahamu chanzo cha friji lako kukata gesi haraka.. jibu zuri ni kwamba, wanaouza mafriji used huwa wanatoa mitungi halisi iliyokuja na friji kisha wanaweka feki.. ukinunua friji dukani, hilo tatizo la mtungi kuisha gesi utaliona baada ya miaka saba au zaidi.
kweli usimhukumu mtu kwa kumwangalia usoni, mkuu kwa hii sura hapo kweny avatar sikutarajia utoe jibu na ushaur murua kama huu,
Asante umenisaidia na mimi
 
Mnadanganyana, kuna friji imenizidi umri huwa inapuliziwa rangi tu, haijawahi kuisha gas, hakuna kitu kuisha gas sema kuna leakage kwa pipes, tafuta fundi azibe halafu akujazie gas.
 
Evaporator ya friji yangu niliitoboa kizembe naomba kujua kuna namna yoyote ya kuiziba.
?
Ni material ya alluminium,je inaungika
Hakuna material ya kuziba evaporator ikitoba,..utakutana na fundi njaa atakuzibia kwa kutumia super glue na unga but hatadumu muda mrefu coz pressure ya gas ni kali sana so lazima ivuje tena but km inaweza kutoka ndani ya fridge unaweza kuichoma kwa kutumia aluminium stick na ikawa poa
 
Hiyo ni gas tu imepungua kama friji inafanya kazi kawaida ila haigandishi ni gas tu akajaze mtungi kitu na boksi. hapo utakuwa umemsadia kiufundi na sio mengine =D =D
Kwa kifupi gas huwa haiishi kweny kifaa chochote kinachotumia gasi I mean Ac,.car Ac, refrigerator nk otherwise iwe ina leak na ukiona imeisha jua ina leak somewhere so lazima uzibe leak ndo u refill
 
Mitungi original huwa inakuja na friji ambayo mingi huaribika safarini.. ukitaka ya kununua utauziwa kama huo uliokuwa nao.. dawa kununua friji dukani other wise uzoee kuongeza gesi kila mwezi.
Kweny fridge hakuna kitu kinaitwa mtungi ila sema compressor, na gas kweny fridge huwa haiishi na ukiona imeisha jua ina leakage sehemu,.. Na pia fridge kutogandisha sio mpk iwe gas inawezekana ikawa tatizo lingine like compressor haitembei au relay au overload mbaya so ni vizuri muite fund akuchekie
 
Mitungi original huwa inakuja na friji ambayo mingi huaribika safarini.. ukitaka ya kununua utauziwa kama huo uliokuwa nao.. dawa kununua friji dukani other wise uzoee kuongeza gesi kila mwezi.
Gesi kila mwezi?? Hiyo sio friji sasa...
 
Back
Top Bottom