Kwanini French speaking African nations ndio zina vita tu?

Nafikiri hitimisho ni kuwa mataifa yote hayo yana madini mengi na yote ukiangalia wana dhahabu, almasi na uranium pamoja na copper
Wazungu waligawana mataifa yetu ili wanyonye rasilimali zetu ila kidogo waingereza wana heshimu kidogo utu kuliko wafaransa na wabelgiji
Wafaransa wao mbinu za kuchonganisha bado wanaendeleza mpaka sasa
Nimeangalia nchi zote hizo zimeshiba madini na ndio chanzo cha kuwachonganisha ili waibe kiulaini

Wanatengeneza waasi na kuwapa silaha huku wakijifanya urafiki na serikali
 
mchungu lakin n ukwel... Bufa

Na ujinga ni mzigo, fanya uutue

Congo:
Capture.JPG

CAR
Capture.JPG

Mali
Capture.JPG

Siera Leone

Capture.JPG

IVORY COAST

Capture.JPG

Nyengine utatizama mwenyewe. Mwambie na huyo Bufa aone mapadre walivojazana. Na asisahau kusema kuwa mtu mweusi pia ni tatizo (According to his/her logic) mana wapo wengi huko na ndio wanaopigana
 
Mwingereza aliisha iba vya kutosha na kuondoka
Lakini mfaransa bado anaona ni haki yake na kuweka mapigano kila kukicha huku akiiba rasilimali zao.

Sent from my SM using Tapatalk
ktk documentary za civil wars nlizoziona nyingi zimeshabiana hoja yako,kuna baadhi ya mataifa hayakuridhika na kutupa Uhuru wetu hivyo hawakuondoka mazima bali walijitahidi kuacha influence yao kisiasa na kiuchumu ktk makoloni yao hivyo uongozi ambao ungeonekana kukinzana na interest zao walijitahidi kuiyumbisha serikali kwa namna yoyote ile either coup de tat,civil wars au kulitumia taifa jirani kuangusha utalawala au kudumaza utawala MF Afrika ya Kati wananchi wanadai viongozi wote ni mapandizi ya Ufaransa na hata Yale machafuko ya miaka ya 2014 yalitenezewa taswira ya uhusika wa chad ila kiuhalisia Chad alitumika na Ufaransa
 
Mapinduzi na vita ni vitu viwili tofauti zingatia hilo mkuu,Mapinduzi hayaitaji uwekezaji mkubwa tofauti na Mapinduzi ambayo yanaweza isha pasipo kumwagika damu ila vita inaitaji misingi imara maana unapigana na mhimili mzima wa serikali au jamii
Kwanza, fahamu kwamba Sierra Leone sio French Speaking ni English Speaking kwani ilikuwa ni Imperial British Colony.

Haya mataifa ya "La Francophonie" yana historia ya kuwa na majeshi yasiyo na nguvu sana na yamekuwa yakiitegemea sana Ufaransa kiulinzi tofauti na mataifa yaliyotawaliwa na Uingereza.

Lakini pia usisahau mapinduzi ya kijeshi nchini Nigeria, Ghana, Sierra Leone, The Gambia na Uganda na hata majaribio ktk nchi kama Tanzania 1964 na 1982; Kenya 1982; Zambia 1990.
 
Nafikiri hitimisho ni kuwa mataifa yote hayo yana madini mengi na yote ukiangalia wana dhahabu, almasi na uranium pamoja na copper
Wazungu waligawana mataifa yetu ili wanyonye rasilimali zetu ila kidogo waingereza wana heshimu kidogo utu kuliko wafaransa na wabelgiji
Wafaransa wao mbinu za kuchonganisha bado wanaendeleza mpaka sasa
Nimeangalia nchi zote hizo zimeshiba madini na ndio chanzo cha kuwachonganisha ili waibe kiulaini

Wanatengeneza waasi na kuwapa silaha huku wakijifanya urafiki na serikali
You are right! hata Rwanda mbelgiji aliwachonganisha wahutu na watutsi, hadi leo ile chuki iliyopandikizwa na mkoloni haijatoka.
 
You are right! hata Rwanda mbelgiji aliwachonganisha wahutu na watutsi, hadi leo ile chuki iliyopandikizwa na mkoloni haijatoka.

Halafu mbaya zaidi waliwafundisha namna ya kumalizana bila kutumia risasi sana bali kisu
Walikuwa wanakatana mshipa mkubwa wa juu ya kisigino na huwezi kutembea na kufa haraka
Yaani kila nikikumbuka Yale mauwaji nasema binadamu unaweza kutumia na kuuwa ndugu zako hivi hivi
 
Mapinduzi na vita ni vitu viwili tofauti zingatia hilo mkuu,Mapinduzi hayaitaji uwekezaji mkubwa tofauti na Mapinduzi ambayo yanaweza isha pasipo kumwagika damu ila vita inaitaji misingi imara maana unapigana na mhimili mzima wa serikali au jamii
Naona hata hunielewi. Unaongea vitu vingine kabisa.
 
Hapa inabidi ujiulize swali moja ni nani anasababisha vita middle east hadi kesho jibu ni US kwa kutumia magaidi wa kiarabu (mfano IS). Swali la pili je ni nani aliongoza vita ya kumuondoa gadafi kwa kutumia waasi jibu ni US(obama alishawahi kusema anajutia kufanya hivyo) . Swali la tatu je ni machafuko ya aina gani yaliyopo kwenye hizo nchi za francophone ni machafuko kati ya serekali dhidi ya wanamgambo wa kiislam wanao fungamana na IS au ni IS wenyewe, tumeskia IS saiv wapo mali, burkina faso, congo, msumbiji na nchi zinginezo kwa hiyo jibu lipo wazi mbinu walizotumia us middle east wakafanikiwa sasa wanazileta africa ili waendelee kutawala dunia
 
Back
Top Bottom