Kwanini familia za nchi zilizoendelea hazina wasaidizi wa kazi za nyumbani (house girls)?

Kwanza kule wanalipwa kwa saa sio kwa mwez kama huku.

Pili mfanyakaz anakuwa na haki zote sawa sawa na mfanyakaz aliopo serikalin kuanzia bima nk.

Tatu privacy: kule swala la faragha linazingatiwa sio kama huku housegirl unambananisha chumba kimoja na vitoto.

Mazingira pia uchangia
 
Maid wa Tanzania ni rahisi sana jaman.... Mfano hawa dada zetu wanaofanya kazi kwa wahindi doooooh huruma tena huruma jamani na hawana wa kuwasemea

Just imagine kazi kuamzia saa 12 asbh mpak 12 jioni mshahara wa mwezi 70,000/= ila kutokana na hali harisi ya uchumi wa Tanzania haina budi watu tunagombania vibarua hivyo hivyo

Kwahiyo mi nafikiri ni urahisi wa house maids ndio unaotofautisha uhitaji kati yetu na nchi zilizoendelea hapa kwetu imekua ni badhaa rahisi sana isiohitaji mambo mengi kumiliki wewe ni kupiga simu tu kijijini anakuja.
 
Nimekuwa nikitafakari kwa muda sasa.
Kwanini familia za waafrika bila dada wa kazi au housegirl mambo hayaendi?

Mke atalalamika, nyumba itakuwa chafu, chakula hakitaiva kwa wakati yaani mambo yote yatakuwa vurumai.

Lakini ukiangalia wenzetu walioendelea familia nyingi ni baba,mama na watoto na wote wanajituma katika majukumu yao.
Ni familia chache za matajiri sana wenye mansions ndio utakuta kuna maids.

Je ni uvivu?
Je ni kwasababu wanapatikana kwa bei chee?

Ni tabia zetu tu kupenda ubwanyenye?

Labour is too expensive Mzee. Sheria za ajira imekaza na kusimamia kila sekta kiasi kwamba mtu hawezi kujiamulia kiasi anachomlipa mtumishi.

Mfano, mtu mfagizi akija kufagia na kufanya usafi, itabidi umlipe kwa saa mshahara ambao umewekwa kisheria labda 10€ kwa saa, maana yake ni kwamba akifanya kwa masaa nane, 80€ zonal doka alafu bado muajiri utachangia bima ya afya, mafao ya uzeeni na mengine.

At the end of the day, inakuwa ghali mno kwako, hii ndiyo maana Ulaya kila kitu kinafanywa ma mashine, kufua, kufagia, hata jikoni, mashine zinatumika ili kupunguza uzito mtu akifika nyumbani.

Sasa kwa mazingira hayo, siyo rahisi kuwa na mtumishi wa ndani. Wanachofanya ni kununua huduma hizo mara moja moja kutoka kwenye makampuni ya usafi na huduma nyingine kama hizo.
 
Mwishoni mwa Uzi wako umeuliza
Mashine za nguo zimeanza lini? Sasa nei ya sufuria na mshahara wa house girl si bora kununua sufuria?
Je ni uvivu?

Ndo jibu linakuwa sio uvivu Bali uwezo wetu Dunia kwakuwa tunategemea mkaa kupika chakula pia tunatumia masufuria dhaifu na kufua nguo kwa mkono.
 
Mwishoni mwa Uzi wako umeuliza

Je ni uvivu?
Ndo jibu linakuwa sio uvivu Bali uwezo wetu Dunia kwakuwa tunategemea mkaa kupika chakula pia tunatumia masufuria dhaifu na kufua nguo kwa mkono.

Gesi na umeme vimeanza kutumika lini? Kabla ya hapo hao wazungu walikuwa na housegirl?
 
Mwingingine ni uduwanzi tu

Imagine nmetoka kuoa tu na tuna miezi mitatu tu kwenye ndoa , maisha bado vurugu vurugu yan hadi bado madeni mengine ya harusi hatuja clear... Halafu wife analilia mfanya kazi na yeye ni mama wa nyumbani.. Kidume nkakaza kwamba hapana hiyo kitu haiwezekani hilo wazo la mfanya kazi lifte kabisa...

Mara ghafla mtu hodi mlangoni na mashangazi kaja mawili safari ya kuvuka mikoa mitatu na nauli kalipiwa na dada ake wife yani shemeji angu... Haloo huyu binti anapiga kazi balaa...

Ataamka mapema atafanya usafi, atapika chai mapema, maji anafata, chakula anapika kwa wakati japo quality inapungua ukilinganisha na anavyopika wife... yani hapa nawaza nmtimue yeye au nmtimue wife Na ni lazima mmoja atimkie mbali fumbafu
 
Kwa kweli wife ambaye ni mama wa nyumbani ambaye hana mtoto wala siyo mjamzito, kutaka msaidizi ni uvivu tu. Halafu ndoa mwanzoni inapendeza mkiwa wawili tu nyumbani. Hiyo ya kuoa kwenye honeymoon tayari mko 3-5 nyumbani inakosesha raha ndoa.
Mwingingine ni uduwanzi tu
Imagine nmetoka kuoa tu na tuna miezi mitatu tu kwenye ndoa , maisha bado vurugu vurugu yan hadi bado madeni mengine ya harusi hatuja clear... Halafu wife analilia mfanya kazi na yeye ni mama wa nyumbani.. Kidume nkakaza kwamba hapana hiyo kitu haiwezekani hilo wazo la mfanya kazi lifte kabisa... Mara ghafla mtu hodi mlangoni na mashangazi kaja mawili safari ya kuvuka mikoa mitatu na nauli kalipiwa na dada ake wife yani shemeji angu... Haloo huyu binti anapiga kazi balaa... Ataamka mapema atafanya usafi, atapika chai mapema, maji anafata, chakula anapika kwa wakati japo quality inapungua ukilinganisha na anavyopika wife... yani hapa nawaza nmtimue yeye au nmtimue wife Na ni lazima mmoja atimkie mbali fumbafu
 
Ulaya ukitaka maid unamlipa mshahara kama mfanyakazi wa serikali au sekta binafsi ana haki zote Hadi mafao,..so wachache wanamudu kuwaajiri...sio kama huku kwetu unamtupia ka hamsini flani kwa mwezi..
Elfu hamsini alaf maza house hampi yote anaambiwa anawekewa siku ya kuondoka anapewa yote 😆😆😆😆
Haka katabia wamama wengi wanacho sijui kwann
 
Hizo familia zilizoendelea hawatumii mkaa kupika Wala masufuria dhaifu ya aluminum yanayopoteza mvuke.

Pia hawafui nguo kwa mikono, Wala hawaendi umbali mrefu kutafuta maji.
na wakitoka asubuhi wanapakia watoto wanawaacha shule au basi linawachukukua na kuwarudisha.

huku ili nitoke chamazi hadi town inabidi nitoke saa kumi kuwahi daladala na foleni.

tunapoambiwa sisi ni dunia ya tatu mleta mada ajilinganishe wa kufanan nae ila sio dunia ya kwanza
 
Back
Top Bottom