Kwanini familia za nchi zilizoendelea hazina wasaidizi wa kazi za nyumbani (house girls)?

singojr

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
5,184
6,595
Nimekuwa nikitafakari kwa muda sasa.

Kwanini familia za waafrika bila dada wa kazi au housegirl mambo hayaendi? Mke atalalamika, nyumba itakuwa chafu, chakula hakitaiva kwa wakati yaani mambo yote yatakuwa vurumai.

Lakini ukiangalia wenzetu walioendelea familia nyingi ni baba, mama na watoto na wote wanajituma katika majukumu yao. Ni familia chache za matajiri sana wenye mansions ndio utakuta kuna maids.

  • Je ni uvivu?
  • Je ni kwasababu wanapatikana kwa bei chee?
  • Ni tabia zetu tu kupenda ubwanyenye?
 

mbenda said

JF-Expert Member
Apr 13, 2019
967
1,825
Baba huwa anaushawishi mkubwa wa kuleta msaidizi ili asaidie kazi za mama akiwa amesafili,

Waza hii mdada wa kazi baada ya kumaliza kazi aliingia chumbani kwa bosa wake ,akasema cjawai lalia kitanda kama hiki ngoja nijaribu akawa ac akajifunika shuka akalala akapitiwa na ucngizi.

Kumbe baba na mama wamegombana cku ya 3 hawaongei, baaada ya muda baba amerudi akapitiliza hadi chumbani akakuta mtu amelala kitandani akajua ni mkewe na kwaku alikuwa na ugomvi na mkewe wala hakumsemesha nae akapanda kalala

baada ya muda mama wa nyumba amerudi kufika chumbani akakuta baba na dada wa kazi wamelala kutandani walipoamshwa kila mmoja anashangaa nn kimetoka, ndio ukaambiwa boss ameamaka chumba kwa hous gerl huku kwetu mwana shamba kaja na baiskeli sheli
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,037
211,145
Kabla hujaajiri mfanya kazi wa ndani Ulaya ni lazima uthibitishe una uwezo wa kumlipa kima cha chini na mshahara, utampa malipo yake kama kawaida akiwa mgonjwa, utampa likizo ya mwezi mmoja kwa mwaka yenye malipo.

Shift itakua masaa nane na zaidi ya hapo umlipe over time. Atafanya kazi siku tano kwa wiki na weekend na usiku malipo yanaongezeka kwakua anafanya untisocial hours.
 

nasrimgambo

JF-Expert Member
Jan 10, 2017
1,579
1,985
Nimekuwa nikitafakari kwa muda sasa.
Kwanini familia za waafrika bila dada wa kazi au housegirl mambo hayaendi?

Mke atalalamika, nyumba itakuwa chafu, chakula hakitaiva kwa wakati yaani mambo yote yatakuwa vurumai.

Lakini ukiangalia wenzetu walioendelea familia nyingi ni baba,mama na watoto na wote wanajituma katika majukumu yao.
Ni familia chache za matajiri sana wenye mansions ndio utakuta kuna maids.

Je ni uvivu?
Je ni kwasababu wanapatikana kwa bei chee?

Ni tabia zetu tu kupenda ubwanyenye?
Usione maisha ya kwenye tv ya huko Ulaya ukafikiri ndio hivyohivyo

Kwanza, wanao hao wafanyakazi (kama kweli wanaishi kwenye mamansions)

Pili, si kila tajiri wa huko ulaya anaishi katika majumba yenye nafasi wengi wanaishi kwenye apartment juu ghorofani, nafasi ni ndogo, wafanyakazi wao ni wale wa kuja na kuondoka

Tatu, maseries na muvi ni maseries na muvi sio maisha halisi ya huko
 

Logikos

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
9,456
14,549
Cheap Labor

Hata hao wakija huku wanaweza kuajiri kijiji kizima...,

Ni opportunity Cost kwa mama kutafuta baby sitter huenda ikawa gharama bora yeye na mwenza wake wapeane shift mmoja afanye kazi usiku mwingine mchana (huenda per hour huyo mtu anapokea sawa na baby sitter per hour)
 

singojr

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
5,184
6,595
Ulaya ukitaka maid unamlipa mshahara kama mfanyakazi wa serikali au sekta binafsi ana haki zote Hadi mafao,..so wachache wanamudu kuwaajiri...sio kama huku kwetu unamtupia ka hamsini flani kwa mwezi..

Halafu tunalaumu wahindi kutupa mishahara midogo
 

singojr

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
5,184
6,595
Usione maisha ya kwenye tv ya huko ulaya ukafikiri ndio hivyohivyo

Kwanza, wanao hao wafanyakazi (kama kweli wanaishi kwenye mamansions)

Pili, si kila tajiri wa huko ulaya anaishi katika majumba yenye nafasi wengi wanaishi kwenye apartment juu ghorofani, nafasi ni ndogo, wafanyakazi wao ni sale wa kuja na kuondoka

Tatu, maseries na muvi ni maseries na muvi sio maisha halisi ya huko

Nani kakuambia nimeona kwenye series na movie?

Wabongo wangapi wamepanga vyumba viwili na housegirl analala sebuleni?
 

Dr Dre

JF-Expert Member
May 23, 2015
2,518
2,494
Nina sista angu mmoja huya ana house girl na hana kazi yoyote ye kulala tu na kwenda viwanja kazi zote anafanya house girl.

mtoto wake wa kike naye amekua hata kujifulia hafui house girl atafua
 

InvisibleTarget

JF-Expert Member
Dec 20, 2014
990
1,823
Kabla hujaajiri mfanya kazi wa ndani Ulaya ni lazima uthibitishe una uwezo wa kumlipa kima cha chini na mshahara, utampa malipo yake kama kawaida akiwa mgonjwa, utampa likizo ya mwezi mmoja kwa mwaka yenye malipo. Shift itakua masaa nane na zaidi ya hapo umlipe over time. Atafanya kazi siku tano kwa wiki na weekend na usiku malipo yanaongezeka kwakua anafanya untisocial hours.
Huyo namsajili awe ndugu kabisa
#nabaki Tanzania
 
12 Reactions
Reply
Top Bottom