GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,516
- 108,791
Kuna Mzazi (Masikini au Mnyonge) Mwenzangu Chumba cha Pili tu nimetoka kumuamlia asimchape mwanae kwakuwa hajui Kiingereza huku akimwambia kuwa ni bora Afeli masomo yote ila siyo Kiingereza ambacho kwake ndiyo Ishara Kuu ya Mtu Msomi.
Cha kushangaza sasa huyu huyu Mwanae asiyejua vyema Kiingereza na kinampiga Chenga ni Bingwa wa Masomo ya Hesabu, Kemia, Fizikia na Jiografia kiasi kwamba hata Wanafunzi wengine huja Kufundishwa nae hapa Kwao na wanamkubali ile mbaya.
Hata Wanawake (Mademu) zetu wa 'Kiswahili' hasa wa huku Kwetu kwa Wanyonge (Masikini) ukithubutu tu Kuwatongoza kwa Kiswahili na siyo kwa Kiingereza si tu kuwa Wanakucheka bali wanasema Wewe si Msomi.
Ni kwanini Masikini tuna Ushamba mno?