Kwanini Ethiopia nchi masikini kuliko sisi, wanatuzidi sana kwa kasi ya maendeleo?

Synthesizer

Platinum Member
Feb 15, 2010
11,316
19,198
NI ajabu sana. Ukilinganisha Ethiopia na Tanzania, tunawaacha kwa rasilimali vibaya sana, hasa ukizingatia dhahabu, gesi, mbuga za wanyama na vivutio vingine, ardhi inayolimika, maji safi (fresh water), mito, bandari nk. Lakini kitu cha ajabu, ksi ya kukua kwa uchumi na maendeleo ya Ethiopia ni ya ajabu ya kutisha, japo wanasemekana ni masikini kuliko sisi Watanzania.

Leo hii, kwa jinsi Addis ilivyojengwa na kupanuka, kutia ndani barabara zake, huwezi kulinganisha hata kidogo na Dar. Sisi tunahangaika na flyover ya Tazara wakati Addis flyovers sasa ni kitu cha kawaida, na hata wameanza kutandika njia za treni za mjini zitakazotumia umeme, ambazo kwa sehemu ya mjini zinapita juu kwa juu! Kwa hiyo soon Addis itakuwa mojawapo ya majiji ya Africa yenye trams.

Na cha ajabu ni kwamba, contract zote hizi za ujenzi wa barabara na reli zinafanywa na Wachina, ambao wanajenga kwa kiwango cha juu cha ajabu. Wachina wakiulizwa mbona wanajenga reli na barabara kwa kiwango cha juu sana Ethiopia tofauti na nchi nyingine, wanajibu kwamba Ethiopia hakuna rushwa na ubabaishaji wa viongozi wa serkali!


Ethiopia-Railway-Project.jpg

Addis train projectMaongezeo ya thread

Nimetafakari sana juu ya hili, nikagundua tatizo letu liko wapi tukijilinganisha na Ethiopia. Imebidi nitafakari yale aliyosema Nyerere miaka mingi iliyopita, ndio nikagundua ni wapi tunakwama. Huyu mzee alikuwa na busara sana, na mambo mengine ni rahisi kuona ukitafakari kauli zake leo hii.

Nyerere alisema tukitaka nchi yetu iendelee inahitaji mambo makuu manne, ambayo nitayatumia kujilinganisha na Ethiopia, kama ifuatavyo;

1. Ardhi - ambayo tunayo tena nzuri kuliko ya Ethopia, ina madini, gesi kwa wingi, maziwa, bahari, milima ya kuvutia, ardhi yenye rutuba, mbuga za wanyama nk

2. Watu - Watanzania wenyewe; je tunazidiwa uzalendo na tabia ya kujituma kazi kama Wa-Ethiopia? Sisi sio wachapakazi, wazalendo wa nchi yetu, kama Wa-Ethiopia?

3. Siasa safi - yaani policy framework. Je, CCM inatupa sera ambazo hazitupeleki popote? Sera za Ethiopia ni nzuri zaidi ya zile za kwetu?

4. Uongozi bora - hapo sina la kusema, labda wenzangu nisaidieni kujilingnisha na Wa-Ethiopia, maana viongozi wetu mnawajua, ndio hao tena wengine wachapa kazi, wengine hawajagundulika bado maovu yao, wengine wanajiuzuru, wengine wanagoma kujiuzuru, wengine wana kesi mahakamani, nk
 
Ni nani aliyekudanganya kwamba Tanzania tuna Rasilimali nyingi kuizidi Ethiopia? Ulipaswa uulize ni kwa nini Ethiopia wana maendeleo au wanakwenda vizuri kuliko Tanzania? lkn SIYO kusema ya kwamba tuna Rasilimali nyingi kuwazidi hilo SIYO kweli!
 
Huwezi kuamini nimesoma title tu nikaamua kuchangia maana jibu ninalo muda mrefu.
Ethiopia wamepata viongozi wenye uchungu na nchi yao na wanaelewa kwa nini nchi yao ni maskini. Rushwa imethibitiwa kwa kiasi kikubwa. Hawana Richmond, EPA wala IPTL. Kule akina Sethi hawana nafasi
 
Nimesoma mahali kwamba financial year ya 2009/2010 Ethiopia waliuza nje bidhaa zenye thamani ya Us $ 1.4 Billion wakati sie hapa tumekazana tu na maslogani.. Eti kilimo kwanza..
 
Tuvute subira. Hata Malaysia miaka 50 iliyopita ilikuwa kama sisi lakini sasa ni moto wa kuotea mbali!
 
Ni nani aliyekudanganya kwamba Tanzania tuna Rasilimali nyingi kuizidi Ethiopia? Ulipaswa uulize ni kwa nini Ethiopia wana maendeleo au wanakwenda vizuri kuliko Tanzania? lkn SIYO kusema ya kwamba tuna Rasilimali nyingi kuwazidi hilo SIYO kweli!

naomba Unijibu Kwanini ETHIOPIA wana Maendeleo Kutuzidi?
 
Halafu jamaa hawaruhusu wawekezaji wa kigeni zaidi ya Wachina walioshika tender za ujenzi, km sio raia ni marufuku kufanya biashara Ethiopia, hata kampuni ya simu ipo moja tu na inamilikiwa na serikali 100%. Kiasi kikubwa uchumi wao unategea sana kampuni ya ndege, (Ethiopia Airlines)
 
umaskini ni imani....iliyopandikizwa na chama cha mapinduzi
'hiki cha sasa' ccm
 
Ni kweli Ethiopia hawana viongozi wezi na wala nchi yao haiongozwi kwa namna ambavyo sisi tunaiendesha nchi yetu. Pili wananchi ni wachapa kazi sana na wanaipenda nchi yao. Tatu misaada ya kujenga miundo mbinu wanaipata kama sisi ila wao wanaitumia inavyotakiwa.Nne wanazalisha bidhaa zao na kuziuza kwa fedha yao inayoitwa Bir ukiwa na dollar zako hawakupapatikii na wala hawakuuzii bidhaa mpaka uzibadilishe kuwa Bir tofauti na sie hatuzalishi ila tunaishi kwa kuagiza vitu nje
 
Chanzo cha umaskini kwa nchi yoyote ile ni:-

Uongozi mbovu wa nchi. (hii ndo sababu kuu kuliko zote).
 
Back
Top Bottom