Unachosema ni sawa lakini siamini kuwa DPP haelewi haya unayoyasema. Kinachowasumbua wenzetu tuliowapa mamlaka ya kusimamia haki ni kuwa wamelewa mvinyo wa madaraka ambao mning'inio (hangover) wake ni mgumu sana kuuondoa. Hawana tofauti na Ghadafi ambaye mpaka sasa anaamini kuwa atashinda vita pamoja na kuwa dalili zote zinaonyesha kuwa ameshindwa tayari na kinachosubiriwa ni kumkamata tu na kumpeleka mahakamani.
Haapo umenena sawasawa..Taabu siyo kutokuwepo sheria na taratibu; taabu ni ni hawa watendaji wetu....WAMELEWA MADARAKA KIASI WANASAHAU AU MAKUSUDI KABISA majukumu yao na taratibu husika zinazotakiwa kufuatwa KISHERIA...