Uchaguzi 2020 Kwanini Dkt. Magufuli anakwepa mdahalo wa ana kwa ana?

Toxic Concotion

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
5,667
20,357
Inawezekana ikawa sikubaliani moja kwa moja na kila analolihubiri Tundu Lissu ila kwa kiasi kikubwa naheshimu sana uwezo wake wa kujenga hoja. Zaidi ya mara moja Tundu Lissu ameomba mdahalo na mgombea wa CCM ambae ndie rais lakini ombi hilo ni kama vile Bw. Magufuli hajalisikia, ila nina yakini kalisikia maana hoja nyingine za Lissu amejaribu kuzijibu kwenye kampeni zake.

Siku zote njia ya kumkamata mtu muongo (Lissu ni muongo kwa mujibu wa CCM) ni kumkabili uso kwa uso na kupangua kila hoja zake. Lakini hili swala la kutokuwa tayari kwa mdahalo kwa upande wa Magufulil inafikirisha sana. Linafikirisha endapo kila analohubiri hana uwezo wa kulitetea, kila anachojinasibu kukifanya hana imani nacho kuweza kukitetea endapo kutakuwa na maswali juu yake ama uwezo wake wa kujenga hoja ni mdogo kiasi kwamba anataka yeye tu awe ndie muongeaji na kusifiwa kwa kila alichokifanya pasi kuhojiwa.

Japo kuna watakaobisha ila ni swala la dhahiri matarajio ya CCM kwenye uchaguzi huu umebadilika sana kinyume na mipango yao. Walihisi kampeni hizi zitakuwa ni nyepesi mno kwa kuamini yale waliofanya ni makubwa mno kuweza kuwapitisha. Lissu kabadilisha fikra za walio wengi kupelekea kufanya watu waanze kuhoji vile ambavyo waliona havikuwa na umuhimu. Waswahili husema 'Usiongelee nafsi ya mtu', CCM waliongelea mioyo ya watu kuamini wote wanahitaji vile walivyovipa kipaumbele.

Isingekuwa Lissu leo hii wote tungekuwa tunaimba mapambio ya flyover na Bombardier kama walivyotaka CCM. Inawezekana hoja za Lissu zisiwe na mashiko lakini zinafikirisha kupelekea kuzua maswali. Njia ya pekee ya kuweza kurejesha watu katika mapambio yaliodhamiriwa awali ni kukubali mdahalo kwa Magufuli ili aweze kutetea na kutuaminisha kuwa alikuwa sahihi na Lissu anakosea (kama tu anakosea kweli). Ni fikra zangu tu.
 
Ukimuacha BWM wakati anagombea si utamaduni wa wagombea wa CCM kushiriki kwenye mijadala. Kuna issue ya kujiamini unapokuwa huna nguvu za dola kukulinda. Hivyo msipoteze muda na hili jambo.
Hii midahalo ilipaswa iendelezwe. Mbali ya umuhimu wake wa kuweza kujua uwezo wa kujenga hoja mgombea, ingesaidia pia kuondoa dhana ya kuwa Rais haojiwi. Sasa imefikia wakati kumhoji Rais ni utovu wa nidhamu ilhali haipaswi kuwa hivyo.
 
Moja kati ya mambo ambayo yalimpa nguvu mdugu Benjamin William Mkapa ni mdahalo uliofanyika pale Kilimanjaro Hotel.

1. Mkapa aliyekuwa anaonekana hajui siasa, alizungumza kitaalam na kiweledi sana kiasi hata waliokuwa wanamshabikia Mrema wakagundua umbali wa kimaarifa ulipo kati yao.

2. Mzee Cheyo hakuwa na hoja zaidi ya kujaza watu mapesa.

Licha ya ugumu uliopo lakini ifike wakati CCM ikubali Mdahalo kwa Mgombea wake wa Urais mwaka 2025.
 
Nani wa kujibu hoja za Magufuli kwenye mdahalo kwa hawa wapinzani njaa?
Kwa mtu kama Lissu, Membe, Zitto hoja zao nyepesi zinajibiwa na wakina Polepole na Bashiru Ally.
 
Kwa nini usiitishwe mdahalo wa wagombea urais wote halafu tuone nani atakacha? Hivi ni akina nani wanaohusika na kuandaa mdahalo?
 
Moja kati ya mambo ambayo yalimpa nguvu mdugu Benjamin William Mkapa ni mdahalo uliofanyika pale Kilimanjaro Hotel...
Itakuwa ngumu kwa watawala wetu wa ki Africa ikiwemo Tanzania kukubali midahalo kirahisi. Watawala (sio viongozi) wa kiafrica wanapenda kusujudiwa, kauli zao wanataka ziwe sheria. Pakiwepo mdahalo na kukapatikana mtu anaeweza kweli kujenga hoja jambo pekee litakalotokea ni kudhalilika kwa mtawala. Picha ya kuwa yeye ndie mwenye kauli ya mwisho itafutika, maana itabidi akubali kujibu kila atakalohojiwa.

Mkapa pamoja na mapungufu yake yote, alikuwa ni statesman wa kweli. Alikuwa mkali lakini pia alikuwa na uwezo wa kutetea kila anachokifanyia ukali.

Kuna mstari mwembaba sana baina ya "shaka" na "imani". Kama vile unavyoweza kumuaminisha mtu kuwa yupo sahihi, vile vile unaweza mfanya mtu kujishuku usahihi wake. Na hili ndilo alilolichezea Lissu kwa Magufuli, amewatia shaka watu katika kila imani waliokuwa nayo awali kwa Magufuli. Pangekuwa na mdahalo pengine Magufuli angeweza kurudisha imani kwa watu. Tofauti na hapo kujibu kiholela holela kwenye mikutano ya kampeni inachukuliwa ni kama porojo na kumpa "kiki" Lissu zaidi.
 
Ili iweje? Wakati wa porojo na maneno ulishaisha, hapa kazi tu
Msipende kukariri maisha kuwa kila kitu ni porojo. Kile kilichokuridhisha wewe pengine kinamkwaza mwingine. Mwisho wa siku kinachohitajika ni usawa wa kuweza kujieleza. Kama vile Lissu alivyokuwa na haki katika kuhoji na kushutumu basi halIkadhalika Magufuli ana haki ya kujibu kila hoja na shutma.
 
Kwanini akomae na apoteze muda kwenye jambo ambalo halimuongezei kura? Pia isitoshe magu ana vijana wengi mnooo wakufanya shughuli ndogo ndogo kama hizo akiwemo huyo kibaraka.

Tangia kampeni zimeanza lini ulimuona Magufuli anaongea na waandishi wa habari kwenye kuweka mambo sawa pale palipokuwa na upotoshaji?

Wapo vijana ndio shughuli zao hizo CCM inawalipa pesa ndefu kwa ajili ya kazi hizo. Magufuli ana kazi nyingi sana ya kuwatumikia watanzania tofauti na huyo kibaraka.
 
Kwani hilo jambo lishawahi kuwepo katika nchi hii??

Unajuaje anaogopa wakati hiki kitu hakipo??

Jaman tupo Tanzania, sio kwa kina Trump..ambapo uchaguzi wao maamuzi yapo kwa senators na sio raia wa kawaida wa U.S.A
 
Back
Top Bottom