Kwanini disha FTA cband hazisumbui signal kama dish za KU band je wadau tufanyaje manake visimbuzi vyote vinatumia KU band?

deo paul555

JF-Expert Member
Oct 22, 2018
1,405
520
Habari wadau,kumekuwepo malalamiko kuhusu signal kua hafifu kwenye visimbuzi hivi vyenye mfumo wa KU band sasa dawa tufanyaje ili kuepuka changamoto hii?
 
Hii changamoto haikwepeki kwani mfumo wa mawimbi ya ku band huathiriwa na hali ya hewa mfano wakati wa mvua kukata ni lazima, makampuni mengi yanatumia mfumo huu kwasababu hutumia antenna ndogo(dish) hivyo ni rahisi kuwafikia wateja wenye minimum space, ebu jiulize azam ingekuwa inapatikana kwa dish LA 6ft yule aliepanga vingunguti angeweza?
Pia ukubwa wa dish huongeza uwezo wa signals hivyo dish kubwa hupokea signal nyingi kuliko dish dogo.
 
Miongoni mwa dawa ni kutumia dish size kubwa kidogo ya size uliopewa na muuzaji kwa mfano dish LA azam ni 90cm hivyo nenda kanunue dish jingine LA 120cm, pia vifaa vya ufungaji vipo vya hadhi tofauti mfano kuna Ku lnb za kuanzia 3000 hadi zaidi ya 80000 hivyo nunua vifaa kulingana na mazingira unayofunga dish lako
 
vipi nikiunga receiver ya azam kwenye dish kubwa,ntapata kitu gani
 
Hili suala ni visimbuzi vyote hakuna unafuu?
 
Miongoni mwa dawa ni kutumia dish size kubwa kidogo ya size uliopewa na muuzaji kwa mfano dish LA azam ni 90cm hivyo nenda kanunue dish jingine LA 120cm, pia vifaa vya ufungaji vipo vya hadhi tofauti mfano kuna Ku lnb za kuanzia 3000 hadi zaidi ya 80000 hivyo nunua vifaa kulingana na mazingira unayofunga dish lako
Hayo madish yanauzwa wapi? mie Niko mkoani bei linauzwaje? Hivyo vifaa vinaitwaje naweza kunga visimbuzi vyote vye kuband?
 
vipi nikiunga receiver ya azam kwenye dish kubwa,ntapata kitu gani
Dish linaweza pokea mawimbi yoyote bila kujali ni la kisimbuzi gani au ni la FTA, kwa kutumia hilo dish unaweza kufungia kisimbuzi chochote tena itakuwa bora zaidi ndio maana hata huko studio kuna midish mikubwa sana ili Ku maximize signals
 
Back
Top Bottom