Kwanini Diamond hajawahi kufungiwa na YouTube kwa kosa la wizi wa nyimbo?

Madimba jr

JF-Expert Member
Aug 12, 2017
1,577
3,143
Licha ya mara nyingi sana Bwana Chibu amekua akishutumiwa kuiba ama kukopi nyimbo za wasanii wengine kitu ambacho ni kosa la haki miliki, je kwanini haijawahi tokea waibiwaji wakalalamika au YouTube kumpiga ban?
 
Ukiona umeiba, ni bora kuongea nao inbox wamiliki then unawakatia mpunga yanaisha.
 
Mida ya lawama yataongewa mengi mara figisu,mara mchawi mara ana mbania dogo.

Kukopi sio issue wala sio kosa as long umefuata sheria na taratibu,ukiona mtu hajafungiwa jua alifuata sheria zote na kuheshimu haki za mtu aliye create.
Na ndo sifa ya msanii wa kimataifa,kuheshimu taratibu za copy right
 
Diamond alivyotumia ile melody aliyoshirikishwa na msanii wa Namibia ile melody ilikuwa produced na Laizer Classic sasa chezesha akili.

Nyingine huwa anawasiliana na wamiliki na hakuna anayeweza kukataa maana jamaa ana subscribers wengi ana followers wengi wanamkubalia tu, si unaona nyimbo ya Soapy nayo imepata viewers wa kutosha tu kisa Diamond
 
Amelalamikiwa ndo maana, na malalamiko yamefika YouTube, Mondi either analalamikiwa juu juu mitandaoni bila walalamikaji kufuata sheria au anawamaliza fasta walalamikaji kabla hawajeenda mbele, ni hivyo mkuu.

Ila inavyoonekana Harmo labda alichukulia poa malalamiko, angeusoma mchezo angewahi kumalizana na jamaa akamkatia mpunga mambo yangeisha kimya kimya na sie mashabiki tungeendelea kula uno kwa raha zetu huko YouTube.

Hata harmonize amesample ila results zimekuja tofauti
 
Mkuu unamzungumziaje Harmonize?
Frankly speaking namkubali sana jamaa, ila kutoka kwakwe WCB hakujipanga sawasawa; fan base aliyokuwa nayo bado haijawa strong, 75% mashabiki zake walikua ni WCB fans kindakindaki, wengi washaanza kumpa kisogo.

Alihitaji muda kidogo ili awe matured enough, simuombei mabaya but he need to work strong so as to mantain his career, otherwise Mungu ndiye mpangaji wa kila jambo lililo jema.
 
Mida ya lawama yataongewa mengi mara figisu,mara mchawi mara ana mbania dogo.

Kukopi sio issue wala sio kosa as long umefuata sheria na taratibu,ukiona mtu hajafungiwa jua alifuata sheria zote na kuheshimu haki za mtu aliye create.
Fact mwamba wahuni hawawezi elewa
 
Licha ya mara nyingi sana Bwana Chibu amekua akishutumiwa kuiba ama kukopi nyimbo za wasanii wengine kitu ambacho ni kosa la haki miliki,je kwa nini haijawahi tokea waibiwaji wakalalamika au youtube kumpiga ban?
Ukweli ni kwamba, Diamond huwa anawapuuza tu haters! Mfano mzuri chukulia ile The One. Mtu ambae alikosea ni King Tee Dee lakini pamoja na kushambuliwa, Diamond hakutaka kusema ukweli na akaamua kubeba gunia la misumari ingawaje kosa halikuwa la kwake!

Beat kila kitu ni mali ya Wasafi lakini King Tee Dee akakiuka makubaliano!! Na ndo maana pamoja na mashabiki wa King kumtaka aseme chochote lakini hakuwa na ubavu wa kufanya hivyo kwa sababu alijua ukweli ni upi!
 
Back
Top Bottom