Kwanini Diamond Alishinda: Tofauti za Wazi na za Msingi Kati ya KTMA na MTV Awards!

reandle

JF-Expert Member
May 6, 2009
11,168
8,142
Toafauti ya kwanza kabisa, inayotofautisha kati ya KTMA na MTV Awards ni kwamba, kwa KTMA, msanii ana uwezo wa kutoka na kontena moja la tuzo peke yake na kwa wakati mmoja wakati kwa MTV ni ndoto kufanya hivyo! Hadi sasa, msaniii anayeongoza kutoka na kontena la tuzo za KTMA kwa wakati mmoja ni Diamond Plutnumz ambae aliibuka na tuzo 7 kisha wanafuatia Ali Kiba na 20% ambao kila mmoja amepata kuibuka na tuzo 5.

Ukweli huo hapo juu unatokana na tofauti za kimsingi zinazounda Tuzo za KTMA na MTV ambazo ni:
>>>Wakati MTV Awards inakutanisha wanamuziki MAHIRI kutoka majiji makubwa kabisa barani Afrika kama vile Dar es salaam, Nairobi, Lagos, Johannesburg, Cape Town, Accra, Kinshasa n.k, KTMA kwa kiasi kikubwa inakutanisha wasanii kutoka kaeneo kadogo tu duniani kanakoitwa Wilaya ya Kinondoni!
>>>Tofauti na MTV Awards, pia MC wa KTMA most likely atatoka wilaya ya Kinondoni, wakabidhi tuzo watatoka huko huko, venue, wilaya ya Kinondoni… tumeenda mbali sana, Wilaya ya Ilala! Majority ya watakaopita Red Carpet-- wilaya ya Kinondoni, watakaokuja kuburudisha, majority watatoka wilaya ya Kinondoni and, to cut story short, almost everything, for KTMA kitakuwa ni Wilaya ya Kinondoni!
>>>Wakati host mkubwa wa KTMA ni wilaya ya Kinondoni na kidogo Ilala na hivyo kuzifanya tuzo za KTMA kuwa ni tuzo za WA HAPA HAPA, hosts wa MTV Africa Awards wanakuwa nchi mbalimbali!! Hawa WA HAPA HAPA wasubirie host city awe Dar es salaam ndipo labda waje kuambua kama ambavyo Wakenya walipata kuzizoa mwaka 2009 baada ya Host City kuwa Nairobi!!!
>>>Wakati kwenda kwenye tuzo za MTV, majority ya wasanii watatakiwa kuchukua air flight, kwa KTMA, in fact, hata kupanda gari ni mbwembwe coz' majority ya wasanii wana uwezo wa kufika kwenye venue hata kwa Bajaj simply because Tuzo zenyewe zinakutanisha WA HAPA HAPA!!!
>>>Wakati MTV Awards inakutanisha wasanii wanaofanya kazi zao kwa lugha mbalimbali za kimataifa kama vile Kiingereza, Kifaransa, Kireno n.k, KTMA, kwa kiasi kikubwa, inakutanisha Wamatumbi peke yao, kwa maana ya watumiaji wa Lugha ya Kiswahili kwa kuwa ni tuzo za WA HAPA HAPA!

Dah! Tofauti zipo nyingi sema wakati ukuta! Je, ewe mwenzangu unaweza kutaja tofauti zingine za WAZI (sio za KIUFUNDI) kati ya MTV Awards na Kinondoni Tanzania Music Awards?

Hata hivyo, kabla sijakusanya kila kilicho changu na kusepa wacha niseme jambo moja! Nimeona watu hapa eti wanaponda Tuzo ya Best Live ACT na kufananisha na suala la kukata mauno! Short and clear, ukitoa hiyo hoja mbele ya watu wanaoifahamu tasnia ya muziki moja kwa moja watakauona muziki huufahamu! Ingekuwa Live Act ni kukata mauno basi hizo tuzo kila mwaka, sio Afrika tu bali hata duaniani zingeenda DRC!!

Biashara ya muziki duniani imebadilika sana, mauzo ya CDs sio deal tena kwa wasanii! Africa ambako hata masuala ya hati miliki ni hovyo, ukiacha endorsement wasanii wanategemea zaidi performance jukwaani na kupitia hili eneo, ndipo pekee msanii kwa kiasi kikubwa anaweza kuwa na uwezo wa kuuza kazi au bidhaa zake zingine inculding hizo CD kwa kuwa fans wako wanakuwa wamekusanyika sehemu moja kuliko kuwataraji kwamba wataenda dukani kununua CDs zako au nguo zako!! Live Act ni eneo lenye faida na mzunguko mkubwa wa pesa pengine kuliko eneo lingine kwenye biashara ya muziki na ndio maana, leo hii tukiambiwa mathalani Lady Gaga anakuja Dar, basi Dar mzima itakuwa full vurugu; kuanzia promotions kwenye medias, maandalizi ya venue, deals za kuuza ticket, kampuni kubwa kutaka kudhamini na kadhalika bila kusahau mzunguko wa pesa utakaotokea kwa wauza vinywaji na chakula!! Huko kote, ni mzunguko wa pesa … watu watapanda magari kutoka hata Mwanza kuja Dar es salaam only for Live Act! Kwahiyo ni kichekesho mtu akisema this's all about kukata mauno! Mauno yanakatwa kitandani, jukwaani is all about performance, nyie watu wa wapi!!!

In short, kwenye Best Live Act wanaangalia pamoja na mambo yafuatayo:
>>>ENERGY: Kuwa Mkata Mauno Bora kuliko wote duniani lakini kama hauna ENERGY, pisha wenye pumzi wafanye kazi yao!
>>>CROWD ENGAGEMENT: Kuwa na pumzi za kutosha lakini ikiwa hauna uwezo wa kushirikisha crowd na kuleta shangwe kwenye show, please, pack and go because you're not BEST LIVE ACT
>>>BEST MUSIC: Huwezi kuwa na muziki wa hovyo halafu ukaota kuwa Best Live Act unless kama ni kwenye hizi tuzo za WA HAPA HAPA!! Huwezi kuwa na crowd engagement or crowd feedback wakati muziki wako ni mbovu unless kama ni kwenye hizi tuzo za WA HAPA HAPA! ​

Halafu mwambieni jamaa, haya mambo mi natembelea kwenye akaunti yake halafu ananiambia nisiue tembo wakati hata Mikumi sijawahi kufika isn't fair at all... huu ni uonezi wa wazi wazi! Yaani mie nimetulia zangu tuli na ka-Techno kangu halafu unaniambia nisiue tembo?
 
mkuu ndio maana mwaka jana ureno mchezaji bora alikuwa pele, cristiano kapuni wakati mchezaji bora wadunia akaja kuchukuwa Cristiano

Wenye gere hapo, bado hawajakuelewa na hakuna wanachokiogopa kama facts, utakuta wamejifungia kwenye uziwao hahahaha
 
huu uzi umekaa kishabiki sana tofauti kubwa wala hujaisema nayo ni mamna ya kumpata mshindi , KTMA kura za mshabiki ndio zinaamua mshindi kwa asilimia kubwa kama sio yote. MTV wao majaji au jopo la wataalamu ndio wanaamua mshindi kwa kiwango kikubwa , ingekua kura tu Leo tungekua tunaongelea mond tuzo tatu Vanessa moja , ila kule vigezo na masharti vinazingatiwa , tofauti nyingine KTMA watu wanapiga kura hata nani aingie lakini MTV hilo halipo , maana wangefanya hivyo hata kiba angekuepo ,wao wanaangalia nani kafanya nini ndio wampe nominee, hapa KTMA wana cha kujifunza
 
Hii tunzo ni funzo kubwa sana kwa waswahili wenzetu maana walikuwa bize sana kujaribu kuharibu mchizi asipate.

Tunzo aliyopata ni pesa kubwa kama hawajui, kakalisha watu giants kwenye industry ni maana kubwa sana kibiashara.

Show aliyofanya ilikuja kupruv wrong ata waliokuwa na mashaka.. Goli jingine hilo, hakuna kuchezea nafasi. Naweza sema ndio show nzuri kuliko show zote jana.

Kingine ni kuonyesha kuwa inawezekana wabongo tunaweza basi tu hatujiamini, Diamond kinachomsaidia ni Confidence na kuweka nguvu ya kutosha kwenye kazi yake. Nategemea Joh makini kuwa nominated mwakani kwenye best hip hop.

Mwisho kabisa zile timu tatu zilizompigia Davido huku mkiwa club mnakuwa crazy na nyimbo za Diamond... Mmeshachelewa mchizi kashapata karibu kila anachotakiwa apate mwanamziki wa kimataifa. Anasubiri marudio tu. Sasa tunaitafuta dunia yote.
 
Dai kafanya vizuri. Ukiangalia shoo ya Jana na ile ya mchezaji bora wa Africa inampa nguvu na ataendelea kuperform kwenye events kubwa
 
Pichaya kibabe washindi tu
Best female
Best live act
Best male
Best new act
 
Attachments

  • 1437294870231.jpg
    1437294870231.jpg
    31.6 KB · Views: 602
huu uzi umekaa kishabiki sana tofauti kubwa wala hujaisema nayo ni mamna ya kumpata mshindi , KTMA kura za mshabiki ndio zinaamua mshindi kwa asilimia kubwa kama sio yote. MTV wao majaji au jopo la wataalamu ndio wanaamua mshindi kwa kiwango kikubwa , ingekua kura tu Leo tungekua tunaongelea mond tuzo tatu Vanessa moja , ila kule vigezo na masharti vinazingatiwa , tofauti nyingine KTMA watu wanapiga kura hata nani aingie lakini MTV hilo halipo , maana wangefanya hivyo hata kiba angekuepo ,wao wanaangalia nani kafanya nini ndio wampe nominee, hapa KTMA wana cha kujifunza

Ulichosema n kweli kabisa huu uzi umekaa kishabiki hadi mwandishi ameshau kuandika alichokuwa anataka kuandika, MTV wana jopo kubwa na zuri la majaji ndomana maamuz wanayotoa yanakuwa straight mbele ya mtu mwelewa. Kiukweli watanzania tuko vzr sana kwenye swala la kupiga kula kweny mamb km haya ya entertainment, naamini at kipengele cha best male na best collaboration kwa kura diamond aliongoza, ila kwakuwa sio tuzo za watu, majaji wametumia vigezo vile vile ambavyo vimempa diamond best live act mbele ya iyanya na nominees wengine. Kikubwa n kuungana tu na kuwa kitu kimoja linapokuja swala la utaifa, congratulation diamond hard work pays
 
Tatizo hamuelewi au hamkutaka kuelewa! Nimesema tofauti za wazi, tofauti ambazo hata asiyejua kusoma ataziona! Suala la kuwapo majaji sio tofauti ya wazi coz' si mimi wala wewe anafahamu Jaji huyu alitoa points ngapi na yule alitoa ngapi na total zilikuwa ngapi kwa kila mmoja... lakini tunaposema kwamba KTMA inakutanisha wasanii kutoka wilaya ya Kinondoni hilo lipo wazi... tunaposema msanii kuhuduhuria show ya KTMA anaweza kwenda hata kwa bajaj, hilo pia lipo wazi... tunaposema KTMA inakutanisha wamatumbi watupu hilo nalo halihitaji kwenda shule kulifahamu!

Lakini pamoja na yote hayo, hamuwezi kunielewa usipofahamu namna mbalimbali za kuwakilisha mada kisanaa ya uandishi matokeo yake mmesoma kitu kama kilivyo na mkakimeza wakati kimsingi hapo ilikuwa ni kuzungumzia local and international awards! Na kwavile ni international awards, huwezi kukuta mafyongo ama mazingaombwe yanayofanyikaga kwenye local awards... Uwezo wa mtu ndicho kinacho-matter!
 
Dai kafanya vizuri. Ukiangalia shoo ya Jana na ile ya mchezaji bora wa Africa inampa nguvu na ataendelea kuperform kwenye events kubwa
Upo sahihi kwa 100% na hii ndo faida kubwa kabisa ya Best Act Award... events kubwa hususani za kibiashara lazima ziwe na best performers!
 
I have loved this thread.... some guys have spoken facts and facts only... there should be a point that people become precise and deal with what is the truth coz ts very clear that despite all his weaknesses as a person and personality in general, diamond is an inspiration if you choose to deal with his music side it and turn it into personal testimony and drive in whatever that you are doing u won't get disappointed but most of us are stupid enough to always look for faults. hate,jealousy, low self esteem na ulimbukeni
 
huu uzi umekaa kishabiki sana tofauti kubwa wala hujaisema nayo ni mamna ya kumpata mshindi , KTMA kura za mshabiki ndio zinaamua mshindi kwa asilimia kubwa kama sio yote. MTV wao majaji au jopo la wataalamu ndio wanaamua mshindi kwa kiwango kikubwa , ingekua kura tu Leo tungekua tunaongelea mond tuzo tatu Vanessa moja , ila kule vigezo na masharti vinazingatiwa , tofauti nyingine KTMA watu wanapiga kura hata nani aingie lakini MTV hilo halipo , maana wangefanya hivyo hata kiba angekuepo ,wao wanaangalia nani kafanya nini ndio wampe nominee, hapa KTMA wana cha kujifunza

hapa ndipo point ilipo
 
Big up Diamond Platnum!! Godbless you all the way through...

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
hapa ndipo point ilipo
Ah! Wapi... unafikiri issue ni kwavile MTV kuna majaji na kama ingekuwa ni kura ndo inaamua bado mambo yangekuwa ni kama KTMA? Kwamba ingekuwa kura ndo inaamua mshindi basi Diamond angenyakua tuzo tatu kama anavyosema EMINEMU kwani huko KTMA kilitumika nini kama sio kura za mashabiki? Kila mwenye akili timamu anafahamu Diamond ana mashabiki wengi kuliko mtu mwingine yeyote!! Yaani msanii subscribers wachache, followers iwe Facebook, Instagram, Twitter kote huko wachache lakini linapokuja suala la kupigiwa kura za kupendwa, ndie anaongoza!! Subiri awards za KTMA nazo ziwe zinaamuliwa na hao majaji uone kama kutakuwa na tofauti... hao majaji watatoka wapi kama sio wale wale wa kule kule wenye tabia zile zile??!!! Ile Miss Tanzania huwa inaamuliwa na nani? Mbona kila mwaka malalamiko? Kitu kinavyokuwa TOO LOCAL kinakosa professionalism, kiwe kinaamuliwa na majaji au kwa kura za mashabiki na huo ndio msingi wa "wasanii, wanatoka Wilaya ya Kinondoni, Majaji wanatoka wilaya ya Kinondoni, watoa tuzo wanatoka Wilaya ya Kinondoni, mabosi wa wadhamini wanatoka wilaya ya Kinondoni... hiki na kile, ni wilaya ya Kinondoni! Itoshe tu kusema kwamba hapo Kinondoni ni kiwakilishi tu!!!! Pasipo na professionalism, hata utaalamu au taaluma ya mada husika, itabanangwa tu... hata huko MTV, kama kusingekuwa na proffesionalism, bado hata hao majaji pamoja na utaalamu wao wote wa muziki, bado wangebananga!! Lakini kwa kuwa MTV Awards hazipo too local, basi majaji wanalazimika kufuata weledi wao coz' kinyume chake, ni ku-abuse taasisi mzima ya MTV Base yenye heshima kubwa duniani! In contrary, ndani ya KTMA who cares about KTMA image?! Who care about BASATA image among watu wa BASATA wenyewe?! No one!
 
Last edited by a moderator:
Unapoona kuna events kubwa kubwa Africa na msanii anaalikwa kwenda kutumbuiza ujue sio jambo dogo hata kidogo
Pesa wanayolipwa kufanya shows zile kila mwanamuziki anazililia kupata

Tuzo hii ya mtumbuizaji bora inamuhakikishia sasa kuendelea kuhost mashows makubwa makubwa ya kimataifa ya pesa ndefu sasa,

Mialiko ya shows za kawaida itategemea kupanda zaidi na pia mkwanja atakao vuta kwa show utakua sio wakitoto tena
Kiufupi tuzo hii imemtengenezea mazingira mazuri zaidi ya ulaji kupitia show ambazo ndio mfumo unaolipa zaidi kimuziki Afrika

Kama kuna mambo namuaminia Chibu ni kujua kutumia fursa iliopo mbele yake, hii ni zaidi ya fursa kwa Chibu tumuombee mema na tumsapoti atafanya makubwa msimu huu

Natamani sana mfano kwenye tuzo kama hizi tungekuwa na vichwa kama hata kumi kama walivyo wanaijeria au south afrika, tumepenyeza wawili amepata mmoja
Chibu ndio balozi wa muziki wetu kimataifa tukimpa sapoti kubwa watu wataamini bongofleva ni muziki mzuri na wataibuka na wengine sasa
Lakini tunatumia nguvu nyingi kumzamisha balozi wetu apotee kwenye ramani ya muzki afrika tubaki kujuana locally tu
 
Thumb Up! Ile award ina bonge la impact tofauti na watu wanavyodhani! Watu siku hizi wanataka wasanii wanaoweza kufanya performance na kudatisha watu kwenye venues; iwe ni concert or else! Watu wanaoweza ku-communicate na crowd; mtu ambae hata ukimlipa thousands of dollars kwenye show bado una uhakika mashabiki kibao wataingia kwa kuwa wanafahamu mtu wa kazi ameingia na watatoka ukumbini wakiwa wameridhika na kuwa tayari kwa twin shows!
Big up kuna kadada kanajiita cute_zuby kalisumbua sana mara tuzo mbovu ya mnenguaji maneno mengi kakaeleweshwa hakakuelewa ,kaelewesheni wenzangu.
 
Music is about selling these days, how can you sell?creativity in your music and good marketing strategies can make you conquer the market. Diamond is learning from Jay Z,lyrically Nas was superior to Jay Z,but Jay Z was more of a businessman, so he focused on good marketing strategies and creativity on his music, that's it!
 
Back
Top Bottom