Kwanini dhana ya/za mapinduzi,haki,amani na uzalendo si masomo yanayoeleweka sana Zanzibar? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini dhana ya/za mapinduzi,haki,amani na uzalendo si masomo yanayoeleweka sana Zanzibar?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nicholas, Oct 9, 2012.

 1. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  Kwa wanaofuatilia matukio ya nyanja mbalimbali visiwani Zanzibara watakubaliana nami kuwa mambo haya hayana tafsiri za kufanana kati ya wazanzibar na watanganyika kama si na wengine duniani.

  Mambo kama:haki, uhuru wa kutoa mawazo, haki, mapinduzi amani na uzalendo uhuru hayana dhana moja yakitumiwa na mtu wa bara na wa Visiwani.Mfano wa haraka ni uzalendo.Watu wabara watapata picture ya uzalendo kama utanzania,wazanzibar watamaanisha uzanzibar kama si upemba na uunguja.Mfano mwingine ni uhuru kamili wa nchi.Wazanzibar wanawatazama bara kuwa wakoloni ingawa wenyewe pamoja na udhaifu wao kiuchumi,kiuzalishaji na hata kuzua manung`uniko,huku pia wakiwadharau.Wazanzibar nao pia wanachanganya kwenye nia yao ya uhuru na utambuzi wake,kwani baadaya kugombea uhuru utawasikia pia wakilalala kuhusu misaada.Hakuna asiyejua kuwa misaada huondoa uhuru.hapa tatizo linaonekana ni kuwa wazanzibar hawaujui uhuru na pia hawautaki uhuru.Wanajijenge taswira kuwa hawapo huru kwa ubaguzi.

  Suala la haki pia halina mtazamo mmoja.Wao haki ni pale wanapopewa wapendalo pila kutoa haki kwa wengine.kwanini wao wanafurahia kuingia bara na kupata uhuru kama huu ila wao wapo very busy kuwakimbiza watuw a bara?

  suala la mani nalo pia ni illusive sana visiwani.Matukio ya kuchoma vitega uchumi na nyumba za ibada hasa za wakwritu na watu wa bara ni sehemu moja inayoonyesha wazanzibar wanatazama amani kwa macho tofauti sana.Hiyo mioto na mengine ni tishio linalopoteza amani kwa wengine.

  Uhuru wa kuongea na kutoa mawazo haujaweza wafanya wazanzibara kuwa responsible kwa waongeacho?Ni rahisi sana Kiongozi wa Kizanzibar kuongea umoja wa wazanzibar bila kutaja umoja wa watanzania.Kwa umoja una haki miliki kwa wazanzibar tuu.Kuna kutowajibika sana kwa kauli za viongozi wa Zenj.Kam ilivyo kwao kuwa uzalendo unapoishia ktk ukubwa wa Zenj, bila kujua kuna uzalendoa wa famili, kijiji, wilaya, mkoa, nchi na bara na dunia kama tungekuwa tuna mahusiano na viumbe wa nje ya dunia.Ingawa tunafanya maombi kwa Mungu ailinde na kuifanyia wema Dunia.

  Kuna mengi sana yasiyokuwa na tafsiri moja katk ya bara na visiwani.Pengine wachangiaji wanaweza ongeza mengine na huku wakisema kati ya Zanj na Bara ni yupi yupo karibu sana na uelewa wa pamoja kama vile sehemu nyingine ya dunia inavyoelewa.Tumeona jinsi gani Arab spring ilivyoshindwa leta chochote kipya kwa waarabu kwa vile uelewa wao kuhusu vitu kama democrasia na vionjo vyake bado nitofauti sana na wengine duniani ndio maana hata kiongozi aingizwapo na wapigania demokrasia hufanya yale yale waliyoyapinga.
   
 2. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Umepoteza muda wako bure kuandika vitu visivyoeleweka...unachangaya mambo kutokana na upeo wako ulivyokuwa finyu, unawaongelea Wazanzibar halafu unarukia issue zingine eti tumeona Arab spring ilivyoshindwa leta chochote kwa waarabu sijui wewe ni raia wa Misri, Tunisia, Yemen?

  Nakushauri jikite zaidi kwenye chama chenu cha Kaskazini kuondoa ukabila na udini.

  Nina miaka mingi sijawahi kusoma uchambuzi dhaifu kama huu.
   
 3. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  Kinakuuma sana kuhusu Arab spring kuwa failure?Bado mengi yatakuwa failure TZ na nilivyoorodhesha ni highlights tuu wengine watachangia vyao.Naomba jikite kuangalia unachoweza andika zaidi ya kuniaandika mimi .Tafadhali.Kosoa unachoona au ongezea unachoona.
   
Loading...