Kwanini 'Customer care' wa mitandao ya simu wanataka tujitambulishe wakati tumejisajili?

dendaboy

JF-Expert Member
Sep 15, 2016
1,085
742
Ma customer care wa mitandao yote ya simu unapowapigia kuomba huduma wakishapokea wataanza kujitambulisha na pia kutaka na wewe ujitambulishe.

Wewe ni nani na unapiga simu ukiwa wapi na vitu kama hivyo, sasa swala la wao kujitambulisha ni sawa ili unapopewa huduma walau ujue ni nani amekuhudumia.

Lakini inakuaje sasa na mimi nijitambulishe wakati nimesajili line kwao, ID yangu wanayo najitambulisha nini tena.

Alafu hata ukikurupuka kuanza kumuelekeza shida yako bado anakurudisha nyuma tena ujitambulishe na ukimtajia jina feki na mahala feki ulipo anaridhika na kusikiliza shida yako.

Hii maana yake nini sasa?
 
Verification ndugu, kumbuka kuna issues nyingi kampuni za simu wana deal nazo kwa sasa including ku transfer pesa. Lazima wajue wanaongea na nani na ikibidi ku confirm zaidi . Zoea tu mana mkiibiwa nyie nyie wa kwanzA kuchafua majina ya kampuni na kudai fidia
 
sijui kama umeelewa nilichoandika
 
sijui kama umeelewa nilichoandika

Nimeelewa hutaki kujitambulisha sababu umejisajili hata ukipotezea anakuuliza. Na nimekujibu kwa jinsi ulivyoandika kuwa ni muhimu popote ESPECIALLY, sehemu zenye huduma za transferring pesa. Hata kama hitaji lako halihusiani na pesa kama ni mteja wao LAZIMA ujitambulishe and more to verify you according to your problem. Sio tz only ndugu.
 
Wasamehe mkuu, tatizo letu kubwa ni kukariri. Nlichogundua ni kwamba hawana system access ya Kutambua au Ku verify customer details in time,ndiyo maana ukitaja jina tofauti wanakubali tu na Huduma unapata.
 
Nimeelewa hutaki kujitambulisha hata ukipotezea anakuuliza. Na nimekujibu kwa jinsi ulivyoandika kuwa ni muhimu popote ESPECIALLY, sehemu zenye huduma za transferring pesa. Hata kama hitaji lako halihusiani na pesa kama ni mteja wao LAZIMA ujitambulishe and more verify you according to your problem. Sio tz only ndugu.
ok sasa ni kwa nini wakati nimesajili kwao na id yangu wanayo

kwa hili la kawaida ninapo save namba yako kwa sm yangu hata baada ya mwaka

siku utakapopiga jina lako litakuja na nitajua wewe ni nani unapiga

vipi kwa wao waniulize?
 
Je nikiibiwa simu mtu alieiba akaichezea na kukupigia au kukutext kwa namba yangu utajuaje wkt ume save jina langu? (Now talk about a thousand of calls they receive wanajuaje wewe ni exactly mhusika mwenye namba uliyepiga)
 
Teh teh.....kaazi kweli kweli.
Sidhani kama kuna ubaya kujitambulisha.
Kuwapo kwa jina lako au picha hakumfanyi mhudumu kutambua sauti yako.
Labda kama ulisajili na sauti

Wakati mwingine sio kila anaepiga simu ni yule aliesajiliwa tu.
Taratibu za kazi zinamtaka afanye hivyo.
 
hata kama imeibwa na alieiba akataja jina lake na wao hawana uwezo wa kutambua kwamba huyu ni mwenyewe ama sio inasaidia nini utambulisho huo?
 
wanaepusha usumbufu usio wa lazima kuanza kutafuta jina lako.. na kuhakikisha pia kuwa wanaeongea nae ni mwenye simu/line halali.
Mimi niliwahi kufanya kazi tigopesa.. kila anaetoa hela namuuliza jina lako nani,?
maana waweza toa hela ya mwingine ukampa mwingine.

kutaja jina ni moja ya uthibitisho.
 
hata kama imeibwa na alieiba akataja jina lake na wao hawana uwezo wa kutambua kwamba huyu ni mwenyewe ama sio inasaidia nini utambulisho huo?

Kwani ina cost kiasi gani kujitambulisha? Mtoto wa kiume vitu vidogo sana hivi kulalamika ni aibu,
kama vipi usijitambulishe uone km utasaidiwa. Walioweka hiyo system dunia nzima hawakuwa wajinga ndugu. Watu wanaibiwa kila siku makampuni wanadaiwa mbona simple. Anaeiba hawezi kujua kila kitu ulichofanya ktk simu yako. Haezi kujua tar yako ya kuzaliwa iliyo ktk system, haezi kujua some tricky information ulizotoa wkt unajisajili.
 
Teh teh.....kaazi kweli kweli.
Sidhani kama kuna ubaya kujitambulisha.
Kuwapo kwa jina lako au picha hakumfanyi mhudumu kutambua sauti yako.
Labda kama ulisajili na sauti

Wakati mwingine sio kila anaepiga simu ni yule aliesajiliwa tu.
Taratibu za kazi zinamtaka afanye hivyo.
kwa nini wanatulazimasha kufanya jambo lisilo na mantiki
 
wanaepusha usumbufu usio wa lazima kuanza kutafuta jina lako.. na kuhakikisha pia kuwa wanaeongea nae ni mwenye simu/line halali.
Mimi niliwahi kufanya kazi tigopesa.. kila anaetoa hela namuuliza jina lako nani,?
maana waweza toa hela ya mwingine ukampa mwingine.

kutaja jina ni moja ya uthibitisho.
anapokutajia jina sio lenyewe unampa pesa?mbona hawa wanatupa huduma hata ukitaja feki
 
Wana lengo la kukuuliza jina lako coz kuna watu wengi wanatumia line zisizo zao na uchakachuaji...
 
Back
Top Bottom