Kwanini cheti cha ndoa hutolewa siku ya ndoa tofauti na vyeti vingine vinavyotolewa baada ya kuhitimu course flani?

Internal

JF-Expert Member
Feb 23, 2017
3,575
3,894
Habarini wanabodi!.

Poleni na majuku ya hapa na pale, swali hapo juu lajieleza vyakutosha. Ni kawaida mtu kupewa cheti baada ya kuhitimu course(fani) flani, kwa upande wa cheti cha ndoa mbona ni tofauti maana mnapewa cheti mwanzo kabisa wa ndoa kwanini msisubiriwe mpaka muhitimu?

Je hatuoni kama tunapewa vyeti bila elimu ndio maana tuwapo kwenye ndoa tunashindwa kuendesha ndoa maana cheti ni fake? Unapewaje cheti bila kuhitimu? Tujadili kidogo hapa

Over
d716ae83591e95a7cb0a05522afb0305.jpg
 
Ndoa ni tasnia ya pekee ambayo inahitaji uvumilivu ndyo mana cheti unapewa mapema kabla ya mitihani utayo enda kukutanayo.

Uthubutu tu wa kuamua kuoa na hatimae ukaoa ni kufuzu kukubwa ndo ama ile cku unatunukiwa cheti.

Sababu zengine pamoja na mambo ya kiimani na kijamii zaidi mana cheti ni sehemu ya mkataba hivyo huwezi kuishi na mtoto wa watu bila makubaliano yeyote ya kimaandishi yanayo ambatanisha mashahidi. Huo ni muono wangu
 
Ndoa ni tasnia ya pekee ambayo inahitaji uvumilivu ndyo mana cheti unapewa mapema kabla ya mitihani utayo enda kukutanayo. Uthubutu tu wa kuamua kuoa na hatimae ukaoa ni kufuzu kukubwa ndo ama ile cku unatunukiwa cheti. Sababu zengine pamoja na mambo ya kiimani na kijamii zaid mana cheti ni sehem ya mkataba hivyo huwez kuish na mtoto wa watu bila makubaliano yyt ya kimaandish yanayo ambatanisha mashahidi. Huo ni muono wng
.

Kuhusu mkataba basi tusingeita chet ili tujue ni mkataba not certificate
 
Habarini wanabodi!.

Poleni na majuku ya hapa na pale, swali hapo juu lajieleza vyakutosha. Ni kawaida mtu kupewa cheti baada ya kuhitimu course(fani) flani, kwa upande wa cheti cha ndoa mbona ni tofauti maana mnapewa cheti mwanzo kabisa wa ndoa kwanini msisubiriwe mpaka muhitimu?

Je hatuoni kama tunapewa vyeti bila elimu ndio maana tuwapo kwenye ndoa tunashindwa kuendesha ndoa maana cheti ni fake? Unapewaje cheti bila kuhitimu? Tujadili kidogo hapa

Over
d716ae83591e95a7cb0a05522afb0305.jpg
Hicho siyo cheti cha taaluma ambacho hutolewa baada ya mafunzo fulani.

Cheti cha ndoa ni alama tu ya kisheria kuwa hawa wawili wamekubaliana kuishi pamoja kama mume na mke hivyo lolote likitokea tofauti na waliyokubaliana kuishi cheti hicho hutumika kama ushahidi mbele ya sheria kudai haki za msingi kwa mmojawapo.
 
Mfano-umemfuata binti ili umuoe na akakwambia yeye hamjui mwanaume bado so mvumiliane hadi ndoa,usiku wa fungate unagudua watu washachenjua sana makinikia huko mgodini na hadi kitu bwawa na hakuna cha bikra,jjtatu ulipaswa ukachukue cheti cha ndoa,utaenda ama utaanzisha mgogoro?!
 
Hicho siyo cheti cha taaluma ambacho hutolewa baada ya mafunzo fulani.

Cheti cha ndoa ni alama tu ya kisheria kuwa hawa wawili wamekubaliana kuishi pamoja kama mume na mke hivyo lolote likitokea tofauti na waliyokubaliana kuishi cheti hicho hutumika kama ushahidi mbele ya sheria kudai haki za msingi kwa mmojawapo.
Nimekupata mkuu ila vipi tungejaribu kuhoji abari ya kubadilishiwa jina badala ya cheti tukaita jina lingine ili kukitofautisha na vyeti vya kufuzu fani flani???.
 
Kwaio unataka wawe wanaambatanisha na cha kifo akae navyo izrael? Au uzikwe navyo ukipaa upae na gamba lako, ukifka izrael akisoma,causes of death....."VIAGRA", utaskia akiita Yudaaa! Ongeza mkaaa.
 
Habarini wanabodi!.

Poleni na majuku ya hapa na pale, swali hapo juu lajieleza vyakutosha. Ni kawaida mtu kupewa cheti baada ya kuhitimu course(fani) flani, kwa upande wa cheti cha ndoa mbona ni tofauti maana mnapewa cheti mwanzo kabisa wa ndoa kwanini msisubiriwe mpaka muhitimu?

Je hatuoni kama tunapewa vyeti bila elimu ndio maana tuwapo kwenye ndoa tunashindwa kuendesha ndoa maana cheti ni fake? Unapewaje cheti bila kuhitimu? Tujadili kidogo hapa

Over
d716ae83591e95a7cb0a05522afb0305.jpg
Utaratibu wake ni sawa na huo wa vyeti hivyo vengine. Ipo hivi..... ukishasoma na kufaulu kwa mfano kuwa daktari kama vile Dr. Shika ndo unapewa cheti. Sio baada ya kutibu wagonjwa. Unapewa cheti ndio ukatabibu. Halikadhalika,baada ya kuhitimu na kuonekana kua utaweza kuhimili yote yanayohusu ndoa. Basi unakabidhiwa cheti. Au sivyo hivyo
 
Umeweka Dr. Shika nimebaki nacheka tu. Lakini mbona mafunzo ya ndoa hakuna? Au huko kwenu kuna course ya ndoa ili uonekane umehitimu?
 
Hakuna mtu anaoa bila kupewa mafunzo kutoka kwa wazee na watu wengine ambao washaoa. Ndo mana ndoa inahusisha familia zote za mume na mke. Kuna mengi unayo ambiwa kabla uingie kwenye ndoa. Na ukionekana bado unakataliwa tu mkuu
 
mpaka mnafikia kufunga ndoa hiyo ni kama mahafali yenyewe, kwamba mnatunukiwa chetu kuwa mmefuzu na mnaweza kuishi pamoja bila kutoana roho. sasa kama wewe umekimbilia ndoa kabla ya kupitia hatua za awali basi cha moto utakiona huko kwenye ndoa
 
Habarini wanabodi!.

Poleni na majuku ya hapa na pale, swali hapo juu lajieleza vyakutosha. Ni kawaida mtu kupewa cheti baada ya kuhitimu course(fani) flani, kwa upande wa cheti cha ndoa mbona ni tofauti maana mnapewa cheti mwanzo kabisa wa ndoa kwanini msisubiriwe mpaka muhitimu?

Je hatuoni kama tunapewa vyeti bila elimu ndio maana tuwapo kwenye ndoa tunashindwa kuendesha ndoa maana cheti ni fake? Unapewaje cheti bila kuhitimu? Tujadili kidogo hapa

Over
d716ae83591e95a7cb0a05522afb0305.jpg
Wanakosea kusema cheti .huu nimkataba kama wakuuziana kitu mnapoandikishana .
 
Back
Top Bottom