Kwanini Chato International Airport na si Omukajunguti international Airport? Kagera inaonewa sana

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
Mpango wa omukajunguti ni wa Siku nyingi

Je, mnatambua kuwa serikali imeshiriki katika kuudumaza mkoa kagera?
Hivi ndivyo mkoa kagera umeachwa yatima na serikali ya Tanzania,
Tulivyopata Uhuru kagera ilikuwa miongoni mwa mikoa mitatu yenye uchumi imara,

1. Dar es salaam
2. Kagera
3. Kilimanjaro

Lakin ukweli usiopingika Kagera imetelekezwa na serikali vya kutosha bila kujali majanga yaliyoikuta au michango ambayo Kagera imetoa kwa watanzania.

Kila MTU kutokea Kagera atakuwa ana kumbukumbu zinazomfanya kusononeka sana,

SABABU MUHIMU ZILIZOSABABISHA KAGERA KURUDI NYUMA KIMAENDELEO

1. VITA YA KAGERA, 1978/79
Vita ya nchi nzima ilipiganwa kwenye mkoa mmoja na kuharibu miundombinu vya kutosha , na ule ndo ulikuwa uwanja wa vita hasa, lakini hakuna sehemu yoyote kuna strategy za kuujenga upya mkoa, tunaishia kusikia maneno ya kashfa tu tena toka kwa viongozi wakubwa kwa wanakagera eti mmeshindwa kujenga hata chuo kikuu kimoja? Aliuliza Kikwete lakini kasahau kuwa yeye kama mkuu wa serikali hajajenga hata chuo cha kutoa cheti.

2. JANGA LA UKIMWI 1983,
Kama inavyojulikana Kagera iko mpakani mwa Uganda, na UKIMWI umeanzia Uganda, na kwa kuwa wana Kagera wana utaratibu wa kufanya Biashara na Uganda , haikukwepeka kupata UKIMWI, nguvu Kazi kubwa ilipotea sana miaka hiyo na kusababisha uchumi kurudi nyuma,

3. AJALI YA MV BUKOBA
Janga la pili ambalo linafanya kudhoofisha mkoa wa Kagera ni kuwa , watoto wengi yatima wameongezeka , nguvu kazi imepungua kutokana na ajali ile.

4.1998 EL NINO
Hii wengi mnaelewa kuwa imekumba sana ukanda wa kanda ya ziwa kuliko kanda yoyote ile hapa nchini , imeharibu miundombinu na kupoteza wazalishaji Mali,

5. KUSHUKA KWA BEI YA KAHAWA 1998 KWA UZEMBE WA SERIKALI.
Inajulikana Kagera ilitegemea sana Kahawa kama kitega uchumi , kwa uzembe wa serikali hakukuwepo utaratibu wa kuhakikisha Kahawa inabaki na bei ya kuridhisha badala yake ikapuuza mpaka wananchi wakakata mibuni maana haikuwa na maana tena,

6. UBAGUZI ULIOJIFICHA TOKA KWA VIONGOZI ( INDIRECT DISCRIMINATION TOWARDS HAYA TRIBE)
Miaka ya nyuma hakuna ambaye hajui kuwa wahaya waliwekewa mizengwe katika baadhi ya sekta, hata kwenye elimu , walipandishiwa alama za ufaulu ili wachache waendelee na elimu ya juu maana walionekana kuwa wao ndio wanafaulu na kujaza madarasa mengine, lakin ili kuitamka sentensi hii (INAHITAJI UJIFANYE MWENDA WAZIMU KIDOGO)

7. KUTENGWA NA NCHI KIJIOGRAFIA
Kagera iko Kaskazini Magharibi mwa Tanzania, waliowahi kufika uko ndio wanaelewa namaanisha nini, Kagera imekuwa kama kisiwa maana jinsi ya kufika kule inabidi ukatishe kilometer kadhaa za msitu, ili uingie Kagera, au upite ziwani kwa meli ndio uende mikoa mingineyo ambayo ni ya Tanzania, hivyo basi wana Kagera walikuwa na urahisi wa kufanya Biashara na Uganda kuliko mikoa mingine ya Tanzania, lakini serikali ilikataza biashara hiyo , wakajikuta wamebaki kama kisiwa ndani ya nchi yao wenyewe,

8.KAGERA KIMBILIO LA WAKIMBIZI MAUAJI YA KIMBALI YA RWANDA 1994 NA MACHAFUKO TANAYOENDELEA UKANDA ULE.
Wanyarwanda wameiteka Kagera hasa wilaya ya Karagwe na Muleba na kujichukulia ardhi , pia wamekuwa watekaji wa magari na kudhalilisha wana kagera , kitu amabacho kimerudisha nyuma uchumi wa mkoa, kwa kasi, majambazi wametamalaki na kufanya uharamia ambao umefanya kusiwepo hali ya utulivu na kujenga uchumi, serikali imechelewa kuchukua hatua,

9. KUTOJUMUISHWA KATIKA VIPAUMBELE VYA MAENDELEO KIKANDA
Kila kanda imetengwa katika kanda fulani ya mkakati wa maendeleo lakini kanda ya ziwa ambayo ndipo kuna mkoa Kagera hakuna ilipoainishwa katika mpango wa maendeleo.Kagera Umekuwa ni mkoa wa kujitegemea kwa kila kitu utasikia

Ukumbi wa mkutano unajengwa Arusha, sijui chuo cha utalii Dar, chuo cha ufugaji Tabora.

Chuo cha reli tabora, chuo cha science cha nelson Mandela arusha,
Chuo cha serikali cha ugavi, Chuo cha ushirika Moshi Mara..

Chuo cha mbao Iringa, kwanini Kagera hakuna mipango endelevu, sasa upo wapi uwanja wa Mukajunguti wa ndege na ulishaahidiwa kuwa wa kimataifa na kutengewa bajeti kipindi cha Mkapa?,Rais Magufuli halioni hilo?

Kagera wanekuwa wa kupandia kama daraja, Kikwete kaenda Bukoba katoa ahadi ambayo imerudiwa na Magufuli sana, eti ntawapa meli ,mbona hata mtumbwi haujaweka,

We unayesoma hapa nitajie chuo chochote kilichojengwa na serikali kuazia cheti mpaka degree, imekuwa vipaumbele kujenga Dodoma na mnasahau kuna deni Kagera inadai kwa taifa hili.

Kilichosaidia Kagera ni vishirika vya wazungu tu kama partage, world vision, gses, yaan serikali haijatenda haki huko.

SOMA HII SASA SERIKALI INA KITU KINAITWA SUBJECTIVE AND OBJECTIVE PLANNINGS,(BIG FOUR REGIONS) IKO HIVI

1.KANDA YA KUSINI AU NYANDA ZA JUU KUSINI
Imetengwa kama kanda ya kilimo hapa kuna mikoa
Njombe
Mbeya
Katavi
Ruvuma
Na Iringa .

2.KANDA NYINGINE KANDA YA KASKAZINI
Hii imeahinishwa na kupewa kipaumbele kama kanda ya utalii,
Mikoa ni
Arusha,
Kilimanjaro na Manyara,

3.NYINGINE NI KANDA YA KATI ,
Taasisi za siasa na Elimu ya juu
Mikoa ni
Morogoro,
Dodoma,
Singida,

4. KANDA YA MASHARIKI INEPEWA Kanda ya viwanda na Biashara, mikoa ni
Dar es salaam,
Mtwara
Lindi
Pwani
Tanga

KANDA YA ZIWA ANBAYO KUNA KAGERA IKO WAPI, ?
Sasa inafika hatua tunapaswa kuusema ukweli ,

Mheshimiwa rais huu ulikuwa ninwakati wa Kujenga MUKAJUNGUTI INTERNATIONAL AIRPORT SIYO CHATO. TUNGEPOZWA ANGALAU NA UWANJA UO MAANA TUMESUBIRI NEEMA KWA MIAKA MINGI LAKIN WAPI

Wengi watasema umejenga huko kwakuwa ni kwenu, lakini pia hata KAGERA KARAGWE NI KWENU KWA MZEE MACHALILA, NA JINA LAKO LA KIHAYA NI KATO (wengi hawajui hii), sasa kama ndo sababu ya kujenga nyumbani anza nyumbani ambapo pako kwenye mipango ya Siku nyingi,
Kajunguti International Airport - Wikipedia, the free encyclopedia

Britannica
 
Kama ni Umuhimu wa Airports basi kwanza tungejenga Viwanja vya Kila Mkoa . Tungehakikisha Mikoa Yote in viwanja vya kimataifa au bora all weather.
bado kuna mikoa haina viwanja vya uhakika,
na hili ndio lengo la serikali zote zilizopita. wamekua wakijenga viwanja vipya katika mikoa .
Chato hakuna sababu wala umuhimu labda kama cm wameamua kumjengea mkuu uwanja wa kutua akienda christmas
 
Hapana mkuu jangwani hapatanisaidia lakin kagera Imetelekezwa sana
Bukaoba ina uwanja wandege, ina uwanja wa mpira, barabara zote za kuingia bukoba ni za lami, umeme upo wa uhakika wa kutoka uganda, mbunge mmepewa Rwakatare mliyempigania kwa muda mrefu, sasa munataka maendeleo gani JPM awapatie hebu funguka.

Geita barabara ni za vumbi, hamna umeme wa uhakika, hakuna maji, hakuna uwanja wa mpira, mkoa pekee hapa Tanzania ambao hauna hata kiwanda cha soda, sasa JPM anataka anagalau kuweka usawa wa kiuchumi mnaanza makelele.
 
Bukaoba ina uwanja wandege, ina uwanja wa mpira, barabara zote za kuingia bukoba ni za lami, umeme upo wa uhakika wa kutoka uganda, mbunge mmepewa Rwakatare mliyempigania kwa muda mrefu, sasa munataka maendeleo gani JPM awapatie hebu funguka.
Bukoba hatuna chuo kikubwa cha serikali, Bukoba hakuna hadhi ya kuitwa manispaa mji umechoka sana hakuna juhudi za serikali za kuuendeleza kama miji mingine
Bukoba imekuwa kisiwa Biashara imekuwa hatari sana hakuna namna ya kufanya na wenzetu
 
Lakin ukweli usiopingika kagera imetelekezwa na serikali vya kutosha bila kujali majanga yaliyoikuta au michango ambayo kagera imetoa kwa watanzania,

Waliotekekeza Kagera ni wana Kagera wenyewe.Watu wa Kagera popote wanapokuwa ndio kwake kafika hana mpango wa kagera wala nini kama wachaga.Kagera wanaenda tu sana sana labda mtu akifariki wanaenda kuzika au kuhani msiba! Kagera kuna wasomi na wenye pesa wamezagaa dunia nzima lakini hawana makazi ya kudumu bukoba na hawana mpango wa kuhamia kukaa kule au kufanya uwekezaji mkubwa kule.

Kila mtu wa kagera anayefanikiwa SANA anachofanya ni kutimukia DAR ES SALAAM ,MIKOA MINGINE.Marekani ,ULAYA NK

Kagera kulitakiwa kuwe na vyuo vikuu kibao.Maprofesa wastaafu wako weengi mno kule wangeanzisha mavyuo kibao walimu wakawa wenyewe na washomile wengine ambao wako every where in the world including UNITED NATIONS and other important UN agencies and ICC.

Kwa watu wa kagera kusubiri serikali ifanye mambo makubwa ni too low na ni aibu.
 
Kauli za hovyo hovyo kama hizi zilizo kaakaa ki UKUTA UKUTA hazina tija.Mbona hukuwahi kuandika kulaani operation hovyo ya ukuta?.
Haya mambo yakujenga hoja kikabilakabila sijui kwanini wahaya mnayapenda sana?
Hii ni ishara kwamba lile linalosemwa kwamba ninyi ni wakabila ni lakweli.
Raisi yupo mbioni kununua meli kubwa lake victoria ili itoe huduma huko kwenu,mbona hujalalamika kwamba amewapendelea akawaacha wengine?
Hemu mwacheni raisi afanye kazi
 
Walioteklekeza Kagera ni wana Kagera wenyewe.Watu wa Kagera popote wanapokuwa ndio kwake kafika hana mpango wa kagera wala nini kama wachaga.Kagera wanaenda tu sana sana labda mtu akifariki wanaenda kuzika au kuhani msiba! Kagera kuna wasomi na wenye pesa wamezagaa dunia nzima lakini hawana makazi ya kudumu bukoba na hawana mpango wa kuhamia kukaa kule.

Kila mtu wa kagera anayefanikiwa SANA anachfanya ni kutimukia DAR ES SALAAM ,MIKOA MINGINE.Marekani ,ULAYA NK

Kagera kulitakiwa kuwe na vyuo vikuu kibao.Maprofesa wastaafu wako weengi mno kule wangeanzisha mavyuo kibao walimu wakawa wenyewe na washomile wengine ambao wako every where in the world including UNITED NATIONS and other important UN agencies and ICC.

Kwa watu wa kagera kusubiri serikali ifanye mambo makubwa ni too low na ni aibu.
Tatizo la wahaya ni kudhani ili uonekane mtu wa matawi lazima ukae Dar au Mwanza, wakisoma hawataki kurudi bukoba wanaenda kuzika na kuondoka, sasa hivi wasukuma wanajenga kwao, tizama mji wa katoro kahama na bwanga inakua kwa kasi, leo hii kukuta nyumba ya kisasa kijijini ni jambo la kawaida sana.
 
Kauli za hovyo hovyo kama hizi zilizo kaakaa ki UKUTA UKUTA hazina tija.Mbona hukuwahi kuandika kulaani operation hovyo ya ukuta?.
Haya mambo yakujenga hoja kikabilakabila sijui kwanini wahaya mnayapenda sana?
Hii ni ishara kwamba lile linalosemwa kwamba ninyi ni wakabila ni lakweli.
Raisi yupo mbioni kununua meli kubwa lake victoria ili itoe huduma huko kwenu,mbona hujalalamika kwamba amewapendelea akawaacha wengine?
Hemu mwacheni raisi afanye kazi
Kwani rais hakumbushwi mbona mapenzi yanakuzidi?
 
Haya haya, naona ule msemo wa 'ukabila' umepiga hodi rasmi!
Ngoja tuwe na subira maana alivyopata waziri wa ujenzi alianza na barabara ya kwake (Bwanga - Kyamorwa) ambayo kimsingi hata kwenye ramani ya barabara za nchi haikuwemo. Lakini tunaona miaka takribani 10 aliyokaa wizara hiyo kila mkoa/wilaya inajivunia kuwa na barabara za kisasa. Acha tuone miaka mitano akiwa ikulu kira tarafa yaweza kuwa na airport!
 
..kama mkoa uliozaliwa "unanyimwa" maendeleo hamia ktk mikoa "inayopendelewa."

..kuna kipindi Mwalimu Nyerere alianzisha mpango wa quota system ktk nafasi za masomo ya sekondari.

..mikoa fulani iliremshiwa pass mark za kwenda sekondari, huku mikoa mingine ikiwekewa ugumu zaidi.

..wazazi toka mikoa ile ambayo Mwalimu aliamua "kuibinya" ktk kufaulu kwenda sekondari wakawa wanahamisha watoto wao, wanabadili hata majina, na kwenda kusoma darasa la 7 kwenye mikoa iliyokuwa "ikipendelewa."

..KAMA MKOA WAKO UNANYIMWA MAENDELEO HAMIA MKOA UNAOPENDELEWA.
 
Back
Top Bottom