Kwanini Chama cha Mapinduzi chaguzi zake za ndani sifa kuu ya mgombea ni fedha?

mtoto wa mchungaji

JF-Expert Member
Oct 24, 2020
279
480
Nilikuwa nafuatilia maadhimisho ya miaka 22 bila baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye sikuwai kumwona kwa macho nikashangaa sana na sikuelewa kuwa aliyokuwa anayaongea yule Mzee ni yakweli au ulikuwa unafiki wa kisiasa. Kama alikuwa muasisi wa Tanu na CCM na alikemea rushwa na alikuwa mkali sana kiasi kile iweje sasa CCM hii inaweka sifa nambali moja ya mgombea ni kuwa na pesa. Inamaana chama akijui wapi kilipotoka.

Inasemekana kuwa haka katabia kalianza baada ya Mwalimu kuondoka na hakuna kiongozi yoyote aliyefuata aliwai kuwa mkali na kukemea hako katabia ndani ya chaguzi. Na niligundua katabia ka rushwa ndani ya chaguzi za CCM kalishamiri zaidi baada ya baba wa taifa kung'atuka na baadaye kuaga dunia kwani katika hotuba yake moja aliwaisema sasahivi sifa kubwa ya mgombea ni pesa ndani ya chama.

Juzi katika kupitisha majina ya ubunge na madiwani ndani ya chama ndiyo ilidhiilika live kuwa hunapesa usipoteze muda ambapo ilipelekea wajumbe kupewajina la WAJUMBE SI WATU. Hii ilitokana na kuto kueleweka kama hawa wajumbe ni watu au wanyama gani maana wote walikuwa pamoja na walisema fulani hatufai hajaleta maandeleo haitishi vikao na mengine mengi lakini walishangaa mwisho wa siku wajumbe wanampa mtu huyo huyo kura zote waliokuwa wakimsema.

Kwa hari ilivyo sasa hasa kwa levo ua udiwani na ubunge mtu hawezi kutoka tena labda atokee mtu wa kumzidi pesa, au ugonjwa au kufa hapo anaweza kupata mtu mwingine. CCM imeenda mbali zaidi kuna baadhi ya maeneo katika nchi kuna koo ndiyo zinatawala udiwani na si ukoo mwingine, na maeneo mengine pia kuna jamii ya watu wenye asili kama wa asia au arabia hawa ndiyo wanakuwaga wabunge tu na si waswahili wa asili kushika ubunge.

Huko nyuma Nyerere anasema zamani hawakuangalia pesa ya mtu hata kidogo katika uchaguzi, na sifa mbaya na hatari ambayo mgombea alikatwa jina likiwa juu angani ilikuwa ni ngombea kuwa na pesa, anasema Nyerere ilikuwa disikwalifai. Leo ndugu unapesa usijiangaishe kwenda kuwanunia wajumbe bure.

Katiba ya CCM imeanza na neno UTU.
Kadi ya chama CCM inaanza na UTU, lakini ndani ya chama chenyewe hilo halipo. Katika ahadi za mwana CCM zipo na moja inasema SINTATOA WALA KUPOKEA RUSHWA.
Kama sasa wanatoa na kupokea kwanini wasibadirishe katiba na ahadi za chama kuwa sasa tunapokea rushwa na kutoa pia.

Kibaya zaidi hizi tabia za rushwa hata vyama vya upinzani pia vimeiga kutoka kwa babalao CCM, leo CUF, CDM na vyama vingine vya upinzani tumeshuhudia nao pia kama huna pesa huna nafsi ya kuwa kiongozi au kupitishwa jina lako, hivyo CCM imewaharibu mpaka watoto yaani vyama vya upinzani. Na vyama vya upinzani vyenyewe ndiyo vikaenda mbali zaidi yaani hata wakiwa katika kampeni ya kuomba kura wakimaliza wanapitisha bakuli kuomba pesa yaani mpaka inashangaza yaani wanaomba vyote awabakizi.

Utu wa mwafrika umebaki jina, wanasiasa ni pesa pesa pesa,wananchi ni kutoa kutoa kutoa kutoa tu, hata huku kanisani ni hivyo hivyo mchungaji akitaka nyumba tunachanga lakini muumini akitaka nyumba anaombewa.
 
Marekani kama sio tajiri kua Rais ni ndoto,wakupe hicho cheo maskini uchote pesa zao,hawataki hiyo
 
Huu ni utamaduni uliojengeka kidogokidogo hadi ukakomaa.
Wajumbe hawakupi kura bila kitu pia wanaangalia watafaidika nini ukishapata

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom