Kwanini CHADEMA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini CHADEMA?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Mar 27, 2009.

  1. Mwiba

    Mwiba JF-Expert Member

    #1
    Mar 27, 2009
    Joined: Oct 23, 2007
    Messages: 7,606
    Likes Received: 201
    Trophy Points: 160
    Kwa nini CHADEMA isiwapeleke mahakamani wahusika wa ufisadi ?
    Chadema wanasikika wakilipua na kutangaza kwenye mikutano yao ya operesheni sangara kuwa fulani na fulani ni mafisadi wamesababisha hili na lile ,s asa kufikia kutangaza huko si jambo dogo ,ni lazima wana ushahidi wa kutosha ,hivyo ni jambo gani linawashinda kuwapeleka mahakamani wahusika wa ufisadi ? blah blah za kila siku hazina mpango ,tunataka kuona kutokana na ushahidi waliokusanya waende mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake wasingojee serikali ya Sultani CCM ichukue hatua au bunge au au,Chadema ni lazima waende mahakamani kufungua kesi ,kwa kadiri ya ushahidi walio nao ,sioni umuhimu wa kuwapotezea muda wananchi na kuwaeleza fulani na fulani walikwapua bilioni kadhaa ,waende mahakamani kama ni kushitaki mtu mmoja mmoja au ni kuishitaki serikali tumeona serikali imeshitakiwa kuhusiana na mauaji ya Albino so huu ni wakati wa Chadema nao kuipandisha serikali au wahusika wa ufisadi mahakamani au waache kutudanganya na ushahidi wa uongo.:cool:
     
  2. zomba

    zomba JF-Expert Member

    #2
    Mar 27, 2009
    Joined: Nov 27, 2007
    Messages: 17,082
    Likes Received: 38
    Trophy Points: 0
    Hapo ndio panapo-shangaza!
     
  3. J

    Jasusi JF-Expert Member

    #3
    Mar 27, 2009
    Joined: May 5, 2006
    Messages: 11,474
    Likes Received: 138
    Trophy Points: 160
    Mwiba,
    Hivi hizi mahakama ziko chini ya utawala wa chama gani? Ukipata jibu hapo umejijibu.
     
  4. Mwiba

    Mwiba JF-Expert Member

    #4
    Mar 27, 2009
    Joined: Oct 23, 2007
    Messages: 7,606
    Likes Received: 201
    Trophy Points: 160
    Unapoenda mahakamani unaenda kuuliza au unaenda kushitaki ? Rev.Mtikila kila siku anakwenda kushitaki na anashinda au uongo ? Msitafute kisibabu ikiwa mna ukweli basi ukweli siku zote unakuja juu ,nendeni mahakamani na list of shame otherwise itakuwa ni majungu tu na kuwadanganya wananchi na ushahidi usioweza kuikabili mahakama.

    Kisingizio cha mahakama zipo chini ya nani hazikubaliki ,sijasikia Chadema kuikataa Mahakama wala kuiponda ama kusema kweli CUF nimewasikia wakisema si mara moja wala mara mbili na wakiponda na kuwapiga madongo mpaka polisi ,sisemi haya kwa kuwa nionekane ni mfuasui wa CUF hapana najaribu kuweka kigezo cha kuzikataa mahakama kuwa hazitendi haki.

    Hivyo CHADEMA ikiwa wanaamini mahakamani hakuna haki watangaze ,na hata hivyo kwa kuweka kumbukumbu za hapo baadae ni lazima waende huko huko mahakamani ,kuliko kupita vichochoroni na kupiga domo kuwarubuni wananchi kwa kuwahubiria mambo yasio weza kushitakika .
     
  5. omarilyas

    omarilyas JF-Expert Member

    #5
    Mar 27, 2009
    Joined: Jan 24, 2007
    Messages: 2,127
    Likes Received: 5
    Trophy Points: 0
    Itakuwa vizuri kama utawashauri/kuwalazimisha CUF kuwapeleka kina HIZA TAMBWE na wengine mahakamani kwa UFISADI waliokuwa wakiufanya CUF..

    omarilyas
     
  6. N

    Ngekewa JF-Expert Member

    #6
    Mar 27, 2009
    Joined: Jul 8, 2008
    Messages: 7,730
    Likes Received: 22
    Trophy Points: 135
    Kwani MTIKILA yuko CCM mbona hushitaki na mara nyingi hushinda? Nahisi kama umekosea kwani Mahakama ni za wananchi na kinachotiliwa maanani ni ushahidi.

    Sasa hizo kelele ndio tuseme ni za bure huku wakijua kuwa hakuna hatuwa yoyote itakayochukuliwa? Nahisi Mwiba kashauri vizuri pengine CHADEMA wangemshirikishaBwana Makesi Mtikila
     
  7. M

    Mkandara Verified User

    #7
    Mar 27, 2009
    Joined: Mar 3, 2006
    Messages: 15,441
    Likes Received: 106
    Trophy Points: 160
    Mwiba,
    Mkuu wangu vipi tena?..
    Hivi unaelewa mashtaka yanavyowezwa kuundwa na kukubalika mahakamani!..
    Mathlan, unajua kwa uhakika kwamba Mkandara ameiba fedha benki ya NMB, lakini benki yenyewe wanasema hawakuibiwa wala kupoteza fedha..Hapa mkuu wangu utaanzia wapi mkuu wangu?..
    Chadema ni chama na ni wananchi kama wewe na mimi hawana kubwa kukushinda zaidi ya kuwa chama cha Siasa.. na Chadema hawakuibiwa kama chama ila tumeibiwa sisi sote Wadanganyika na kuna watu miongozi mwetu wasiokubali wala kuamini kwamba tunaibiwa acha mbali hiyo serikali na viongozi wake..

    Ikiwa leo Kikwete amefumbia macho maswala haya haya, kiasi kwamba Lowassa na Rostam sio tu walitubebesha mzigo wa Richmond, walidiriki ku transfer mkataba toka Richmond hadi Dowans kampuni yenye utata sawa kabisa na Richmond, hakuna kilichofanyika wewe utakuwa na ushahidi upi zaidi ya kuwepo kwa mashirika feki ya Richmond na Dowans nchini..
    Fedha zimeibiwa toka EPA, ni Chadema wanaosimama mahakamani?..mbona hata kuwapa pongezi mnashindwa wakati mnafahamu wazi kuwa Dr. Slaa ndiye chanzo cha yote haya..

    Haya Mwakyembe katupa ushahidi wote unaotakiwa kuwasimamisha viongozi wahusika mahakamani, sisi wananchgi tumefanya nini?.. au ulitaka pia Mwakyembe pia akawashitaki mahakamani!..
    Jamani tupikiwe watutengee mezani na vijiko bado tunadai watulishe kweli sisi tunataka shibe au Ubwanyenye!
     
  8. Nono

    Nono JF-Expert Member

    #8
    Mar 28, 2009
    Joined: Feb 11, 2008
    Messages: 1,277
    Likes Received: 69
    Trophy Points: 145
    Mwiba,
    Mawazo yako sio mabaya ila gharama yake kwa chama cha siasa inaweza isilingane na tija. Sio kuwa vyama vyote havioni sababu za kwenda mahakamani, kwani hata hujuma nyingi ambazo CUF kwa mfano imefanyiwa haijaenda mahakani. Kazi kubwa ya wanasiasa ni kueneza sera na kueleza wananchi mapungufu yalipo kwa serikali na chama tawala. Leo hii mkichukua mapungufu hayo na kuyapeleka mahakami, basi mahakama inaweza kutumika kisiasa kuendesha hizi kesi kwa miaka 5 au zaidi. Kumbuka jambo likishakwenda mahakani basi huruhusiwi tena kuliongelea nje ya mahakama, which mean huwezi tena kulitumia kama mtaji wa kisiasa kwa kipindi ambacho swala hilo linakuwa na mashiko katika masikio na fikra za wananchi.

    Kwa maana hiyo ushauri wako ni mzuri, lakini utaisaidia CCM na sio vyama vya upinzani. Mimi mtizamo wangu ni kuwa wapinzani waendelee kuyatumia kama mtaji wa kisiasa na CCM ijisafishe kwa kuishinikiza serikali yake kuwachukulia hatua wahusika, na wananchi washuhudie haki ikitendeka.

    Vinginevyo, wananchi wanayaona na wanayasikia na hawahitaji kuthitishiwa na mahakama kuwa hayo yanayosemwa na CHADEMA kuwa ni ukweli.
     
  9. P

    Petu Hapa JF-Expert Member

    #9
    Mar 28, 2009
    Joined: Jan 2, 2008
    Messages: 714
    Likes Received: 3
    Trophy Points: 0
    Hivi kama tunataka kuishitaki jamhuri sasa! tunaishitaki kwa kipi!
     
  10. zomba

    zomba JF-Expert Member

    #10
    Mar 28, 2009
    Joined: Nov 27, 2007
    Messages: 17,082
    Likes Received: 38
    Trophy Points: 0
    Kwa misingi hiyo wanaweza kuwa wanazuwa vilevile.
     
  11. The Farmer

    The Farmer JF-Expert Member

    #11
    Mar 28, 2009
    Joined: Jan 7, 2009
    Messages: 1,497
    Likes Received: 342
    Trophy Points: 180
    Kwani aliyeibua swala la UFISADI si mnamjua ( Dr Slaa) na sasa kuna kesi inaendelea dhidi ya hawa MAFISADI, sasa Mlitaka wapelekwe kwenye Mahakama zipi tena?
     
  12. Mpita Njia

    Mpita Njia JF-Expert Member

    #12
    Mar 28, 2009
    Joined: Mar 3, 2008
    Messages: 7,014
    Likes Received: 29
    Trophy Points: 135
    Kwani hakuna oversight institutions za kuhakikisha kuwa kesi kama hii inasikilizwa kwa haki?
     
  13. kinepi_nepi

    kinepi_nepi JF-Expert Member

    #13
    Mar 28, 2009
    Joined: Aug 16, 2007
    Messages: 870
    Likes Received: 4
    Trophy Points: 0
    Mwiba tayari Chadema wamekwenda mahakamani.
    angalia ile list of shame halafu angalia walipoanzia
    1. yona anakesi ya ufisadi
    2.mramba anakesi ya ufisadi
    3. balali kajiua kwa kujificha
    4. chenge safari yake haiko mbali
    5. mgonja yupo mahakamani
    6. wanapigana kubadili katiba wamburuze mkapa.

    kwa hiyo chadema wapo pazuri taratibu wote wataionja keko, hii vita sio lelema kwani hata kikwete anayeteua majiji yupo kwenye ile list.sio lazima wote waende mahakamani leo ila wataenda tu angalia malawi nini kimetokea au zambia kwanza tumewajua halafu tunazidisha presha mpaka chupa ipasuke.
     
  14. Mpita Njia

    Mpita Njia JF-Expert Member

    #14
    Mar 28, 2009
    Joined: Mar 3, 2008
    Messages: 7,014
    Likes Received: 29
    Trophy Points: 135
    Sikuwa na habari kwua Chadema ndio imefungua kesi dhidi ya watu hawa!
     
  15. kinepi_nepi

    kinepi_nepi JF-Expert Member

    #15
    Mar 28, 2009
    Joined: Aug 16, 2007
    Messages: 870
    Likes Received: 4
    Trophy Points: 0
    soma viganja vyako
     
  16. Mpita Njia

    Mpita Njia JF-Expert Member

    #16
    Mar 28, 2009
    Joined: Mar 3, 2008
    Messages: 7,014
    Likes Received: 29
    Trophy Points: 135
    Mhhhh, labda nimpelekee Sheikh yahya, mie sina ujuzi huo
     
  17. Fidel80

    Fidel80 JF-Expert Member

    #17
    Mar 28, 2009
    Joined: May 3, 2008
    Messages: 21,981
    Likes Received: 89
    Trophy Points: 145
    Duh yale yale kesi ya Nyani unampelekea ngedere sijui utasikilizwa mkuu mwiba.....utaambiwa faili linachunguzwa miaka 5 ndo liende kwa DPP mnaambiwa kama wananchi mkae mkijua mchague pumba ni nn na mchele ni nn....
     
  18. Zak Malang

    Zak Malang JF-Expert Member

    #18
    Mar 28, 2009
    Joined: Dec 30, 2008
    Messages: 5,410
    Likes Received: 17
    Trophy Points: 0
    Hadi sasa post zote za thread hii hazijasema lile la ukweli kutokana na sheria zetu zilivyo. Ufisadi ni masuala ya jinai (criminal) na kwa hiyo mashitaka yote ya jinai ni jukumu la Jamhuri -- yaani serikali -- katika kitengo cha Mwendesha Mashitaka Mkuu (DPP). Sasa kina Slaa hawana wao uwezo kufungua kesi za jinai -- wanaloweza ni kufungua kesi za madai tu (Civil cases).

    Ukweli huu unaifanya serikali kuwa mfalme katika masuala ya jinai, ikitaka inaweza kupeleka kesi mahakamani, na ispotaka basi huamua kuuchuna -- kama inavyofanya ktkt wahusika wa ufisadi wa Kagoda, Deep Green na Radar.

    Na hata kesi ikipelekwa mahakamani, serikali inaweza kuamua kuiondoa, ikitaka, iwapo serikali hiyo hiyo itaona itaathirika kama kesi itaendelea.

    Iko namna ambapo mtu binafsi anaweza kupelea kesi ya jinai mahakamani kwa utaratibu maalum na kwa ruhusa kutoka kwa serikali yenyewe -- nadhani kupitia kwa AG. Lakini historia inaonyesha kuwa hili limekuwa linashindikana kutokana na kuwepo vizingiti hasa katika utaratibu.

    Kesi ya Nawab Mulla dhidi ya Kanali Edmund Mjengwa (aliyetuhumiwa kutafuna fedha za michango ya elimu wilaya ya Mbarali), na ile ya mtu mmoja binafsi dhidi ya Mbunge wa Buchosa, Samuel Chitalilo (kwa kughushi vyeti vya elimu) ni mifano hai la ugumu wa suala lenyewe.

    Naungana na wale waliosema kuwa baadhi ya waliofikishwa mahakamini kuhusu ufisadi -- ule wa EPA na mwingine, unatokana na jitihada za akina Dr Slaa.

    Mimi nadhani mwanzilishi wa thread hii alikuwa ana nia ya kujaribu kuwaponda mashujaa hawa wa Chadema, basi.
     
    Last edited: Mar 28, 2009
  19. Nono

    Nono JF-Expert Member

    #19
    Mar 28, 2009
    Joined: Feb 11, 2008
    Messages: 1,277
    Likes Received: 69
    Trophy Points: 145
    Kama wanazuwa, basi wanaotuhumiwa pamoja na CCM wathibitishe kuwa sio hivyo, au wawashitaki kwa kuwazulia!
     
  20. Mwiba

    Mwiba JF-Expert Member

    #20
    Mar 28, 2009
    Joined: Oct 23, 2007
    Messages: 7,606
    Likes Received: 201
    Trophy Points: 160
    Hapana sina nia ya kuwaponda labda fikira zako zimekwenda mbali,kiasi mwanzo umeeleza vizuri na hiyo naweza kusema ni hoja ya kuwaeleza wananchi kuwa hamuwezi kwenda mahakamani kwa sababu hizo ulizoziainisha hapo juu.

    Lakini mkereketwa anaweza kuhoji mbona kesi ya maalbino imefikishwa mahakani na imeshitakiwa serikali ,japo kwa kuwataja wachache ambao ndio wenye dhamana ,sasa hili ambalo ushahidi wake mnao kwa makaburasha ,hundi na barua ,inakuwaje wale wa maalbino wenye ushahidi wa kuokotea kwenye magazeti na vyombo vya habari wameweza kulifikisha suala mahakamani ?

    Nahitaji maelezo yakina ,hawa waliofikishwa mahakamani wapo katika kinyang'anyiro ,kumbuka hata haya ya kuwanadi mafisadi na kuwavalia njuga wafuasi wa CCM wao nao wanadai ndio walioanzisha mapambano ,na hivi sasa wanadai serikali yao ndio inawapandisha mahakamani na sio makelele ya Chadema.

    Kama haitoshi Chadema ingeliweza kuzuia Bajeti isipitishwe kutokana na ubadhirifu wa fedha katika wizara husika zinazohusiana na ufisadi au mawaziri wake wapo katika list yao "List of Shame" walihusika na upotevu wa fedha ,wape uzito Chadema kuwa wana ushahidi wa ubadhirifu huo hivyo nguvu ya wabunge wao pengine wakishirikiana na upinzani wangeweza kusuia au kuweka shilingi na Mtanzania akaweka historia ya kuimbuka nguvu ya shilingi ,lakini mikiki na mabomu mliyokuwa mkilipua yote yalionekana yametiwa ndani ya gunia lililoloweshwa ,mkawa kimya na hakuna kura zilizopinga ,How Comes mnaweza kupitisha bajeti inayokwenda kuliwa mnawambia nini wananchi na majilabu ya kuwanadi mafisadi ? Tunahitaji maelezo hapa ,mnasema kuwa hamuwezi kwenda mahakamani aidha kwa sababu mahakama zimemilikiwa na Sultani CCM ,sasa pale Bungeni mna nguvu ya kulitetemesha Bunge na kuzuia jambo ambalo lingevuma nje ya mipaka ya Tanzania ,nguvu ya Shilingi inashinda mahakama katika Bunge. Kwa ufupi tunahitaji kuona mnakwamisha bajeti mpaka kilichoibiwa kinarudishwa na wahusika waote wanakamatwa na kuwekwa mahabusu ili wasiharibu uchunguzi by the Power of Tanzania shiling.
     
Loading...