Kwanini CHADEMA walisusia uchaguzi mdogo?

Chadema hawakujifunza CUF znz kuhusu kususia hakujawahi kukiacha chama salama hamna ruzuku wala nn
 
Waliojiandikisha kupiga walikua wangapi?

Waliopiga kura walikua wangapi?

Mgombea alieshinda alipata kura ngapi?

Je kati ya wale waliomchagua na wale waliosusa wapi walikua wengi? Hebu tuanzie hapo kisha tuendelee na mjadala
 
Waliojiandikisha kupiga walikua wangapi?

Waliopiga kura walikua wangapi?

Mgombea alieshinda alipata kura ngapi?

Je kati ya wale waliomchagua na wale waliosusa wapi walikua wengi? Hebu tuanzie hapo kisha tuendelee na mjadala
Wangapi kati ya waliojiandikisha 2015 wamehama ,kufa au kusafiri?
 
Kwahiyo kasoro zimerekebishwa?Lini kamati ilikaa kikao na kuja na Tamko kuwa sasa NEC ni shwari na tutashiriki uchaguzi?

Halafu Misuli acha utoto, nje ya mada. Tanzania iligoma kushirikiana na Morocco kwa kuwa imeivamia Sahara Magharibi. Je Morocco imeshatangaza kuacha kuikalia? Je Tanzania sasa haishirikiani na Morocco?

Je ni sifa tume kutokurekebisha kasoro zilizopo ili cdm iendelee kususua uchaguzi. Halafu shida iko wapi , waliosusia uchaguzi ni cdm, na walioamua kushiriki ni haohao cdm, je wamevunja sheria yoyote? Hao mliowaingiza chaka kwa kuwahonga majimbo basi togwa limeingia nzi
 
Hata hao wagombea wa Chadema wakijitoa utaona wafuasi wa Chadema wakishangilia

Kwahiyo kasoro zimerekebishwa?Lini kamati ilikaa kikao na kuja na Tamko kuwa sasa NEC ni shwari na tutashiriki uchaguzi?
MTz yeyote mwenye akili timamu, akashabikia hila zinazofanywa na NEC kwa kushirikiana vyombo vya dola, basi huu ni ulemavu kichwani. Tungependa tuwe na free & fair election kwa wakati wote. Hila hazitaijenga Tz ya viwanda bali mawazo mkinzano. Na ndivyo ilivyo tokea duniani pote ambapo wanaadamu wanafaidi matunda ya uhuru wao. Kulazimisha kuongoza watu ati tu ni Chama kilichopigania uhuru ni upotofu.
 
Mkuu
Ulitaka tuache hadi SIHA??
Kwani Longido si waliiachia?! Yaani watu wanajifanya kutoona wanayotendewa chadema. Ni kwenye chaguzi hizi wanakouliwa wafuasi wa CDM .

SO TUTAFUTE SOLUTION kwa Tz ya baadaye
 
KWANINI CHADEMA WALISUSIA UCHAGUZI MDOGO ULIOPITA?

Sir Taylor

Habari Wakuu.Sote tunajua kwa kilichotokea uchaguzi mdogo uliopita.Kupitia kamati kuu chadema kiliadhimia kususia uchaguzi mdogo wa Longido,Singida na Songea,Kwa sababu walizodai ni kuwepo kwa kasoro nyingi ambazo NEC wanatakiwa wazirekebishe.Nimekuwa mfuatiliaji wa Chaguzi mbalimbali za kisiasa hapa Tanzania kuanzia za Udiwani,Umeya Ubunge hadi Urais.NIWE MKWELI TU,Hakuna uchaguzi ambao umewahi kuwa huru na wa HAKI ktk mazingira yenye ushindani mkubwa kati ya CCM na CHADEMA.

Kwa asilimia kubwa kila uchaguzi matukio yanayotokea ni yaleyale ya awamu zote yaani HAKUNA SIKU CHADEMA iliiutangazia umma kuwa UCHAGUZI ULIKUA HURU NA HAKI.Licha ya madhira yote hayo lakini CHADEMA haikuwahi kususia uchaguzi. Chadema ilizidi kupambana hata sehemu ambayo ilikua haina ushawishi wa kushinda na hii ilipelekea CHADEMA kujijenga sana na kufika kwa watu wengi zaidi.HATUKUWAHI SIKIA CHADEMA INASUSA KISA NEC au sababu zozote zile,CHADEMA ilijikita HAKI inatafutwa kwa vyovyote vile.Hii ndio CHADEMA niliyoifahamu.

Hili la kususia uchaguzi mdogo NISEME TU UKWELI,LILIKUWA NI UPUMBAVU KIWANGO CHA MAKINIKIA.Kama nilivyosema hapo juu kuwa CHADEMA ilikua inashiriki chaguzi zote licha ya kutokuwa huru na Haki,CHADEMA ilikua inashiriki chaguzi hata sehemu zenye ushawishi mdogo.Pamoja na kushindwa lkn Iliweza kujitanua kisiasa zaidi.Sababu walizosusia uchaguzi ni za kipuuzi kabisa na Mimi kwa mtazamo wangu naondoa madai ya NEC ktk kususia uchaguzi.Sababu zinazoweza kuwa ni sahihi kwa wao kususia ni kama

1)Kuogopa kushindwa,Tunakumbuka baada ya Tamko la kususia uchaguzi, Singida waliteua Mgombea,Makada wakaanza kupinga kuwa ni NEC wamemweka na wanalazimisha CHADEMA waweke mgombea lkn baadae Mbowe akaja kuthibitisha kuwa Kamati ya Singida iliteua mgombea.Yaliibuka maswali mengi how Singida wawe kinyume na Tamko la kamati kuu Taifa?Haukupita mda jamaa akajitoa.

Singida ni ngome ya ccm na kwa hesabu Nyarandu ilitakiwa arudi kugombea.Baada ya mahesabu makali wakaona Nyarandu atoboi hata kwa dawa na kulinda Heshima yake na Chama wakaona Hakuna kusimamisha mgombea na Sababu watu wakaambiwa ni NEC.Hata kwa majimbo mengine waliyosusa sababu ni hiyo,Hakuna story za NEC kuwa mbovu.

2)Sababu hii inaweza tokea ktk mahesabu makali ya Sababu namba moja.Kutokuwa na fedha za kutosha kumudu chaguzi za marudio zote zilizokuwa mbele yao.Hivo wakaona waangalie ni wapi kwa fedha walizonazo wanaweza toboa.Kuingia kwenye uchaguzi tayari ni kuwekeza,tofauti na zamani walikua wanawekeza hata wasipopata kiti lkn wanapata wafuasi wengi kwa matumizi ya baadae,saizi wao mission ni kupata kiti tu.So kuwekeza kwenye jimbo unaloona huwezi pata kiti na fedha huna kwao ni hasara.

Na hizi sababu zote zinaleta picha ya CHADEMA kushiriki Uchaguzi wa Siha na Kinondoni.Washapima lkn NAAMINI WAMEPIMA VIBAYA,kuwa wanaamini watatoboa na hakutawahitaji fedha nyingi na ni rahisi kushinda. Hawajaleta mrejesho wa NEC kubadili mfumo lkn wanakuambia wanashiriki.Ukiuliza Sababu kutoka kwa wafuasi utaambiwa,lazima tupambane Hakuna kumwachia mtu apite kirahisi.Sababu mlizofanya washinde kirahisi longido,Songea na Singida ni zipi?Utaambulia matusi.

So utaona hiki chama hakijui kinasimamia nini zaidi ya kuendeshwa kwa HISIA NA MATUKIO.Kila Tamko linalotolewa na CHADEMA unatakiwa ulichuje kwanza maana unaweza jikuta hujui uko pande gani.Leo Hatushiriki Unashangilia,kesho tunashiriki Unashangilia.HIZI SIO AKILI ZA BINADAMU WA KAWAIDA.
Umeishia form ngapi?

Mwalimu nani aliyekufundisha kuchanganya herufi kubwa na ndogo?
 
Akili za wafuasi wa chadema hasa mitandaoni wanazijua wenyewe!!!
Ni mwanachama kindakindaki wa CCM kata ya Hananasifu Kinondoni anayejielewa sio kama nyie mnaoburuzwa na mkiti wenu, msikilize.

Anaitwa MacDonald Paschal Lunyilija.
Kadi no AB 1531040.
 
Back
Top Bottom