Kwanini CHADEMA ni muhimu ishiriki Uchaguzi wa Ukonga na Monduli licha ya uhalifu na udhalilishaji wa CCM, NEC na Polisi!

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,270
Nikope maneno ya tafsiri ya chama cha siasa kutoka katika kitabu cha "Mapambano ya Madaraka" (Yericko Nyerere, Sura 1, Uk 7. Toleo la 2018). "Chama cha kisiasa ni maungano ya watu wanaotafuta mamlaka katika dola na hasa serikali kwa kusudi la kutekeleza shabaha za kisiasa au za kifalsafa pamoja na faida kwa ajili ya vikundi fulani faida zao za binafsi.
Vyama mara nyingi hutamka mwelekeo au itikadi fulani inayoandikwa katika programu yao. Katika mfumo wa vyama vingi kila chama kinagombea nafasi za bunge au serikali dhidi ya vyama vingine. Wakati wa uchaguzi kila chama kinapaswa kujieleza, kutetea matendo yake ya nyuma na kuonyesha jinsi kinavyotaka kuboresha mambo tofauti na vyama vingine. Kwa njia hii kila chama huchangia harakati ya kujenga nia ya jamii inamofanya kazi kama inashinda au kushindwa kwenye uchaguzi".

Chadema ni chama cha siasa, hili lazima watu walielewe, Chadema sio kanisa wala msikiti kwamba uendeshaji wa shughuli zake utafuta kalenda ya biblia na ama kuruwani (Quran), laa hasha, Chama cha siasa kitafanya shuguli za siasa kwa tafsiri ya siasa tu na sio vinginevyo..
Wapo watu na pengine wengine ni wanachama kabisa wa Chadema, wanaona wanachanganywa na uamuzi huu wakizingatia uamuzi uliopita, Hawa si makosa yao, ni makosa ya kimazingira na elimu ndogo ya kisiasa kwa jamii zetu ambao wengi wamebobea kwenye uharakati na kuendesha maisha ya siasa kiharakati.

Huwezi kuwa mwanasiasa bila kwanza kuwa mwanaharaka, lakini unaweza kuwa mwanaharakati bila kuwa mwanasiasa, Siasa ni itikadi inayofuatwa na kundi au jamii fulani ambayo ni msingi wa kuendesha uchumi, utamaduni na mwenendo mzima maisha ya jamii hiyo. Siasa maana yake ni NJIA azitumiazo mtu au kundi la watu kupata nguvu na madaraka, na ikitokea mtu akapata nguvu hizo huendelea na hatua ya pili ya njia hizo ili kuhahihisha anabaki na nguvu zake au na madaraka yake kwa lengo la kuendelea kufanya kile alichokikusudia.

Kinachogomba hapo ni mamlaka/madaraka/nguvu azipatazo mwanasiasa anazitumia kwa maslahi ya nani. Katika tafasiri ya kijumla, Siasa ni mambo mengi lakini sio SAYANSI, Siasa ni medani ya mapambano ya kimadaraka (power struggle)

Kifalsafa Mwanasiasa ni adui wa uzalendo, simuumini wa uzalendo, huamini katika itikadi ya siasa ya chama chake. Uzalendo na siasa hukinzana lakini uzalendo huo huhanikizwa katika siasa. Uzalendo makazi yake ni kwa mwanaharakati na sio kwa mwanasiasa, lakini uzalendo huo hulindwa vema chini ya mwanasiasa madhubuti.

Mwanaharakati hunyooka kama kamba katika misimamo yake, na mwanasiasa hutembea katka fursa na za kisiasa akizingatia alama muhimu za nyakati. Chama cha siasa lengo ni kushika dola kwanza, kwa lengo la kuwatumikia watu wake kwamisingi ya itikadi na sera zake, na harakati na mwanaharakati lengo lake ni usawa wa maisha kati jamii na haki za kiraia zaidi tu.

Ikiwa tunakubaliana kuwa Siasa ni mambo mengi lakini sio SAYANSI, Siasa ni medani ya mapambano ya kimadaraka (power struggle), basi ni lazima tukubaliane kwamba tupo katika vita vya mapambano ya kimadaraka, njia za vita hazinyooki kama njia za fizikia au baolojia, vita ni fursa za kijeshi na lazima zitumiwe.

Ni Mtanzania ama ni mwanachadema mjinga tu na asiyelitakia mema taifa hili ndie atakayepinga njia wazitumiazo Chadema kuendesha siasa za Upinzani katika nyakati hizi ngumu za mkono wa chuma. Tunataka kulikomboa taifa toka mikononi mwa wahalifu ccm, kila nyenzo na njia iliyombele yetu tutaitumia na kila mwenye uthubutu tutakuwa nae, Chadema imeamua kushiriki uchaguzi wa Ukonga, na Monduli baada ya tafakuri ya mrejesho wa matokeo ya kata 77 na jimbo la Buyungu ambako hujuma na uhalifu dhidi ya ubinadamu vilitamalaki kisawasawa na chama chetu kuporwa ushindi waziwazi.

Hoja za msingi za Chadema katika uchaguzi zote na uchaguzi mkuu ni madai muhimu ya UMMA ambayo ni Katiba Mpya na Tume huru ya Uchaguzi ambapo Watendaji wa Serikali (Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi) kuingilia uchaguzi na kuvuruga uchaguzi, Vyombo vya dola kushiriki kuvunja haki za watu na sheria kiuchaguzi na ama kuratibu vurugu na kujeruhi watu na hasa kuwajeruhi makada wa vyama pinzani. Hoja hizi zilisimamiwa na zitaendelea kusimamiwa na Chadema, Chama kikitaka pawepo na majadiliano na wadau wa uchaguzi kabla ya kurudia hizi chaguzi za manunuzi ya lumumba na kabla ya Uchaguzi wa 2020.

Tunataka kushika dola, nilazima dunia ijue hili na ijue uhalifu wowote unaotendeka nchini linapokuja suala la chaguzi, Dunia haitajua kama Chadema hatushiriki Chaguzi hata kama tunaporwa kweupe. Kupitia uchaguzi mdogo ulioisha na yaliyojiri, wahisani wa maendeleo wa nchi yaani Marekani wamejua yaliyotokea na wametoa maoni yao, maoni hayo sio kama yale ya Twaweza ambao tunaweza kuwatishia na kusema wajieleze uhalali wao, Sahau hilo, hii ni USA, kinyume chake utajieleza wewe kwanini unavunja haki za binadamu na utawala wa sheria.

Tunaingia uchaguzi mwingine tukijua wazi ccm wanaingia wakiwa na matokeo yao mkononi waliyoyasaini kabisa, lakini sasa tunaingia huku jicho la dunia yaani wahisani wa bajeti wale wanaochangia bajeti yetu, wale tunawaabudu kwakusema "Kwahisani ya Watu wa Marekani", na sasa hatakuwa Marekani tu, bali Umoja wa Ulaya kwa ujumla watafuatilia uchaguzi huu kwa lengo moja tu, nalo ni kujiridhisha kauli ya Marekani kwamba kweli Tanzania kuna uvunjifu wa haki za binadamu na utawala wa sheria katika chaguzi hizi? Chadema tunashiriki, tena kwa nguvu zote, sasa tuna Political Legitimacy, huku wenzetu wakibaki na Legal Legitimacy tu.

Katika mfumo wa vyama vingi Chama kilicho nje ya madaraka huwa na Political Legitimacy pekee wakati chama kilicho madarakani huwa na Political Legitimacy na legal legitimacy. CCM imepoteza Political Legitimacy, imebaki na Legal Legitimacy pekee ambapo chama kilicho madarakani kikifikia hali hiyo, msaada wacho huwa ni kutumia vyombo vya dola tu kubaki madarakani. Katika mizani hii Chadema tuna wajibu wakuilinda Political Legitimacy kwa kucheza siasa za viwango vya kimataifa, na mbinu zetu zitabadilika kulingana wakati na mazingira husika. Kitendo cha kususia uchaguzi ule wa marudio ya 2017 kabla ule wa mauaji ya Akwilina, tulituma ujumbe mkubwa sana kwa wananchi, na kwa wadau wa uchaguzi, ilikuja kudhihirika pale tulipona wazi tume inakiri watendaji wa serikali wanaingilia uchaguzi, hili ni jambo ambalo kabla ya mgomo ule hungelisikia likisemwa na tume popote. Tumerejea kwenye uchaguzi lakini hali imekuwa ileile, mabadiliko makubwa ni kuwa Dunia sasa inatumulika hata tuchomwe visu gizani na Green Guard.

Leo Chadema tumepata wagombea sahihi kule Ukonga tuna kamanda Asia Msangi, Korogwe tuna Kamanda Aminata Saguti na Monduli tuna kamanda Yonas M. Laizer, Kwa mjibu wa Katiba ya Chadema Kamati kuu ndio yenye wajibu wa kuteua mgombea wa ubunge na urais, Jopo la watu makini weledi na wenye hekima za juu kabisa wanaoijua siasa ngumu na nyepesi, wakiwa zaidi ya 30, wamekutana wakiunda kamati kuu, wametuletea majabali wa siasa za ujana. Tunayo kila sababu ya kusonga mbele na kuhubiri ushindi bila kuingia kwenye mkumbo wa propaganda za maadui zetu....

Na Yericko Nyerere
IMG_20180816_205015_125.jpg

FB_IMG_1534442678760.jpg
 
Nikope maneno ya tafsiri ya chama cha siasa kutoka katika kitabu cha "Mapambano ya Madaraka" (Yericko Nyerere, Sura 1, Uk 7. Toleo la 2018). "Chama cha kisiasa ni maungano ya watu wanaotafuta mamlaka katika dola na hasa serikali kwa kusudi la kutekeleza shabaha za kisiasa au za kifalsafa pamoja na faida kwa ajili ya vikundi fulani faida zao za binafsi.
Vyama mara nyingi hutamka mwelekeo au itikadi fulani inayoandikwa katika programu yao. Katika mfumo wa vyama vingi kila chama kinagombea nafasi za bunge au serikali dhidi ya vyama vingine. Wakati wa uchaguzi kila chama kinapaswa kujieleza, kutetea matendo yake ya nyuma na kuonyesha jinsi kinavyotaka kuboresha mambo tofauti na vyama vingine. Kwa njia hii kila chama huchangia harakati ya kujenga nia ya jamii inamofanya kazi kama inashinda au kushindwa kwenye uchaguzi".

Chadema ni chama cha siasa, hili lazima watu walielewe, Chadema sio kanisa wala msikiti kwamba uendeshaji wa shughuli zake utafuta kalenda ya biblia na ama kuruwani (Quran), laa hasha, Chama cha siasa kitafanya shuguli za siasa kwa tafsiri ya siasa tu na sio vinginevyo..
Wapo watu na pengine wengine ni wanachama kabisa wa Chadema, wanaona wanachanganywa na uamuzi huu wakizingatia uamuzi uliopita, Hawa si makosa yao, ni makosa ya kimazingira na elimu ndogo ya kisiasa kwa jamii zetu ambao wengi wamebobea kwenye uharakati na kuendesha maisha ya siasa kiharakati.

Huwezi kuwa mwanasiasa bila kwanza kuwa mwanaharaka, lakini unaweza kuwa mwanaharakati bila kuwa mwanasiasa, Siasa ni itikadi inayofuatwa na kundi au jamii fulani ambayo ni msingi wa kuendesha uchumi, utamaduni na mwenendo mzima maisha ya jamii hiyo. Siasa maana yake ni NJIA azitumiazo mtu au kundi la watu kupata nguvu na madaraka, na ikitokea mtu akapata nguvu hizo huendelea na hatua ya pili ya njia hizo ili kuhahihisha anabaki na nguvu zake au na madaraka yake kwa lengo la kuendelea kufanya kile alichokikusudia.

Kinachogomba hapo ni mamlaka/madaraka/nguvu azipatazo mwanasiasa anazitumia kwa maslahi ya nani. Katika tafasiri ya kijumla, Siasa ni mambo mengi lakini sio SAYANSI, Siasa ni medani ya mapambano ya kimadaraka (power struggle)

Kifalsafa Mwanasiasa ni adui wa uzalendo, simuumini wa uzalendo, huamini katika itikadi ya siasa ya chama chake. Uzalendo na siasa hukinzana lakini uzalendo huo huhanikizwa katika siasa. Uzalendo makazi yake ni kwa mwanaharakati na sio kwa mwanasiasa, lakini uzalendo huo hulindwa vema chini ya mwanasiasa madhubuti.

Mwanaharakati hunyooka kama kamba katika misimamo yake, na mwanasiasa hutembea katka fursa na za kisiasa akizingatia alama muhimu za nyakati. Chama cha siasa lengo ni kushika dola kwanza, kwa lengo la kuwatumikia watu wake kwamisingi ya itikadi na sera zake, na harakati na mwanaharakati lengo lake ni usawa wa maisha kati jamii na haki za kiraia zaidi tu.

Ikiwa tunakubaliana kuwa Siasa ni mambo mengi lakini sio SAYANSI, Siasa ni medani ya mapambano ya kimadaraka (power struggle), basi ni lazima tukubaliane kwamba tupo katika vita vya mapambano ya kimadaraka, njia za vita hazinyooki kama njia za fizikia au baolojia, vita ni fursa za kijeshi na lazima zitumiwe.

Ni Mtanzania ama ni mwanachadema mjinga tu na asiyelitakia mema taifa hili ndie atakayepinga njia wazitumiazo Chadema kuendesha siasa za Upinzani katika nyakati hizi ngumu za mkono wa chuma. Tunataka kulikomboa taifa toka mikononi mwa wahalifu ccm, kila nyenzo na njia iliyombele yetu tutaitumia na kila mwenye uthubutu tutakuwa nae, Chadema imeamua kushiriki uchaguzi wa Ukonga, na Monduli baada ya tafakuri ya mrejesho wa matokeo ya kata 77 na jimbo la Buyungu ambako hujuma na uhalifu dhidi ya ubinadamu vilitamalaki kisawasawa na chama chetu kuporwa ushindi waziwazi.

Hoja za msingi za Chadema katika uchaguzi zote na uchaguzi mkuu ni madai muhimu ya UMMA ambayo ni Katiba Mpya na Tume huru ya Uchaguzi ambapo Watendaji wa Serikali (Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi) kuingilia uchaguzi na kuvuruga uchaguzi, Vyombo vya dola kushiriki kuvunja haki za watu na sheria kiuchaguzi na ama kuratibu vurugu na kujeruhi watu na hasa kuwajeruhi makada wa vyama pinzani. Hoja hizi zilisimamiwa na zitaendelea kusimamiwa na Chadema, Chama kikitaka pawepo na majadiliano na wadau wa uchaguzi kabla ya kurudia hizi chaguzi za manunuzi ya lumumba na kabla ya Uchaguzi wa 2020.

Tunataka kushika dola, nilazima dunia ijue hili na ijue uhalifu wowote unaotendeka nchini linapokuja suala la chaguzi, Dunia haitajua kama Chadema hatushiriki Chaguzi hata kama tunaporwa kweupe. Kupitia uchaguzi mdogo ulioisha na yaliyojiri, wahisani wa maendeleo wa nchi yaani Marekani wamejua yaliyotokea na wametoa maoni yao, maoni hayo sio kama yale ya Twaweza ambao tunaweza kuwatishia na kusema wajieleze uhalali wao, Sahau hilo, hii ni USA, kinyume chake utajieleza wewe kwanini unavunja haki za binadamu na utawala wa sheria.

Tunaingia uchaguzi mwingine tukijua wazi ccm wanaingia wakiwa na matokeo yao mkononi waliyoyasaini kabisa, lakini sasa tunaingia huku jicho la dunia yaani wahisani wa bajeti wale wanaochangia bajeti yetu, wale tunawaabudu kwakusema "Kwahisani ya Watu wa Marekani", na sasa hatakuwa Marekani tu, bali Umoja wa Ulaya kwa ujumla watafuatilia uchaguzi huu kwa lengo moja tu, nalo ni kujiridhisha kauli ya Marekani kwamba kweli Tanzania kuna uvunjifu wa haki za binadamu na utawala wa sheria katika chaguzi hizi? Chadema tunashiriki, tena kwa nguvu zote, sasa tuna Political Legitimacy, huku wenzetu wakibaki na Legal Legitimacy tu.

Katika mfumo wa vyama vingi Chama kilicho nje ya madaraka huwa na Political Legitimacy pekee wakati chama kilicho madarakani huwa na Political Legitimacy na legal legitimacy. CCM imepoteza Political Legitimacy, imebaki na Legal Legitimacy pekee ambapo chama kilicho madarakani kikifikia hali hiyo, msaada wacho huwa ni kutumia vyombo vya dola tu kubaki madarakani. Katika mizani hii Chadema tuna wajibu wakuilinda Political Legitimacy kwa kucheza siasa za viwango vya kimataifa, na mbinu zetu zitabadilika kulingana wakati na mazingira husika. Kitendo cha kususia uchaguzi ule tumetuma ujumbe mkubwa sana kwa wananchi, na kwa wadau wa uchaguzi, leo unaona wazi tume inakiri watendaji wa serikali wanaingilia uchaguzi, hili ni jambo ambalo kabla ya mgomo ule hungelisikia likisemwa na tume popote.

Leo Chadema tumepata wagombea sahihi kule Ukonga tuna kamanda Asia Msangi na Monduli tuna kamanda Yonas M. Laizer, Kwa mjibu wa Katiba ya Chadema Kamati kuu ndio yenye wajibu wa kuteua mgombea wa ubunge na urais, Jopo la watu makini weledi na wenye hekima za juu kabisa wanaoijua siasa ngumu na nyepesi, wakiwa zaidi ya 30, wamekutana wakiunda kamati kuu, wametuletea majabali wa siasa za ujana. Tunayo kila sababu ya kusonga mbele na kuhubiri ushindi bila kuingia kwenye mkumbo wa propaganda za maadui zetu....

Na Yericko Nyerere
Chadema iende mbali zaidi. Pamoja na kuwa international observers hawahusiki na chaguzi hizi za marudio, let them be notified kuwa tunaenda kwenye uchaguzi being aware of the last gross human right violation in the last elections. Iambie dunia kuwa tunakwenda, tunaomba mkemee haya, just to alert them, ingawa hawezi kuingilia. Nakubaliana na wewe! Waende mbali zaidi!
 
Achen bla bla blaa , kila siku mnalialia tu, mnapoteza hela kwenye chaguz mnazojua mnaenda kusindikiza, kwann hiyo hela msijengee ofisi?
 
Nikope maneno ya tafsiri ya chama cha siasa kutoka katika kitabu cha "Mapambano ya Madaraka" (Yericko Nyerere, Sura 1, Uk 7. Toleo la 2018). "Chama cha kisiasa ni maungano ya watu wanaotafuta mamlaka katika dola na hasa serikali kwa kusudi la kutekeleza shabaha za kisiasa au za kifalsafa pamoja na faida kwa ajili ya vikundi fulani faida zao za binafsi.
Vyama mara nyingi hutamka mwelekeo au itikadi fulani inayoandikwa katika programu yao. Katika mfumo wa vyama vingi kila chama kinagombea nafasi za bunge au serikali dhidi ya vyama vingine. Wakati wa uchaguzi kila chama kinapaswa kujieleza, kutetea matendo yake ya nyuma na kuonyesha jinsi kinavyotaka kuboresha mambo tofauti na vyama vingine. Kwa njia hii kila chama huchangia harakati ya kujenga nia ya jamii inamofanya kazi kama inashinda au kushindwa kwenye uchaguzi".

Chadema ni chama cha siasa, hili lazima watu walielewe, Chadema sio kanisa wala msikiti kwamba uendeshaji wa shughuli zake utafuta kalenda ya biblia na ama kuruwani (Quran), laa hasha, Chama cha siasa kitafanya shuguli za siasa kwa tafsiri ya siasa tu na sio vinginevyo..
Wapo watu na pengine wengine ni wanachama kabisa wa Chadema, wanaona wanachanganywa na uamuzi huu wakizingatia uamuzi uliopita, Hawa si makosa yao, ni makosa ya kimazingira na elimu ndogo ya kisiasa kwa jamii zetu ambao wengi wamebobea kwenye uharakati na kuendesha maisha ya siasa kiharakati.

Huwezi kuwa mwanasiasa bila kwanza kuwa mwanaharaka, lakini unaweza kuwa mwanaharakati bila kuwa mwanasiasa, Siasa ni itikadi inayofuatwa na kundi au jamii fulani ambayo ni msingi wa kuendesha uchumi, utamaduni na mwenendo mzima maisha ya jamii hiyo. Siasa maana yake ni NJIA azitumiazo mtu au kundi la watu kupata nguvu na madaraka, na ikitokea mtu akapata nguvu hizo huendelea na hatua ya pili ya njia hizo ili kuhahihisha anabaki na nguvu zake au na madaraka yake kwa lengo la kuendelea kufanya kile alichokikusudia.

Kinachogomba hapo ni mamlaka/madaraka/nguvu azipatazo mwanasiasa anazitumia kwa maslahi ya nani. Katika tafasiri ya kijumla, Siasa ni mambo mengi lakini sio SAYANSI, Siasa ni medani ya mapambano ya kimadaraka (power struggle)

Kifalsafa Mwanasiasa ni adui wa uzalendo, simuumini wa uzalendo, huamini katika itikadi ya siasa ya chama chake. Uzalendo na siasa hukinzana lakini uzalendo huo huhanikizwa katika siasa. Uzalendo makazi yake ni kwa mwanaharakati na sio kwa mwanasiasa, lakini uzalendo huo hulindwa vema chini ya mwanasiasa madhubuti.

Mwanaharakati hunyooka kama kamba katika misimamo yake, na mwanasiasa hutembea katka fursa na za kisiasa akizingatia alama muhimu za nyakati. Chama cha siasa lengo ni kushika dola kwanza, kwa lengo la kuwatumikia watu wake kwamisingi ya itikadi na sera zake, na harakati na mwanaharakati lengo lake ni usawa wa maisha kati jamii na haki za kiraia zaidi tu.

Ikiwa tunakubaliana kuwa Siasa ni mambo mengi lakini sio SAYANSI, Siasa ni medani ya mapambano ya kimadaraka (power struggle), basi ni lazima tukubaliane kwamba tupo katika vita vya mapambano ya kimadaraka, njia za vita hazinyooki kama njia za fizikia au baolojia, vita ni fursa za kijeshi na lazima zitumiwe.

Ni Mtanzania ama ni mwanachadema mjinga tu na asiyelitakia mema taifa hili ndie atakayepinga njia wazitumiazo Chadema kuendesha siasa za Upinzani katika nyakati hizi ngumu za mkono wa chuma. Tunataka kulikomboa taifa toka mikononi mwa wahalifu ccm, kila nyenzo na njia iliyombele yetu tutaitumia na kila mwenye uthubutu tutakuwa nae, Chadema imeamua kushiriki uchaguzi wa Ukonga, na Monduli baada ya tafakuri ya mrejesho wa matokeo ya kata 77 na jimbo la Buyungu ambako hujuma na uhalifu dhidi ya ubinadamu vilitamalaki kisawasawa na chama chetu kuporwa ushindi waziwazi.

Hoja za msingi za Chadema katika uchaguzi zote na uchaguzi mkuu ni madai muhimu ya UMMA ambayo ni Katiba Mpya na Tume huru ya Uchaguzi ambapo Watendaji wa Serikali (Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi) kuingilia uchaguzi na kuvuruga uchaguzi, Vyombo vya dola kushiriki kuvunja haki za watu na sheria kiuchaguzi na ama kuratibu vurugu na kujeruhi watu na hasa kuwajeruhi makada wa vyama pinzani. Hoja hizi zilisimamiwa na zitaendelea kusimamiwa na Chadema, Chama kikitaka pawepo na majadiliano na wadau wa uchaguzi kabla ya kurudia hizi chaguzi za manunuzi ya lumumba na kabla ya Uchaguzi wa 2020.

Tunataka kushika dola, nilazima dunia ijue hili na ijue uhalifu wowote unaotendeka nchini linapokuja suala la chaguzi, Dunia haitajua kama Chadema hatushiriki Chaguzi hata kama tunaporwa kweupe. Kupitia uchaguzi mdogo ulioisha na yaliyojiri, wahisani wa maendeleo wa nchi yaani Marekani wamejua yaliyotokea na wametoa maoni yao, maoni hayo sio kama yale ya Twaweza ambao tunaweza kuwatishia na kusema wajieleze uhalali wao, Sahau hilo, hii ni USA, kinyume chake utajieleza wewe kwanini unavunja haki za binadamu na utawala wa sheria.

Tunaingia uchaguzi mwingine tukijua wazi ccm wanaingia wakiwa na matokeo yao mkononi waliyoyasaini kabisa, lakini sasa tunaingia huku jicho la dunia yaani wahisani wa bajeti wale wanaochangia bajeti yetu, wale tunawaabudu kwakusema "Kwahisani ya Watu wa Marekani", na sasa hatakuwa Marekani tu, bali Umoja wa Ulaya kwa ujumla watafuatilia uchaguzi huu kwa lengo moja tu, nalo ni kujiridhisha kauli ya Marekani kwamba kweli Tanzania kuna uvunjifu wa haki za binadamu na utawala wa sheria katika chaguzi hizi? Chadema tunashiriki, tena kwa nguvu zote, sasa tuna Political Legitimacy, huku wenzetu wakibaki na Legal Legitimacy tu.

Katika mfumo wa vyama vingi Chama kilicho nje ya madaraka huwa na Political Legitimacy pekee wakati chama kilicho madarakani huwa na Political Legitimacy na legal legitimacy. CCM imepoteza Political Legitimacy, imebaki na Legal Legitimacy pekee ambapo chama kilicho madarakani kikifikia hali hiyo, msaada wacho huwa ni kutumia vyombo vya dola tu kubaki madarakani. Katika mizani hii Chadema tuna wajibu wakuilinda Political Legitimacy kwa kucheza siasa za viwango vya kimataifa, na mbinu zetu zitabadilika kulingana wakati na mazingira husika. Kitendo cha kususia uchaguzi ule wa marudio ya 2017 kabla ule wa mauaji ya Akwilina, tulituma ujumbe mkubwa sana kwa wananchi, na kwa wadau wa uchaguzi, ilikuja kudhihirika pale tulipona wazi tume inakiri watendaji wa serikali wanaingilia uchaguzi, hili ni jambo ambalo kabla ya mgomo ule hungelisikia likisemwa na tume popote. Tumerejea kwenye uchaguzi lakini hali imekuwa ileile, mabadiliko makubwa ni kuwa Dunia sasa inatumulika hata tuchomwe visu gizani na Green Guard.

Leo Chadema tumepata wagombea sahihi kule Ukonga tuna kamanda Asia Msangi na Monduli tuna kamanda Yonas M. Laizer, Kwa mjibu wa Katiba ya Chadema Kamati kuu ndio yenye wajibu wa kuteua mgombea wa ubunge na urais, Jopo la watu makini weledi na wenye hekima za juu kabisa wanaoijua siasa ngumu na nyepesi, wakiwa zaidi ya 30, wamekutana wakiunda kamati kuu, wametuletea majabali wa siasa za ujana. Tunayo kila sababu ya kusonga mbele na kuhubiri ushindi bila kuingia kwenye mkumbo wa propaganda za maadui zetu....

Na Yericko Nyerere
Mkuu Yeriko upo sawa lkn kulingana na hali halisi huo uchaguzi hauna umuhimu cha muhimu ni kuwajenga wanachama wa vyama vya upinzani kuelewa hali halisi ilivyo nchini hasa vijijini kwani kwa mjini tayari wote ni wapinzani tu
 
Chadema wameacha kufanyia kikao kwenye banda la ufipa , wameenda kufanyia kwenye five star hotel ambayo wanalipa dollar 100 kwa saa.!!!

Kwa nn bavicha msihoji haya??
 
Hata mimi naunga mkono washiriki ili hujuma ziwe wazi. Kisha wapiga kura tuzidi kuwa wachache kuonyesha kwamba ccm haikubaliki.
 
Chadema wameacha kufanyia kikao kwenye banda la ufipa , wameenda kufanyia kwenye five star hotel ambayo wanalipa dollar 100 kwa saa.!!!

Kwa nn bavicha msihoji haya??

Unashanga cdm kufanyia hotelini wanapolipa mpaka kodi, hushangai ccm kufanyia vikao ikulu?
 
Kwa nn cdm wasifanyie ufipa?

Wamevunja sheria gani kufanyia mkutano kwenye ukumbi wa mikutano? Wangefanyia kwenye nyumba ya ibada hapo ungepaswa kuhoji. Unalazimishia sababu hata wenzio wamebaki wanakusanifu tu. Kama umeishiwa hoja kalale kwani hata kesho ni siku.
 
Wewe ulisha dharaulika kitambo
Swali fupi kwa Yeriko kwa nini chadema mligoma kumpa nyalandu form kugombea ubunge wabaguzi wakubwa nyie.Kwingine ruksa nyalandu mlimfanyia unyama yaani why kama mko consistent for legitimacy?
 
Back
Top Bottom