Kwanini CHADEMA na wafuasi wake wanakuwa kitu kimoja na serikali kwenye suala la sensa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini CHADEMA na wafuasi wake wanakuwa kitu kimoja na serikali kwenye suala la sensa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ritz, Sep 1, 2012.

 1. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Siku zote Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, wamekuwa wapingaji wakubwa wa serikali ya chama cha mapinduzi CCM imefikia wakati mpaka viongozi wa Chadema Dr. Slaa, pamoja na Freeman Mbowe kutamka kuwa hawana imani na serikali pamoja na vyombo vya usalama, John Mnyika naye kutamka serikali ya Kikwete ni dhaifu.

  Chadema walipinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa rais, Chadema walipinga mchakato mzima wa katiba, Chadema walipinga mpango wa kilimo kwanza, Chadema walikuwa wanaipinga serekali kwenye mgongoro wa madaktari, Chadema walikuwa wakiipinga serikali kwenye mgogoro wa walimu.

  Lakini lilipokuja suala la sensa Chadema na viongozi wao pamoja na wafuasi wao karibia wote walikuwa bega kwa bega na serikali ya CCM kushirikiana kufanikisha zoezi la sensa na Chadema pamoja na wafuasi wao ndio wamekuwa wa kwanza kupambana na yeyote anayepinga zoezi la sensa.

  Kwa nini Chadema wameungana na serikali ya CCM kwenye zoezi la sensa ni maslahi yapi wanayoyapata kama chama cha siasa.
   
 2. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  :yawn::yawn:
  :sleepy::sleepy:
   
 3. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #3
  Sep 1, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Ni suala lenye tija, huwa tunapinga ujinga tu.
   
 4. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #4
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Sikuwahi kufikiria kuwa hata wewe Ritz upo katika kundi la hawa watu, though covertly presented,the message behind your post is overt,MUNGU atufungue akili tuweze kuona,kuutambua na kuukubali ukweli!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Escobar

  Escobar JF-Expert Member

  #5
  Sep 1, 2012
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 576
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 60
  For what i know CHADEMA ni chama chenye watu makini na wenye nia ya dhati ya kuleta maendeleo katika taifa la watu waliokata tamaa! So, for that case CDM hawawezi kupinga kitu chenye maslahi kitaifa kama sensa na isitoshe CHADEMA ni chama kinachojiandaa kuchukua dola hivyo takwimu zitakazo patikana zitasaidia kutekeleza mipango ya maendeleo ya serikali ijayo. Kuhusu suala la kilimo kwanza si CDM tu wanaolipinga, hata swahiba wa mwenye sera Mr Lowassa a.k.a Waziri mkuu mstaafu hakubaliani nalo. Katika kumbukumbu zangu sijawahi kuwaona CDM wakipinga kitu chenye maslahi kitaifa na wasiwe na sababu za msingi! Ni hayo tu
   
 6. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #6
  Sep 1, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  Inaonesha kwamba jk yuko nyuma au anasimamia ugomaji wa sensa. Cdm wanajua umuhimu wa sensa kama ikifanyika kwa malengo kusudiwa. Hakuna mtu asiyejua umuhimu wa sensa isipokuwa nyie mnaotaka kodi zetu zitumike kuwahesabia na waumini wasiokuja msikitini. Makanisani cku hizi wanahesabu waumini waliohudhuria kila j2,at least wanakuwa na average ya waumini wao.
   
 7. B

  Babuu Rogger JF-Expert Member

  #7
  Sep 1, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 80
  Ndio maana unaambiwa CHADEMA ni chama makini. kwenye uonevu lazima wapinge.
   
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  Sep 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hii sensa ya mwaka huu imetuumbua sana sisi Tanzania. 2012 bado kuna watu wanahoji umuhimu wa sensa? Tunaonekana kama 'primitive' society - what a shame?
   
 9. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #9
  Sep 1, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Samahani, kuna tamko lolote liliwahi kutolewa na Chadema kuhusu ku'suport au kupinga sensa?
   
 10. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #10
  Sep 1, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Ritz Sijui kama nimeelewa the underlying reasons za wewe kuuliza hili; Ila tu msingi nisema saa ingine huwa kuna sababu ya viongozi ambazo huwa nazo na mwananchi wa kawaida asiweze kutambua.

  Ila tu Kwa hili nawapongeza sana CDM mana wangetaka kuchangia kwa kiasi kikubwa hii sensa isifanyike wangefaulu katika hilo, ingekuwa balaa hasa tukiongezea swala la viongozi wetu wengi wa dini ya Kiislamu kupingana na hilo.

  Kama kweli you are curious mie naweza sema kuwa zifuatazo ni sababu;

  1. Wanatambua umuhimu wa sensa, kuwa sio kwa ajili ya CCM ni kwa kiasi kikubwa ni kwa ajili ya maendeleo ya nchi na sio chama.
  2. Wana confidence sana kuwa 2015 Uongozi ni wao. Tokana na kuwa kumekuwa na ubabaishaji sana wa takwimu ya idadi ya wananchi Tanzania ni ngapi wameona ni bora wasaidie ku support katika kuhakikisha zoezi linaenda sawa; swala ambalo ni muhimu sana kwa uongozi kutambua endapo kweli wanataka kuleta maendeleo zaidi.

  Hata hivo naomba nitoke nje ya mada kidogo Ritz... Naomba maoni yako ya baadhi ya viongozi wa CCM kukiuka matakwa ya Serkali kusimamisha shughuli zozote ambazo zinaweza kwamisha uhesabuji wa sensa. Wakiwa kama viongozi wa Serkali husika chini ya CCM, Kwa nini unadhani walikaidi na kuendelea? Au ni uongozi wa CCM waliwaagiza kukaidi ili kutuma ujumbe fulani?
   
 11. Ngongoseke

  Ngongoseke JF-Expert Member

  #11
  Sep 1, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 3,212
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wanadhihirisha jinsi gani wanachuki na uislam na kama waislam wote wangesapoti sensa basi cdm na wapambe wao pia wangeipinga sensa haina haja kuumiza kichwa waislam wanaijua cdm vizuri na malengo yao wanayajua'tusubiri 2015 jibu litapatikana kama wao wanaweza kuingia ikulu kwa kura zao tu'
   
 12. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #12
  Sep 1, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,539
  Likes Received: 10,461
  Trophy Points: 280
  chadema wanatabu mwaka huu... Madhaifu yote ya serika li wanabebeshwa chadema...! Ama kweli utu uzima jalala.
   
 13. only83

  only83 JF-Expert Member

  #13
  Sep 1, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Unajua sijui ubongo wako kama upo salama, hivi kwa umri huo hujui maana ya sensa? Ulitaka CHADEMA wapinge sensa ili iweje?
   
 14. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #14
  Sep 1, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Sensa ni jambo lenye manufaa kwa nchi,na CDM kama chama makini ni lazima kusupport.
   
 15. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #15
  Sep 1, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Ritz bwana, Mbona huwa wakihamasisha wananchi kulinda kura zao mpaka matokeo yatakapotangazwa huwa hauulizi ni kwa nini?
   
 16. engwe1980

  engwe1980 Member

  #16
  Sep 1, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 53
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  CDM inaweka maslahi ya Taifa mbele siyo unakurupuka tu na kusema inaungana na CCM kwenye sensa. Sensa ni suala muhimu kwa maslahi ya nchi
   
 17. engwe1980

  engwe1980 Member

  #17
  Sep 1, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 53
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sangarara jua Ritz anazeeka vibaya na nina shaka kifo chake pia kitakuwa kibaya!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #18
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Naimani huyu jamaa ana akili timamu kabisa,
  ila kazipeleka likizo na kuficha udini ndani ya post yake.
  Anataka kusema chadema haipingi zoezi la sensa kwa sababu
  waislamu wana ipinga.

  Kwa mtu mwenye akili timamu kabisa,hawezi kupinga sensa maana
  hata wauza gongo wana tamani sana kujua eneo gani lina watu wengi
  ili waweke huko biashara zao.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #19
  Sep 1, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  AdhaDii. unamuuliza Ritz swali? He will never answer you. Hakubarikiwa na busara za kujibu watu, popote na chochote anachokijua kwenye maisha yake ni kulalamika lalamika tu, mlalamishiiiiiiiiiiiii.
   
 20. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #20
  Sep 1, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ritz usisahau kwamba tunajiandaa kuchukua uongozi wa nchi mwaka 2015 kwahiyo zoezi hili la sensa ni muhimu sana kwetu ili tutakapoingia madarakani tutakuwa na uhakika na idadi ya watanzania tutakaotakiwa kuwahudumia.

  Lakini nikukumbushe tena kwamba siku zote Chadema tunaunga mkono mambo ya msingi tu yanayofanywa na serikali kwa ajili ya manufaa ya watanzania. Kama una kumbukumbu nzuri kuna mambo mengi tu tumepata kuyaunga mkono kwa maslahi mapana ya watanzania.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...