Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Tangu Rais Magufuli aingie madarakani, chama kikuu cha upinzani nchini, CHADEMA wameshindwa kabisa kufurukuta na kujenga hoja ya kuungwa mkono na Watanzania juu ya Utendaji wa Rais Magufuli. Ilizoeleka hapo awali kuwa CHADEMA walijikita katika kukosoa utendaji wa Serikali zilizopita. This time around, CHADEMA hawana tena nguvu wala tashwishwi ya kumshambulia Rais kwa muktadha wa utendaji wake.
Nashindwa kuelewa nini kimewakumba hawa ndugu zetu wa upinzani. Zitto Kabwe alijaribu kufurukuta wakati wa ununuzi wa Bombardier. Hata hivyo naye kwa sasa ni kama hayupo. Kwa sasa wanavizia tu nini Rais anaongea. Niliwahi kuandika humu kuwa ikitokea Rais akageuka kuwa bubu sijui CHADEMA na upinzani watakuwa na hoja gani.
Niwasihi ndugu zangu wa CHADEMA, fanyeni kazi ya upinzani. Majungu na mipasho waachieni akina Mzee Yusuph. Ndo tunakaribia 2020. Magufuli na Serikali yake yupo busy kutekeleza Ilani na ahadi zake ili ikifika 2020 awe amezimaliza. Dalili zinaonesha atazimaliza kabla ya mwaka huo.
Jiandaeni kuyatema majimbo mengi mnayoshikilia kwa sasa