The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,355
- 17,321
Nakumbuka mara baada ya uchaguzi wa mwaka 2015 chadema walianza kashfa dhidi ya wasukuma, walianza kutengeneza kila aina ya kashfa dhidi ya wasukuma kwa sababu ya wingi wa kura aliopewa Magufuli na watu wa kanda ya ziwa.Ni rahisi sana kuelewa machungu ya viongozi wa Chadema na wafuasi wake kufuatia kushindwa Uchaguzi wa mwaka 2015.
Laukama sii Ukanda wa Ziwa kumpa kura nyingi Magufuli na Chama cha CCM, Magufuli asingeshinda Uchaguzi huo. Ukanda wa ziwa ndio ulomaliza ubishi wote Uchaguzi wa 2015 na Chadema hawakutegemea kabisa.
Kwa hiyo Chadema wana hasira sana na Ukanda wa ziwa na sijui nani alowambia Wasukuma ndio wenyeji, ndio kabila pekee au basi tu wamechukulia yeye Msukuma basi walobakia woote huko ni Wasukuma.
Na hata Ukitazama Asili ya wakazi wa Chato haikuwa Wasukuma bali wenyeji wake waliitwa Wazinza! Haawana Ukaribu kama vile Wapare na Wachagga! Leo hii hatuwezi kusema wakazi wa Chato ni kabila fulani au gani maanake yapo Makabila yote mchanganyiko. Historia Chato haikuwa Mkoa wa Mwanza wala Shinyanga bali ilikuwa kijiji wilaya ya Biharamulo, Mkoa wa Ziwa Mgharibi (Kagera).
Kama Hayati angewapendelea kweli Wasukuma nadhani angekuwa na wakati mgumu sana maanake Wasukuma ni wenyeji wa Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Geita, Tabora na Simiyu.
Kwa takwimu za NEC, bado kanda ya ziwa ndio itaweza ku determine urais wa nchi hii maana ina watu wengi kuliko kanda yoyote ile.
Sasa Chadema badala wajikite kutaka kuelewana na watu wa kanda ya ziwa ama wasukuma kama wanavyowaita, wao wanawakashfu, wanawadhihaki. Chadema wasubiri mwaka 2025 wainamishwe na kushikishwa ukuta waje kulalamika wameibiwa kura.