Kwanini CCM wanasisimuliwa na ugandamizaji?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
17,871
33,236
Huwa sielewi ni kwa nini Viongozi na wanachama wa CCM huwa wanasisimuliwa sana na maneno na matendo ya kiugandamizaji.

Kwa mfano huwezi kuamini inakuwaje wabunge wa CCM wengi wao wanakuwa kinyume na Mbunge Mwenzao Tundu Lissu wakati wanajua kabisa alishambuliwa nusura auawe. Ukiwasikiliza Wabunge wa CCM baadhi yao utaona ni kama vile wanafurahia kushambuliwa kwa Lissu.

Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambao wengi wao kama siyo wote ni wana CCM, mara nyingi sana matamko yao huwa ni yenye kuashiria kutumia nguvu ndiyo sura halisi ya dola dhidi ya wananchi.

Mitaani wafuasi na wananchama wa CCM wao huwa wanaona sawa tu kutumia nguvu dhidi ya nguvu za hoja za wapinzani wao. Kule Zanzibar kuna watu hadi wamepachikwa jina la "Zombie" na ni watu wenye matendo mabaya sana dhidi ya wale wasio wana-CCM wenzao.

Hata kufananisha uongozi na viongozi wa CCM ni rahisi sana kulinganisha viongozi wao na viongozi wale wasiofuata kanuni za kuheshimu haki za binadamu.

Wao utasikia wakisema "China iliendelea kwa kutoendekeza haki za binadamu" ama "watu kama nyie mngekuwa Korea kaskazini mngeshatwangwa risasi".

Kwa nini CCM huwa wanasisimuliwa sana na mambo yanayosadifu ugandamizaji?
 
Wanadhani wao wako salama. Wanadhani wanakula matunda ya uhuru.
 
Wanadhani wao wako salama. Wanadhani wanakula matunda ya uhuru.
Hii nayo ni hoja ya msingi sana. Yule jamaa aliyekuwa akisema "Apigwe Lissu apigwe!" wenzake wanaitikia "Apigwee" alishabikiwa sana na wana CCM wenzake!!
 
Hulka za baadhi ya wanadamu ni za kustaajabisha kweli wakati mwingine,viongozi wakatili sana kama Adolf Hitler,Iddi Amini,Mobutu,Kim Jong,Maduro,Bashir n.k walikuwa na wana watu na ambao wanawahusudu,wanawatetea na kuwaamini.Mpaka leo hii kuna watu wenye itikadi za unazi barani Ulaya.Wakati mwingine ni suala la kisaikolojia, mazingira au kukatishwa tamaa na kukosa uvumulivu na aina ya siasa zinazokuwepo kwa kipindi fulani.

Loyalty To country Alyways,To government When it deserves
 
Wote wanamuiga mwenyekiti wao, wanajua fika kwa sasa ccm hiana uungwaji mkono wa kisiasa kama zamani, hivyo matumizi ya mabavu tu ndio salama yao kwa kadiri watakavyoweza. Wanajua pindi ccm ikitoka madarakani wengi wao wataishia kubaya, hivyo yoyote anayetishia nafasi yao ya kuwa madarakani ni lazima akutane na dhahama ikiwemo kifo.
 
Hata siku ikatokea chama kingine mfano chadema kikashika dola, lazima viashiria kama hivyo vitatokea tu kwa wapinzani wake. Zaidi labda vitatofautiana tu viwango. Kwa sasa tunaiongelea ccm tu kwa sababu yenyewe ni lichama dola na hatujui ni lini litakuja kuondoka kwenye huu umiliki wa siasa za nchi yetu.
 
Kujiamini katika kutumia violence nguvu hili kutetea hoja sera nk ni jambo la kuepukana nalo maana hao wasioamini katika kutumia nguvu ni wanyonge wasio na nguvu wakimulilia Mungu wao atawaitikia
 
Kuanzia 2010 kadri upinzani ulivyoimarika viongozi wa ccm wamejawa hofu ya kupoteza madaraka. Kadri hofu Yao inavyoongezeka ndivyo wanavyopoteza uvumilivu, ustaarabu na utu. Viongozi wengi wa ccm huamini hakuna maisha nje ya madaraka na wako tayari kufanya lolote wasipoteze madaraka.
 
Jee ni sawa kwa chama kilichoko madarakani kunyanyasa wapinzani wake kisiasa.

Siyo sawa kabisa ila kwa bahati mbaya ndiyo hulka ya wanadam wakiwemo wanasiasa. Kiongozi pekee ambaye aliweza kuwasamehe watesi wake hata pale alipochukua mamlaka ya nchi, nadhani ni Mzee Mandela tu wa Afrika Kusini. Kama wapo wengine basi ni wachache sana.

Ila walio wengi mfano Senegal na Ivory Coast viashiria vya kisasi vimeonekana baada tu ya wapinzani kuchukua madaraka ya nchi kupitia sanduku la kura.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom