Kwanini CCM ndio wanalia CHADEMA wapeleke Wabunge wa Viti Maalum na si CHADEMA wenyewe?

S V Surovikin

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
13,590
32,672
Habari

Kila mmoja wetu ni shahidi kwamba tangu alipoingia madarakani bwana John Joseph pombe magufuli kauli zake na vitendo vyake ilikuwa ni kuua upinzani hasa CHADEMA.

Tumekuja mpaka 2020 kwenye uchaguzi mkuu tukashuhudia ambayo kila mmoja wetu anajua pamoja na kauli tata kwamba wapinzani ndio wanachelewesha maendeleo ya watanzania.

Hatimaye Uchaguzi ukaisha na CCM wakaibuka kidedea kwa mbinu wanazojua wao. Ndugu zetu upande wa pili/CHADEMA wakaamua kujiweka pembeni ili serikali ya CCM iweze kuharakisha maendeleo kwa wananchi, ila cha ajabu kuna kilio kikubwa kutoka CCM kuhusiana na jambo hili.

Yani viongozi wetu pamoja na sisi wafuasi wa chadema tumejiweka pembeni kuhusiana na jambo hili ila ccm wanahangaika sana kulikoni?

Naombeni mnisaidie nipate kuelewa nini kiko nyuma ya kilio hiki cha CCM wakati mahubiri yao siku zote ni kwamba wapinzani hawafai, wapinzani wanachelewesha maendeleo ya wananchi, wapinzani wanashirikiana na mabeberu, upinzani umekufa na maneno mengi ya namna hiyo.

Hata hapa jamiiforums tunaona vijana wa CCM wakijitahidi kuanzisha mada za kuwaomba viongozi wetu wakubali kupeleka wabunge wa viti maalum, wamefika mbali hadi kuleta nukuu za makada wa CCM wakitaka CHADEMA wakubali kupeleka wabunge wa viti maalum.

Je, kuna nini nyuma ya pazia?
 
Nimesoma kutoka twitter kwenye akaunti ya kamandana mmoja akiandika kuwa Job anawapigia simu baadhi ya wanawake wa CHADEMA waliowahi kuwa wabunge akiwataka wakubali nafasi za viti maalamu
Sasa tatizo nini chadema wamegeuka lulu kwao wakati mahubiri yao na vitendo vyao kwa wananchi ni kwamba wapinzani hawafai?
 
Kwan cdm hawatapeleka wawakilishi?
Maana sijasikia tamko lolote rasmi la chama!!
 
Kuna kama 2 trillions huwa zinaletwa kwa condition moja ya Bunge kuwa na wasimamizi wa LAC na PAAC....kwa idadi iliyopo akidi haijatimia kuwa na hizo kamati mbili zinazoundwa na wabunge wa upinzani....
Hapa ndio naanza kuelewa kwanini ccm wameanza kutongoza viongozi wa chadema
 
Kuna kama 2 trillions huwa zinaletwa kwa condition moja ya Bunge kuwa na wasimamizi wa LAC na PAAC....kwa idadi iliyopo akidi haijatimia kuwa na hizo kamati mbili zinazoundwa na wabunge wa upinzani....
Halafu inasemekana hata wahisani huwa wanakubali kuchangia bajeti kuu ya serikali baada ya kupata maoni ya kambi ya upinzani.
Kwa staili hii hiyo kambi ya upinzani wataipatajeee
 
Kwan cdm hawatapeleka wawakilishi?
Maana sijasikia tamko lolote rasmi la chama!!
 
Back
Top Bottom