Kwanini CCM inapoteza wapiga kura na Chadema inaokoteza waliopo..

Zekidon

JF-Expert Member
May 29, 2013
1,903
566
1.Mfumo wa upendeleo na takrima iliyopitiliza katika michakato ya uchaguzi wa wagombea, inasababisha wagombea wenye sifa halisi na zinazokubalika kutopata nafasi ya kunadi sera zao kama wagombea wa CCM.

2. Wanaochaguliwa kutokana na utaratibu huo hapo juu, kutopata support ya wote kutokana na kuwepo kw akundi lililojeruhiwa bila haki na kundi lenye mabavu, hivyo lile lenye mgombea hafifu kusababisha CCM ishindwe. mfano halisi, kilichotokea Arumeru Mashariki. Wnanachi waliipa kura chadema SI kwamba chadema ina mgombea anekubalika bali kutokana na hasira za kulazimishwa kupewa mgombea ambae hawamtaki. Ukweli ni kwamba KAMA CCM ikisimamisha mgombea anayekubalika katika mchakato huru, si ajabu kusikia 2015 Nassari hatarudi Bungeni. Hili limetokea pia kwa Iringa mjini, (mwakalebela).

3. Ushindi wa Chadema si kutokana na ubora wa chama chenyewe, Bali ni matokea ya HASIRA za wananchi juu ya injistice inayoendelea katika michakato ya uteuzi wa wagombea.

4. CCM ikiacha utaratibu huu wa kuteua wagombea kutokana na utajiri walio nao, au influence za majina yao ya mwisho, au mtandao walionao, basi itashinda katika Chaguzi nyingi.

5. Chadema bado kama chama cha upinzani, haina wagombea ambao wanasifa na rekodi za kipekee kuliongoza taifa.

6. Utaratibu wa Hasira unaotokana na wananchi kukiadhibu chama cha mapinduzi ukipungua na watu kuanza kuangalia ubora wa wagombea na si chama wanachotoka , basi Chadema itakosa kura nyingi na vyama vingine pia.

7. Umefika wakati kwa wananchi kupewa elimu ya uraia na upigaji kura ili kuwa na uwezo wa kuchanganua pumba na mchele (zilizopo nyingi ni pumba tu).

Mustakabali wa Taifa letu unatokana na aina ya viongozi tunao wachagua hivyo RAI yangu ni kama ifuatavyo:

Kiini cha Rai hii kinatokana na kauli aliyowahi kunipa rafiki yangu wakati natafuta dojo muafaka la kujifunzia michezo ya kujilinda " karate" Mjue kwanza mwalimu wako kwanza kabla ya kujiunga na dojo lake..fanya uchunguzi mdogo kuhusiana na historia yake, anaishi vipi na jamii, tabia zake, je ni mbabe, mlevi, mzinzii, aina ya mchezo anaofundisha na nini malengo yako kutokana na mchezo huo.

Hivyo basi, ni vyema kabla ya kupiga kura, au kushabikia, au kua mwanachama wa chama chochote kile , ni vbora kuzingatia haya:

1. Malengo ya chama/kiongozi.
2. Historia ya kiongozi.
3. Elimu.
4. rekodi ya utumishi wake, Je amefanya nini kinachooonekana kwa taifa hili, iwe katika ngazi ya familia, kata mkoa. kimataifa.
5. Je ana quality za uongozi.
6. Ana Familia ( sio vyema kuwa na viongozi ambao hawana familia, tukumbuke kua nguzo ya Taifa lolote lile ni familia, kua na kiongozi bora katika familia ni kua na kiongozi bora katika ngazi ya kitaifa, Haya yanahusiana).

Zingatia haya katika maamuzi yako.

CCM kwa nafasi yake Ikitakakuendelea kushinka dola ya nchi, ni kuwa na mfumo huru na wazi wa kugombea nafasi za uongozi, rushwa, majina ya mwisho, namitandao iwekwe pemmbeni, Kuna watu wenye ubora uliotukuka lakini hawana nafasi CCM.

Chadema, iwe na viongozi wenye sifa, na si mradi wagombea tu wanaopiga kelele nakusema pipooz power, mtachokwa na kusahaulika.

Tunahitaji serikali bora, na upinzani bora, si Bora upinzani, tu upinzani hafifu wenye kupinga kila kitu....

Taifa hili ni letu sote, na rasilimali zake ni zetu wote.

Amani na upendo.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Hayo unayoita makosa ya CCM ndio dalili za vyama vinavyo kufa. KANU ya Kenya ilikuwa hivyo hivyo, hadi ikang'olewa madarakani.
Vumilia tu, hata Kama unaipenda sana CCM Mungu anaipenda zaidi, mapenzi yake lazima yatatimia
 
Back
Top Bottom