Kwanini CCM inaogopa ushindani ulio huru?

lendila

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
5,806
4,370
Kwanini CCM inaogopa ushindani ulio huru na haki?

Kuna haja ya CCM kuacha kuogopa uchanguzi ulio huru na haki,hiki chama kupitia polepole wametuambia kuwa ni CCM mpya inayojali wanyonge,kuanzia machinga,wakulika,wafanyakazi na kadhalika kwa maaana hiyo uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ccm itashinda kwa kishindo sio?

Kama ndivyo kwanini ccm chama changu kisiridhie tume huru ya uchaguzi?

Viongozi wengi wa vyama vya upinzani wameunga mkono juhudi za mh rais,nafikiri sisi ccm tukikubali tume huru tutashinda tu kwa kishindo,sioni sababu za uoga kabisa
 
Kwanini ccm inaogopa ushindani ulio huru na haki?
Kuna haja ya ccm kuacha kuogopa uchanguzi ulio huru na haki,hiki chama kupitia polepole wametuambia kuwa ni ccm mpya inayojali wanyonge,kuanzia machinga,wakulika,wafanyakazi na kadhalika kwa maaana hiyo uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ccm itashinda kwa kishindo sio?kama ndivyo kwanini ccm chama changu kisiridhie tume huru ya uchaguzi?

1. Kushindwa ni aibu
2. Watakaokuja watafumua madhambi yaliyofanywa.
3. CCM watauana wenyewe kwa wenyewe.
 
umeanza kuandika mada yako kama mpinzani lakini ukamalizia kama mwana CCM, ninyi ndio mwenyekiti anawatafuta kila leo kwa sababu usiku mpo upinzani na mchana ni CCM.

Anyway , CCM ina sababu ya kupinga rufaa kwa sababu CCM ndio yenye serikali hivyo imefanya tathmini ya tume kuwa na watumishi wenyewe kitendo ambacho kitaongeza gharama kubwa ya uendeshaji wa tume.

Pia kukata rufaa si kupinga ila ni kuhitaji hukumu ya haki zaidi na ndiyo maana halisi ya kuwepo kwa mahakama kutoka ngazi ya mahakama ya mwanzo mpaka rufani.
 
Kwanini ccm inaogopa ushindani ulio huru na haki?
Kuna haja ya ccm kuacha kuogopa uchanguzi ulio huru na haki,hiki chama kupitia polepole wametuambia kuwa ni ccm mpya inayojali wanyonge,kuanzia machinga,wakulika,wafanyakazi na kadhalika kwa maaana hiyo uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ccm itashinda kwa kishindo sio?kama ndivyo kwanini ccm chama changu kisiridhie tume huru ya uchaguzi?
Viongozi wengi wa vyama vya upinzani wameunga mkono juhudi za mh rais,nafikiri sisi ccm tukikubali tume huru tutashinda tu kwa kishindo,sioni sababu za uoga kabisa
mkuu misemo iliwekwa/tungwa ili watu tujifunze, "mzoea vya kunyongwa vya kuchinja hawezi" mtu kama anaamini anapendwa na anafanya vizuri hofu yake nini?? watuache wTz tufanye maamz yetu.
 
umeanza kuandika mada yako kama mpinzani lakini ukamalizia kama mwana CCM, ninyi ndio mwenyekiti anawatafuta kila leo kwa sababu usiku mpo upinzani na mchana ni CCM.

Anyway , CCM ina sababu ya kupinga rufaa kwa sababu CCM ndio yenye serikali hivyo imefanya tathmini ya tume kuwa na watumishi wenyewe kitendo ambacho kitaongeza gharama kubwa ya uendeshaji wa tume.

Pia kukata rufaa si kupinga ila ni kuhitaji hukumu ya haki zaidi na ndiyo maana halisi ya kuwepo kwa mahakama kutoka ngazi ya mahakama ya mwanzo mpaka rufani.
Yani haya ni maelezo ya kujitetea?ptuu!
 
Kwanini CCM inaogopa ushindani ulio huru na haki?

Kuna haja ya CCM kuacha kuogopa uchanguzi ulio huru na haki,hiki chama kupitia polepole wametuambia kuwa ni CCM mpya inayojali wanyonge,kuanzia machinga,wakulika,wafanyakazi na kadhalika kwa maaana hiyo uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ccm itashinda kwa kishindo sio?

Kama ndivyo kwanini ccm chama changu kisiridhie tume huru ya uchaguzi?

Viongozi wengi wa vyama vya upinzani wameunga mkono juhudi za mh rais,nafikiri sisi ccm tukikubali tume huru tutashinda tu kwa kishindo,sioni sababu za uoga kabisa
Kwa sababu hawana uwezo wa kupambana kwa hoja hata na panya kwa hiyo kama chama tawala, wamejijengea uzoefu wa kubebwa na vyombo vya kibabe vya dola. Sababu nyingine in kuwa viongozi wa chama na Serikali yao wana madhambi mengi dhidi ya wananchi wanaogopa wataishia lupango Serikali ya chama kingine ikiingia madarakani.
 
umeanza kuandika mada yako kama mpinzani lakini ukamalizia kama mwana CCM, ninyi ndio mwenyekiti anawatafuta kila leo kwa sababu usiku mpo upinzani na mchana ni CCM.

Anyway , CCM ina sababu ya kupinga rufaa kwa sababu CCM ndio yenye serikali hivyo imefanya tathmini ya tume kuwa na watumishi wenyewe kitendo ambacho kitaongeza gharama kubwa ya uendeshaji wa tume.

Pia kukata rufaa si kupinga ila ni kuhitaji hukumu ya haki zaidi na ndiyo maana halisi ya kuwepo kwa mahakama kutoka ngazi ya mahakama ya mwanzo mpaka rufani.
"Inapobidi haki kutendeka lazima itendeke hata kwa gharama ya mbingu kushuka" - David Maraga - Chief justice Kenya.

Hivi mabilioni yaliyotumika kurudia chaguzi ndogo zisizokuwa na kichwa wala miguu, na kutekeleza hukumu ya mahakama kwa ajili ya kulinda katiba ambayo Rais ameapa kuilinda kipi bora?
 
Wakati wapinzani wanahama baada ya kununuliwa na ccm kwenye project iliyopachikwa jina la kuunga juhudi za rais, malalamiko ya gharama za kurudia uchaguzi ccm walikuwa wanatoa kejeli kwamba demokrasia ni gharama. Je kwasasa gharama zimeanza kuwa kitisho kwa ccm kwenye hiyo demokrasia?
 
Unaangaika kumjibu tu mwenzako keshalamba buku7000 anasubiri ya leo.
 
Kwanini CCM inaogopa ushindani ulio huru na haki?

Kuna haja ya CCM kuacha kuogopa uchanguzi ulio huru na haki,hiki chama kupitia polepole wametuambia kuwa ni CCM mpya inayojali wanyonge,kuanzia machinga,wakulika,wafanyakazi na kadhalika kwa maaana hiyo uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ccm itashinda kwa kishindo sio?

Kama ndivyo kwanini ccm chama changu kisiridhie tume huru ya uchaguzi?

Viongozi wengi wa vyama vya upinzani wameunga mkono juhudi za mh rais,nafikiri sisi ccm tukikubali tume huru tutashinda tu kwa kishindo,sioni sababu za uoga kabisa
wanaogopa njaaa
 
Asante sana mwanaccm mwenzangu kwa kuliona hili Chama kiache mbeleko ili kijipime kwani sio cha kwanza kushindwa hapa Afrika.
Viongozi wangu Bashiri na Polepole waliangalie hili ili kujua uhai wa chama
Kwanini CCM inaogopa ushindani ulio huru na haki?

Kuna haja ya CCM kuacha kuogopa uchanguzi ulio huru na haki,hiki chama kupitia polepole wametuambia kuwa ni CCM mpya inayojali wanyonge,kuanzia machinga,wakulika,wafanyakazi na kadhalika kwa maaana hiyo uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ccm itashinda kwa kishindo sio?

Kama ndivyo kwanini ccm chama changu kisiridhie tume huru ya uchaguzi?

Viongozi wengi wa vyama vya upinzani wameunga mkono juhudi za mh rais,nafikiri sisi ccm tukikubali tume huru tutashinda tu kwa kishindo,sioni sababu za uoga kabisa
 
umeanza kuandika mada yako kama mpinzani lakini ukamalizia kama mwana CCM, ninyi ndio mwenyekiti anawatafuta kila leo kwa sababu usiku mpo upinzani na mchana ni CCM.

Anyway , CCM ina sababu ya kupinga rufaa kwa sababu CCM ndio yenye serikali hivyo imefanya tathmini ya tume kuwa na watumishi wenyewe kitendo ambacho kitaongeza gharama kubwa ya uendeshaji wa tume.

Pia kukata rufaa si kupinga ila ni kuhitaji hukumu ya haki zaidi na ndiyo maana halisi ya kuwepo kwa mahakama kutoka ngazi ya mahakama ya mwanzo mpaka rufani.
CCM inaogopa gharama? Ccm ipi unayoongelea wewe ? Hii ya manunuzi?
 
umeanza kuandika mada yako kama mpinzani lakini ukamalizia kama mwana CCM, ninyi ndio mwenyekiti anawatafuta kila leo kwa sababu usiku mpo upinzani na mchana ni CCM.

Anyway , CCM ina sababu ya kupinga rufaa kwa sababu CCM ndio yenye serikali hivyo imefanya tathmini ya tume kuwa na watumishi wenyewe kitendo ambacho kitaongeza gharama kubwa ya uendeshaji wa tume.

Pia kukata rufaa si kupinga ila ni kuhitaji hukumu ya haki zaidi na ndiyo maana halisi ya kuwepo kwa mahakama kutoka ngazi ya mahakama ya mwanzo mpaka rufani.

Garama kwani serikali inatumia pesa ngapi kwenye kodi zetu? Kurudia majimbo ya uchaguzi? Ishu ya garama ni chaka la kujifichia kwani hao wakurugenzi hawalipwi maposho kedekede?
 
"Inapobidi haki kutendeka lazima itendeke hata kwa gharama ya mbingu kushuka" - David Maraga - Chief justice Kenya.

Hivi mabilioni yaliyotumika kurudia chaguzi ndogo zisizokuwa na kichwa wala miguu, na kutekeleza hukumu ya mahakama kwa ajili ya kulinda katiba ambayo Rais ameapa kuilinda kipi bora?
Gharama za udikteta na kuvunja sheria ni kubwa sana duniani kote.

Itafikia mahali inabidi mtawala dikteta mpe cheo kila anayemsaidia kutimiza ubabe wake.

Itabidi ndani ya vyombo vya kushurutisha atoe vyeo vingi vya juu ambavyo gharama za kuwahandle ni kubwa sana.
Ndani ya Vyombo vya kuihami nchi wakubwa wahonge vyeo vikubwa vingi ili wafanye kazi ya kudaidia ubabe.

Kwenye vyombo vya maamuzi ya sheria inabidi mahakimu wengi wahongwe vyeo vya ujaji ili wasimame upande wa ubabe ,jambo ambalo litaongeza gharama kubwa za kuwahandle majaji.

Itadi mabalozi wateuliwe kila kukicha ili kupata watakaoendana na ubabe na kuutangaza nje hasa kwenye nchi zenye Demokrasia ,jambo linaloongeza gharama kubwa.

Uivu wa Wakurugenzi wa kuvuruga Demokrasia unawafanya wahamishwe usiku kwa usiku kwa hofu ya kuvuna wanayoyapanda baada ya kupindisha kura,gharama zinazidi kwa serikali.

Kuna wakati Mkurugenzi na mkuu wa wilaya walikua wapo huru bila hofu kutokana na kujitahidi kutenda haki lakini siku hizi wamejawa na hofu na kupita na misafara mikubwa na makundi ya vyombo vya maguvu nyuma yao. Hii ni gharama kubwa sana

Kifupi Demokrasia gharama yake ni ya wakati wa uchaguzi tu na baada ya hapo nchi inatulia na upendo unatawala.

Gharama za udikteta ni kubwa sana na endelevu muda wote na chuki inaongezeke kila kukicha.

Mtaji wa CCM na wabunge wake na time yake ya uchaguzi ni ujinga wa watanzania wengi kuamini kuwa CCM ni chama kitakatifu hakitakiwi kupata ushindani na kukipinga ni dhambi.
 
Ili kuwaondoa wapinzani wasisi wa kuwa Ccm haitendi haki katika uchaguzi ni vema sasa serkali ikakubaliana na hukumu ya mahakama ili kuiambia Dunia kwamba Ccm ni chama dume na watanzania wanaimani nacho ndio maana kinashinda. Na kamwe hakishindi kwa hila wala dhuruma

Back
Top Bottom