Kwanini CCM imesalia madarakani kwa muda mrefu?

zagarinojo

JF-Expert Member
Jul 26, 2020
2,622
2,836
Ndugu zangu wana JF and other masters of politics, nadhani hata nyie mtakuwa mnajiuliza hili suala kwa muda sasa.

CCM imesalia madarakani toka kuanzishwa kwake mpaka sasa. Ni zipi sababu haswa za kuifanya ikae madarakani muda wote?

Tumekuwa tukishuhudia siasa za nchi Kama Marekani ambayo Ina ukomavu mkubwa wa kisiasa. Madaraka yamekuwa yakibadilika Katika vyama vikuu viwili Democratic na Republic.

Je, kwa hapa Tanzania Sababu za CCM kukaa madarakani ni zipi?

Wenda sababu ikawa ni siasa na uongozi dhabiti wa Mwalimu Nyerere katika kujenga uaminifu mkubwa katika nyanja zote muhimu za uongozi?

Au pengine labda ni uadilifu wa viongozi wa Chama Tawala katika kugawana keki ya Taifa. Yani kuongoza kwa awamu na kuzingatia ukomo wa madaraka kikatiba bila kuvunja sheria.

Sababu pia yaweza kuwa ni urafiki wa Chama na katiba ya Nchi.Katiba yetu ya mwaka 1977 iliundwa wakati CCM ikiwa madarakani labda ufanisi uliotumika ulizingatia misingi ya Ukanushaji wa baadhi ya dhana zinazoifanya CCM kuwa madarakani kwa muda mrefu.?

Hata hivyo mfumo wa vyama vingi ulianza mwaka 1992 lakini mpaka sasa hakuna chama pinzani kilichowahi kushika dola...Je hii inaweza kuvifanya vyama hizo kukosa nguvu na dhana ya vyama vingi kukosa mashiko?
 
Ni kwa kuwafanya Watanzania masikini na wanyonge ndipo kumewafanya wasalie madarakani.

1806075_Screenshot_2018-07-30-18-49-18.jpg
 
Back
Top Bottom