Kwanini CCM imejaza wanajeshi kwenye uongozi wake? Nayo inatishia amani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini CCM imejaza wanajeshi kwenye uongozi wake? Nayo inatishia amani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bwegebwege, Sep 24, 2010.

 1. bwegebwege

  bwegebwege JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2010
  Joined: Jul 30, 2010
  Messages: 1,031
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Kuna mtu ametuma post yake hapa JF anadai ile “PEOPLE’S POWER” ya CHADEMA inatishia amani...Mimi namuuliza, kwa nini asijiulize mbona CCM imejaza WANAJESHI kwenye safu yake ya juu ya uongozi? Siyo kwamba wamekuwa wakitumia hao kama STRATEGISTS wakuu wa kutumia MABAVU NA NGUVU ZA DOLA kuwakandamiza wapinzani??

  Wapo wengi hadi kwenye ngazi za mikoa na wilaya ambako unyanyasaji ndiyo unafanyika…Chukua mifano hii michache, mingine malizia…..

  1. JAKAYA KIKWETE
  2. YUSUPH MAKAMBA
  3. ABDULRAHMAN KINANA
  4. GEORGE MKUCHIKA
  5. JOHN CHILIGATI
  6. ......uliza mikoani na wilayani wamejaaa
   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Tunatawaliwa kijeshi
   
 3. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wa kwenu ni "wanajeshi feki" wa kupenda kuvaa "magwanda"! Teh teh teh.
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Huoni hata maamuzi yao ni ya kijeshijeshi tu!
   
 5. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  amri, shurutisha
  toa hongo ya uongozi kwa wanajeshi. watakulinda hata kwa nguvu endapo umma utakukataa kwenye kura
   
 6. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #6
  Sep 25, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Unajua kuna ujanja mmoja ulifanyika baada ya wanajeshi wasomi kutaka kumuondoa Nyerere madarakani. Nyerere alijitahidi sana ku consolidate madaraka na kuyaweka yote Ikulu. Alianzisha kitu kimoja kilikuwa kinaitwa mkoa wa majeshi lengo lilikuwa ni kulibananga jeshi. Then akawaingiza watu fulani jeshini na kuwachagua watu fulani jeshini na kuwatrain pale kivukoni na kuwa makada wa chama ndani ya jeshi.

  Wengi kati ya hawa mnaowataja kuwa ni wanajeshi ambao wanaserve serikalini, are not professional soldiers, if they were kungekuwa na discpline ya hali ya juu. Hakuna discipline kwa kuwa si wanajeshi halisi bali ni makada wa chama waliokuwa jeshini ambao somehow for political reasons walikwea ranks.

  Hii ni sababu jeshi letu halina uwezo wa kutetea maslahi ya nchi, na ndio maana wakati mwingine hata lenyewe linatumika kuibia watanzania.

  Professor Baregu amewahi kuja na theory moja ya jeshi na chama kutawala hand in hand hapa Tanzania, watu walimwona chinzi lakini ukiangalia idadi ya wakuu wa mikoa, wilaya na hata watu wengine wanaoteluliwa na rais unaweza kukuta kuna wanajeshi wengi tu. Hii ndio njia ambayo chama kimetumia kuliteka jeshi, same applies to usalama wa taifa.
   
 7. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #7
  Sep 25, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanajeshi ORIJINO. Wale feki wengine wana vitambi mpaka kufuani na hayo magwanda wanaonekana kama Kawawa.
   
 8. n

  ntakisigae JF-Expert Member

  #8
  Sep 6, 2014
  Joined: Nov 26, 2013
  Messages: 255
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kweli kabisa mkuu.That's genius analysis!
   
 9. masai dada

  masai dada JF-Expert Member

  #9
  Sep 6, 2014
  Joined: Dec 29, 2013
  Messages: 13,212
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  hahahah mkuu
   
 10. S

  SHAIDI JF-Expert Member

  #10
  Sep 23, 2014
  Joined: Aug 23, 2014
  Messages: 241
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 45
  niacheni nijipendekeze kwao wakinipindua ndiyo maana hata mishahara nawapendelea tofaut na washika chaki
   
 11. Brightman Jr

  Brightman Jr JF-Expert Member

  #11
  Oct 21, 2014
  Joined: Mar 22, 2009
  Messages: 1,233
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Jeshi halina Chama wala halijihusishi na chama chochote. Hao wanaoteuliwa toka ndani ya jeshi nao ni bahati yao, tusiwaonee wivu...!
   
 12. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #12
  Jun 18, 2015
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na M aendeleo CHADEMA Dr,P.W.SLAA amesikika mara kadha akilalamika kwamba Tanzania hakuna Usalama wa taifa nali kuna usalama wa ccm siyo hilo tu bali pia amenukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari akililaumu jishi la Polisi Tanzania kwamba nalo pia ni polisi wa chama cha mapinduzi ccm.

  Mwanzoni wengi tulikataa hatiku kubaliana na kauli hizi na tukawa mstari wa mbele kuziita ni kauli za kipuuzi na kizushi mimi na wenzangu hatuku kubaliana na kauli kwamba usalama wa taifa (TISS) wanaweza kuwa usalama wa ccm na Polisi wakawa ccm na tulifanya hivyo tukijua kwamba vyombo vya dola haviwezi kupendelea upande mmoja katika nchi ya kidemokrasia.

  Pamoja na imani yetu hiyoya kuamini wana usalama na walinzi wa maisha ya wananchi na mali zao matukio ya hivi karibuni yamenionyesha wazi kuwa usalama wa Taifa waweza kuwa usalama wa chama cha mapinduzi ccm na malizao na kuacha usalama wa raia na mali zao,ili kuthibitisha haya inabidi tutajane majina hapaili kudhihirisha tunayosema kwamba CCM ni POLISI na TISS NA PIA TISS na POLISI ni CCM.

  1. IGP Omari Mahita:
  Baada ya kuwasingizia CUF kwamba wameingiza majambia ili kuvuruga uchaguzi alipo staafualienda kugombea ubunge huko Morogoro kupitia CCM Japoalishindwa.

  2. Brigadia Dk.Guido Gorogolio Singanda:
  Alipo staafu uofisa usalama jeshini aligombea ubunge kupitia CCM huko mkoani Mbea.

  3. Jenerali Robert Mboma:
  Aliekuwa Mkuu wa Majeshi Mstaafu aligombea Ubunge kupitia CCM japo hakushinda.

  4. Alfred Tibaigana:
  Aliekuwa kamandwa wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kustaafu nae alirudi kwao muleba mkoani Kagera kugombea Ubunge kupitia CCM na hii ikiwa ni mwaka mmoja tu baada ya kustaafu.

  5. J.K Kikwete:
  Huyu ukisoma CV yake nae ni mwana Usalama aliyewahi kuhudumu Makao Makuu CCM kabla ya kupandishwa vyeo na kuwa waziri kwa nafasi tufauti hadi kugombea na kuwa raisi.

  Hadi sasa kuna wana Usalama wa tano na Majaji wastaafu wametia nia ya kugombea Uraisi kupitia Chama Cha CCM nao si vibaya kuwataja kwa majina.

  6. Mizengo Kayanza Peter Pinda:
  Mtaalam wa kupiga watu na Waziri Mkuu wa sasa anafahamika kuwa ni shushushu aliyewahi kuhudumu pale Ikulu kwa muda mrefu .

  Mathias Chikawe;
  UWaziri wa mambo ya ndani huyu ni shushushu aliekubuhu nae ametia nia ya kugombea Uraisi kupitia CCM.

  Balozi Agustino Philip Mahinga:
  Aliwahi kuwa balozi wa kudumu wa Tanzania pale Umoja wa Mataifaanasemekana pia aliwahi kushika wadhifa wa Unaibu Mkurugenzi Usalama wa Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje nae ametangaza nia ya kugombea Uraisi kupitia CCM

  7. Bernard Camillius Membe:
  Huyu nae ni shushushu wa kupindukiapia ​metia nia ya kugombea uraisi kupitia CCM.

  8. Hinnes Kitine:
  Ambae alishawahi kushika wadhifa wa Mkurugenzi wa Usalama wa Taita enzi ya Utawala wa Mwalimu Nyerere akihudumu katika Ikulu ya Magogoni kwamba nae pia ametia nia ya kugombea Uraisi kupitia CCM.

  Hoja ni moja msururu wa wana usalama wanaotia nia sasa kupitia ccm na hata hao waliowahi kugombea kupitia ccm inaonyesha ishara gani kama siyo udhibitishokwamba Usalama wa Taifa ni usalama wa ccm kama anavyodai Dr.W.P.Slaa wa CHADEMA?

  Msululu wa Maofisa wa Polisi na Majenerali wa Jeshi la Wananchi (JW) wanaogombea kwa tiketi ya CCM ni udhibitisho wa kitu gani kama siyo kweli kwamba vyombo vya dola ni vyombo vya CCM?

  Matukio ya kupigwa na kuteswa kwa watetezi wa wananchi,Kuibiwa kwa kura wakati wa uchaguzi mkuu na kashfa za ufisadi miezi kadhaa kabla ya uchaguzi mkuu na ikadaiwa pesa hizo zimetumiwa na CCM kwenye uchaguzi na matukio hayo hayajawahi kuchunguzwa wala kupatiwa ufumbuzi na hao wanaokuja kugombea baadae kupitia CCM sisi raia wa kawaida tusemeje?

  Hayo yote tisa kumi ni yale yaliyomkuta Jemedari wa vita vya Kagera, Meja Jenerali Kambale (Mwita Marwa) almaarufu Mwita Wabhachira, alipogombea kupiyia CHADEMA Ubunge wa Tarime,mimi sisemi alikutwa na nini mitaambiwa ni mwongo waulize wanajeshi au ndugu zake utashangaa.
   
 13. Ghosryder

  Ghosryder JF-Expert Member

  #13
  Jun 18, 2015
  Joined: Jul 6, 2014
  Messages: 9,151
  Likes Received: 2,162
  Trophy Points: 280
  Umeandika meengi hata hayana cha maana kumbe ni hisia zako tu ! usituchanganye hapa tuko kwenye mambo ya msingi sana hapa.
   
 14. M

  Mtia nia JF-Expert Member

  #14
  Jun 18, 2015
  Joined: Jun 12, 2015
  Messages: 286
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Slaa gongo inamsumbua kichwani
   
 15. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #15
  Jun 18, 2015
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  hayo ya msingi na ya maana ni yapi?
   
 16. d

  desertfox Senior Member

  #16
  Jun 18, 2015
  Joined: Oct 4, 2014
  Messages: 162
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Mwenye taarifa ya jenerali marwa plz
   
 17. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #17
  Jun 18, 2015
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  kama ambavyo unafiki unakusumbua
   
 18. Ghosryder

  Ghosryder JF-Expert Member

  #18
  Jun 18, 2015
  Joined: Jul 6, 2014
  Messages: 9,151
  Likes Received: 2,162
  Trophy Points: 280
  We hujui kuwa hujui hutanielewa.
   
 19. Erythrocyte

  Erythrocyte JF-Expert Member

  #19
  Jun 18, 2015
  Joined: Nov 6, 2012
  Messages: 44,577
  Likes Received: 25,469
  Trophy Points: 280
  sikumbuki siku ambayo Dr slaa alikurupuka , list of shame ni ushahidi .
   
 20. DCONSCIOUS

  DCONSCIOUS JF-Expert Member

  #20
  Jun 18, 2015
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,272
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Bora yeye kichwani kuliko wewe inae kusumbua kwenye ule mtandao wa mwalubadu
   
Loading...