Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,991
Sasa kuna majibu ya haraka na ya pupa. Na yapo majibu yanayohitaji kutafakari kidogo. Kwa haraka mtu anaweza kusema kuwa CCM iko matatani kwa sababu CDM wanapandikiza mbegu ya chuki kwa wananchi. Mwingine (katika haraka yake) anaweza kuja na kusema CCM iko matatani kwa sababu wameshindwa kujivua "gamba". Mwingine naye katika kujaribu kuelezea kwanini CCM iko matatani anaweza kuja na kusema kwa sababu ndani yake kuna "migongano".
Naomba kupendekeza kwamba kuna jawabu la kina zaidi. Naamini vyote hivi tunavyoviona ni dalili tu ya tatizo (symptoms). Sasa kwa wale ambao mnaifahamu CCM labda tangu ikiwa TAA hadi leo hii mnaweza kutusaidia na kuwasaidia vijana wetu kuelewa kwanini CCM iko matatani leo hii? Kwanini inajitahidi kutumia nguvu sana kushinda uchaguzi wakati zamani ilikuwa rahisi sana. Kwanini kwa mfano mwaka 2005 ilifanya vizrui sana kuliko wakati mwingine wa vyama vingi na miaka mitano baadaye ikafanya vibaya kuliko wakati wowote wa historia yake?
Katika majibu yetu tujaribu kuleta yote bila kujali ukweli wake. Ieleweke siulizii majibu ya kisayansi; najaribu kufanya brain storming ambayo inaweza ikatuelewa kwanini hiki chama ambacho kiliwahi kuwa mashuhuri zaidi, kupendwa zaidi na hata kuhofiwa leo hii kinaonekana kigeni machoni pa watu?