Kwanini CCM Iko Matatani?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,460
39,928
Sasa kuna majibu ya haraka na ya pupa. Na yapo majibu yanayohitaji kutafakari kidogo. Kwa haraka mtu anaweza kusema kuwa CCM iko matatani kwa sababu CDM wanapandikiza mbegu ya chuki kwa wananchi. Mwingine (katika haraka yake) anaweza kuja na kusema CCM iko matatani kwa sababu wameshindwa kujivua "gamba". Mwingine naye katika kujaribu kuelezea kwanini CCM iko matatani anaweza kuja na kusema kwa sababu ndani yake kuna "migongano".

Naomba kupendekeza kwamba kuna jawabu la kina zaidi. Naamini vyote hivi tunavyoviona ni dalili tu ya tatizo (symptoms). Sasa kwa wale ambao mnaifahamu CCM labda tangu ikiwa TAA hadi leo hii mnaweza kutusaidia na kuwasaidia vijana wetu kuelewa kwanini CCM iko matatani leo hii? Kwanini inajitahidi kutumia nguvu sana kushinda uchaguzi wakati zamani ilikuwa rahisi sana. Kwanini kwa mfano mwaka 2005 ilifanya vizrui sana kuliko wakati mwingine wa vyama vingi na miaka mitano baadaye ikafanya vibaya kuliko wakati wowote wa historia yake?

Katika majibu yetu tujaribu kuleta yote bila kujali ukweli wake. Ieleweke siulizii majibu ya kisayansi; najaribu kufanya brain storming ambayo inaweza ikatuelewa kwanini hiki chama ambacho kiliwahi kuwa mashuhuri zaidi, kupendwa zaidi na hata kuhofiwa leo hii kinaonekana kigeni machoni pa watu?

ccm ya leo imepoteza asilia yake ya angalu kujali maslahi ya wengi sasa inakumbatia ya wachache. kuongezeka kwa uelewa wa wananchi ambapo (ignorance) ya wananchi umekuwa mtaji wa ccm kwa miaka kadhaa sasa nayo yachangia kuiweka matatani chama la kijani, ndiyo maana sasa wanadiriki hata kununua kura,kutumia polisi kutisha/kuminya demokrasia kujisababishia ushindi

Sasa kuna majibu ya haraka na ya pupa. Na yapo majibu yanayohitaji kutafakari kidogo. Kwa haraka mtu anaweza kusema kuwa CCM iko matatani kwa sababu CDM wanapandikiza mbegu ya chuki kwa wananchi. Mwingine (katika haraka yake) anaweza kuja na kusema CCM iko matatani kwa sababu wameshindwa kujivua "gamba". Mwingine naye katika kujaribu kuelezea kwanini CCM iko matatani anaweza kuja na kusema kwa sababu ndani yake kuna "migongano".

Naomba kupendekeza kwamba kuna jawabu la kina zaidi. Naamini vyote hivi tunavyoviona ni dalili tu ya tatizo (symptoms). Sasa kwa wale ambao mnaifahamu CCM labda tangu ikiwa TAA hadi leo hii mnaweza kutusaidia na kuwasaidia vijana wetu kuelewa kwanini CCM iko matatani leo hii? Kwanini inajitahidi kutumia nguvu sana kushinda uchaguzi wakati zamani ilikuwa rahisi sana. Kwanini kwa mfano mwaka 2005 ilifanya vizrui sana kuliko wakati mwingine wa vyama vingi na miaka mitano baadaye ikafanya vibaya kuliko wakati wowote wa historia yake?

Katika majibu yetu tujaribu kuleta yote bila kujali ukweli wake. Ieleweke siulizii majibu ya kisayansi; najaribu kufanya brain storming ambayo inaweza ikatuelewa kwanini hiki chama ambacho kiliwahi kuwa mashuhuri zaidi, kupendwa zaidi na hata kuhofiwa leo hii kinaonekana kigeni machoni pa watu?
Jibu langu ni kwamba, Wananchi wa Tanzania siyo walewale wa miaka ya 80 na viongozi wa CCM ni wale waliozoea kuendesha nchi kwa mazoea. Wakidhani wanaiongoza Tanzania ileile na wananchi walewale wanaoimbiwa kwamba Tanzania ni nchi ya amani na kushangiliwa bila kuhojiwa amani maana yake nini, na kikubwa zaidi uongozi wa sasa(awamu ya nne) ni mbovu zaidi kiasi kwamba inawafanya hawa watanzania wapya wa-notice haraka sana

Ni kwasababu hakuna maendeleo kwa wananchi,kuongezeka kwa tabaka la masikini walio wengi na wachache matajiri,ahadi ambazo hazitekelezwi,BORA JANA KULIKO LEO...

Kwa sababu imekuwa mabingwa maneno, wa kuwaahidi wananchi maendeleo, ilhali kivitendo ni kinyume chake

ccm IMEPOTEZA dira na mwelekeo, viongozi wanaangalia maslahi yao na familia zao. Watendaji wanateuliwa kwa kujuana na sio utaalamu matokeo yake ni mawazo rahisi kwa mambo magumu, no creativity, kila kitu wa cut na ku paste. Hakuna kauli moja ya viongozi(kila kiongozi ana kauli yake kwenye jambo moja) AHADI hazitekelezwi. (Bora ukae kimya ufanye kitu cha maana au usifanye kabisa kuliko uahidi usitekeleze).

Kutokusoma alama za nyakati na kwenda sawa na uelewa wa wananchi, kutokubali kukosolewa............

kwa sababu kilikuwa ni chama cha kutafuta uhuru bila kujua baada ya uhuru ni nini kitafuatia,viongozi ni walewale na sera zilezile wakati unabadilika.
walikuwa wamelenga kupata uhuru na baada ya uhuru ni kutawala(copy and paste)kutoka kwa wakoloni,sasa wananchi wamegundua kumbe uhuru bado aliondoka mkoloni mweupe kaja mkoloni mweusi tena anayefahamika mpaka babu yake aliko toka.
sasa wanataka chama cha kuwaongoza kuliko cha kuwatawala,rais wa kuongoza kuliko kutawala,serikali ya kuwajika kwa wananchi sio ya kuogopwa na wananchi,rais ambaye ni mwajiriwa namba moja na si mwajiri namba moja.
ccm wakiweza kulijua hili wataanza kurudi juu na mimi ni mmoja wapo wa watakao rudi ccm.

Jibu langu ni kwamba, Wananchi wa Tanzania siyo walewale wa miaka ya 80 na viongozi wa CCM ni wale waliozoea kuendesha nchi kwa mazoea. Wakidhani wanaiongoza Tanzania ileile na wananchi walewale wanaoimbiwa kwamba Tanzania ni nchi ya amani na kushangiliwa bila kuhojiwa amani maana yake nini, na kikubwa zaidi uongozi wa sasa(awamu ya nne) ni mbovu zaidi kiasi kwamba inawafanya hawa watanzania wapya wa-notice haraka sana
Haswaa! kwa hapo umelenga, Tunahitaji kuendelea kuwabadilisha wananchi wengi wajitambue na wadai haki zao! ili CCM waendelee kudhoofu na hatimae kufa kabisa.

Sasa kuna majibu ya haraka na ya pupa. Na yapo majibu yanayohitaji kutafakari kidogo. Kwa haraka mtu anaweza kusema kuwa CCM iko matatani kwa sababu CDM wanapandikiza mbegu ya chuki kwa wananchi. Mwingine (katika haraka yake) anaweza kuja na kusema CCM iko matatani kwa sababu wameshindwa kujivua "gamba". Mwingine naye katika kujaribu kuelezea kwanini CCM iko matatani anaweza kuja na kusema kwa sababu ndani yake kuna "migongano".

Naomba kupendekeza kwamba kuna jawabu la kina zaidi. Naamini vyote hivi tunavyoviona ni dalili tu ya tatizo (symptoms). Sasa kwa wale ambao mnaifahamu CCM labda tangu ikiwa TAA hadi leo hii mnaweza kutusaidia na kuwasaidia vijana wetu kuelewa kwanini CCM iko matatani leo hii? Kwanini inajitahidi kutumia nguvu sana kushinda uchaguzi wakati zamani ilikuwa rahisi sana. Kwanini kwa mfano mwaka 2005 ilifanya vizrui sana kuliko wakati mwingine wa vyama vingi na miaka mitano baadaye ikafanya vibaya kuliko wakati wowote wa historia yake?

Katika majibu yetu tujaribu kuleta yote bila kujali ukweli wake. Ieleweke siulizii majibu ya kisayansi; najaribu kufanya brain storming ambayo inaweza ikatuelewa kwanini hiki chama ambacho kiliwahi kuwa mashuhuri zaidi, kupendwa zaidi na hata kuhofiwa leo hii kinaonekana kigeni machoni pa watu?
Mchango wangu katika bangua bongo hii unaweza kuwatatiza wengi lakini nitasema ili nitimize wajibu wangu kwa JF na wananchi wa Tanzania. Asili ya CCM ni TANU ambayo pia ilirithi majukumu ya TAA ambacho hakikuwa chama cha siasa bali Asasi isiyokuwa ya kiserikali ambayo ilikuwa na makusudi ya kupigania haki na ustawi wa watu weusi na kuondoa ubaguzi na dhuluma za wakoloni dhidi ya wafanyakazi wa kiafrika. Makusudi yake ilikuwa kuwaunganisha waafrika ili wawe na sauti kubwa wakati wakilalamikia haki zao hasa wale wa mijini. TANU ilipokuja iliingiza harakati za ukombozi wa kisiasa na kumng'oa mkoloni. TANU ilijipambanua kama chama cha siasa ambacho kilikuwa na jukumu la kuwaunganisha Watanganyika kujitawala kwa kudai uhuru kutoka mikononi mwa wakoloni. Kilikuwa chama cha wanyonge kikiunganisha makundi makubwa ya kijamii kwa wakati ule ya wakulima na wafanyakazi. Hata hivyo katika kufikia malengo yake hakikufanya dhambi ya ukaburu kwa rangi bali kilijitenga na makundi ya kifisadi na yale ambayo yalikuwa na ubnafsi katika harakati za kujitafutia riziki. TANU haikuwahukumu lakini iliwatenga kisiasa hasa katika uongozi. Wafanyabiashara na wapinzani wa itikadi yake hawakupatiwa nafasi ya uongozi na waliwachuja mapema kwa wale waliodiriki kuomba.

CCM ilirithi mambo yote ya tanu na pengine iliyafafanua kitaalamu zaidi, hata hivyo muda ulivyozidi kupita CCM imekuwa ikionyesha uchovu wa kisiasa na kushindwa kuhimili ushindani wa hoja na hivyo kilichofanyika ilikuwa ni kufungulia kundi ambalo halikuasisi siasa za chama hicho kushika hatamu za uongozi (uliwahi kuona wapi fundi wa gari awe mtu ambaye hakusomea kutengeneza gari?). Wafanya biashara wakawa wafadhili wakubwa wa Chama, na kwa kupitia hii dhana ya ufadhili katika siasa wakapata nafasi adimu ya kuwa karibu na viongozi wa chama na serikali wakaanza kuwaonyesha viongozi wetu waliokuwa maskini wa mali lakini werevu utamu wa fedha. Walipozidi kunogewa wakawambia asali hii ya fedha ni tamu zaidi kama na nyinyi mtalibomoa azimio la Arusha na miiko ya uongozi nao bila uoga na kwa ujasiri usiozoeleka wakabomoa miiko hiyo ya uongozi.

Viongozi hawakujua kuwa kuwaingiza katika chama kundi ambalo halikuasisi siasa za chama walikuwa wakiwapigia kura ya kuondoka walalahoi wakitanzania ambao sasa walikosa mtetezi wa kisiasa na masilahi yao sasa yalikuwa hayana nafasi . Niliwahi kumsikia Rais Mkapa akisema katika moja ya hotuba yake ya mwisho wa mwezi akiwaambia watanzania waache wivu na badala yake wafanye bidii, sikujua kauli hii ya mkapa kama ilitoka kwa bahati mbaya au alitaka kujilinda na uhalifu wake wa kisiasa alipokuwa Ikulu. Watanzania hawakuwa wanalalamika kwa sababu za wivu walilalamika jinsi utaratibu wa uongozi ulivyokuwa umeanza kupinda na kuhatarisha maslahi ya wengi. Siasa za uchumi wa ubinafshaji si mbaya kama zitafanywa katika misingi ya uwazi na wenye kuzingatia masilahi ya umma na siasa za uchumi wa uwekezaji si hatari kama wawekezaji watawekewa misingi ya kuwajibika na kunufaisha watanzania. Wanachojivunia CCM leo kama mafanikio ni pale wanapohesabu idadi ya shughuli zilizofanya hasa katika miradi ya ubinafshaji na uwekezaji. Hawadiriki kabisa kujua uhalifu wa kiuchumi wanaofanya katika miradi hii kwa jamii ya watanzania, hawaulizio ajira je kwa mtanzania, kodi je? bei chee ya kuwauziia mashirika yetu na rasilimali asili zetu. Wanahesabu miradi ya uwekezaji katika madini na utalii hawadiriki kutwambia kile tunachonufaika nacho ni sehemu kidogo sana ya haki yetu ama hakuna kabisa.

Wametujengea shule, barabara, miradi ya maji, afya na mingineyo mingi lakini kwa gharama kubwa kiasi kuwa hakuna thamani ya hela tena na watanzania wa leo ni waelewa wanaona hapa wameibiwa. Wafanyabiashara/matajiri hawajui siasa, wengi hawana utu tulichoambulia kutoka kwao ni kuasisiwa kwa mfumo wa kura za kununua, kusitawi kwa rushwa katika siasa na mengine mengi machafu na viongozi kupakatwa na matajiri kiasi kuwa wakiingia madarakani wanajishughulisha na ulipaji fadhila ili waendelee kuwapo.

Sitegemei wa kufikiria CCM iliyoasi asili yake kwa kuasisiwa na kundi lisilo asili iache kuwa na mgogoro na makundi yake asilia. Bahati mbaya sasa CCM ilipofikia haiwezi tena kukidhi haja ya makundi hasimu yaani makundi asilia na yale yaliyoibuka karibuni. Wanataka kura kutoka makundi yake asilia ili wawe madarakani vilevile wanataka fedha kutoka katika kundi jipya ili wamudu siasa za ushindani. CCM hawawezi kujua mvutano huu ndio uliowapotezea mvuto, hawezi kujua kuwa mvutano huu ndio unaowaweka matatani, kwao viongozi wetu, yote sawa na walipojaribu kujitambua na kutaka kuchukua hatua ya kujinasua nadhani wote mumeona na katika siasa zetu Igunga imeingia katika rekodi ya siasa kigeugeu.

kustawi kisiasa ni kutafuta udhaifu wa adui yako vyama shindani kisiasa na CCM vimeona upenyo huo na sasa vinajaribu kutupia makonde mazito hapohapo ili pavimbe papasuke na damu itoke kwa wingi mpaka CCM iwe dhaifu waiondoe kiulani madarakani, hilo mnaliona ingawa si kwa sipidi mnayotaka lakini CCM wenyewe wanatambua kuwa mzigo walionao umeanza kuwaelemea, wameanza kukodi wabebaji ambao nao nahisi watachoka haraka kuliko wanavyotegemea umma ukiendeleza nguvu zake kwao. Ni swali dogo tu kwa vyombo vya dola ambao sasa ndio wabebaji wakuu wa mzigo wa CCM "wangepanda kuona watanzania wangapi wanakufa ili CCM iendelee kuwa madarakani"

Mwanakijiji na wewe nae ni sehemu ya kilo ambazo zinafanya mzigo wa CCM kuwa hauwezi kubebeka endelea kazi nzuri sana ambayo italipa muda mfupi ujao

Aluta condinua, Our lost glory and stolen freedom will be with us soon

Sasa kuna majibu ya haraka na ya pupa. Na yapo majibu yanayohitaji kutafakari kidogo. Kwa haraka mtu anaweza kusema kuwa CCM iko matatani kwa sababu CDM wanapandikiza mbegu ya chuki kwa wananchi. Mwingine (katika haraka yake) anaweza kuja na kusema CCM iko matatani kwa sababu wameshindwa kujivua "gamba". Mwingine naye katika kujaribu kuelezea kwanini CCM iko matatani anaweza kuja na kusema kwa sababu ndani yake kuna "migongano".

Naomba kupendekeza kwamba kuna jawabu la kina zaidi. Naamini vyote hivi tunavyoviona ni dalili tu ya tatizo (symptoms). Sasa kwa wale ambao mnaifahamu CCM labda tangu ikiwa TAA hadi leo hii mnaweza kutusaidia na kuwasaidia vijana wetu kuelewa kwanini CCM iko matatani leo hii? Kwanini inajitahidi kutumia nguvu sana kushinda uchaguzi wakati zamani ilikuwa rahisi sana. Kwanini kwa mfano mwaka 2005 ilifanya vizrui sana kuliko wakati mwingine wa vyama vingi na miaka mitano baadaye ikafanya vibaya kuliko wakati wowote wa historia yake?

Katika majibu yetu tujaribu kuleta yote bila kujali ukweli wake. Ieleweke siulizii majibu ya kisayansi; najaribu kufanya brain storming ambayo inaweza ikatuelewa kwanini hiki chama ambacho kiliwahi kuwa mashuhuri zaidi, kupendwa zaidi na hata kuhofiwa leo hii kinaonekana kigeni machoni pa watu?

Una haki ya kutoa maoni lakini siyo kubuni maoni. Hoja yako imeshakuja na majibu hata kabla hujauliza swali. Labda ungeanza kwa kueleza kwanini unaona CCM ipo matatani. Kwa mtazamo wangu naona chama kinchoongoza serikali ya Tanzania kinapita kwenye hali ya kawaida tu ambayo inaweza ikaikuta taasisi yoyote hasa yenye dhamana ya kuongoza kundi la watu, nchi nk. Inakuwa rahisi sana kukosoa makosa ya CCM kuliko ya Chadema kwasababu ndicho kilichopo madarakani. Inatokea kwa Democrats ya Obama seuze CCM?

Unaparamia lugha za watu ya kwenu inakushinda. Hiki Kiswahii gani?

CCM imepoteza misingi yake ya kuwatumikia wakulima na wafanyakazi, leo hawazitaki kura za wafanyakazi hadharani, na wakulima kila siku bei ya mazao yao inashuka huku gharama za maisha zikiongezeka.Kilichopo ni kuwaangukia mafisadi na wafanyabiashara wakubwa wa kuwapa mshiko. Hapo umaarufu lazima upotee

Una haki ya kutoa maoni lakini siyo kubuni maoni. Hoja yako imeshakuja na majibu hata kabla hujauliza swali. Labda ungeanza kwa kueleza kwanini unaona CCM ipo matatani. Kwa mtazamo wangu naona chama kinchoongoza serikali ya Tanzania kinapita kwenye hali ya kawaida tu ambayo inaweza ikaikuta taasisi yoyote hasa yenye dhamana ya kuongoza kundi la watu, nchi nk. Inakuwa rahisi sana kukosoa makosa ya CCM kuliko ya Chadema kwasababu ndicho kilichopo madarakani. Inatokea kwa Democrats ya Obama seuze CCM?

Huwa mnanichekesha sana pale mnapokimbilia kutoa mifano ya Uingereza, Marekani when u think it suits u. Tukija kwenye masula ya msingi kama elimu, maji, umeme, miundombinu ikitolewa tu mfano wa Marekani au UK huwa hamkawii kuruka " hapa sio Marekani bana" haha haha ahaha ahaha!!!!!.... Hoja yako inaonyesha pamoja na majukumu uliyopewa na CCM bado unaishi kwenye denial which will not help u and ur party altogether!!!!!

Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha.ccm waliokuwa wanaccm wameshazeeka na wengine wamekufa.kwa maana hiyo waliokufa wamekufa nayo na waliozeeka wamezeeka nao.ndo maana hata wale ambao wapo wanatumia siasa za mwaka 47.mia

13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom