Kwanini CAG Ludovick Utouh hana sifa za kuandaa taarifa ya ukaguzi maalum UDA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini CAG Ludovick Utouh hana sifa za kuandaa taarifa ya ukaguzi maalum UDA?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Patriote, Dec 30, 2011.

 1. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Katika toleo la mwananchi la jana nisiloma habari kuwa Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh amesema ripoti ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), ipo katika hatua za mwisho na ifikapo mwishoni mwa mwezi ujao, kila kitu kitawekwa wazi. Hakika sikuelewa kwamba Bw. Ludovick Utouh bado anaendelea kushikilia ofisi ya Umma hasa baada ya kuongea upupu katika issue ya Jairo na Bunge kuthibitisha kuwa CAG alitoa ushauri ambao ni substandard kwa lengo la kupotosha ukweli na kuhadaa umma wa watanzania na kulinda ukiukwaji wa sheria na taratibu za fedha alizoapa kuzilinda. Mtu wa aina hii kimsingi ameshapoteza sifa na imani kwa wananchi kwa kuuthibitishia umma kuwa ni mwongomwongo na anatetea wizi wa rasilimali zetu na hivyo hapaswi kuaminiwa. Inakuwaje tena watanzania sisi sisi tunasubiri kupokea taarifa ya UDA anayoiandaa mtu wa namna hii??? Rejea sehemu ya taarifa ya kamati teule ya bunge katika sakata la Jairo.

  "Katika sehemu ya ushauri na hitimisho la CAG, Taarifa ya Ukaguzi Maalum haikuzingatia yaliyojitokeza ndani ya Taarifa ili kutoa majibu kwa Hadidu za Rejea badala yake ushauri pekee unaonekana kuegemea katika idadi ya Taasisi kuwa 20 na kiwango cha fedha ilizochangwa kuwa Sh.1,000,000,000.00. Hatua hii imesababisha upotoshaji mkubwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi ambaye naye alitumia ushauri huu kama msingi wa Maamuzi yake katika Uchunguzi wa Awali alioufanya. Hata hivyo baada ya kukabidhiwa, Katibu Mkuu Kiongozi alipaswa kuitumia Taarifa ya Ukaguzi Maalum kwa ujumla wake badala ya kipengele cha ushauri ambacho ni upotoshaji" (Taarifa ya kamati, 2011)

  Hivi inamana tumeshasahau aliyoyafanya kwenye ripoti ya Jairo au ndo tutake tusitake lazma CAG awe ni huyu huyu??? Mimi nadhan kazi ya CAG inahitaji mtu muadilifu sana na mtu asiye na hulka ya uongo uongo na asili ya upotoshaji hata kidogo. Sasa kama CAG ndo anaongoza kwa uongo, upotoshaji na kuficha ukweli pamoja na kulinda wizi katika serikali yetu, anatarajia wasiadizi wake wafanye nini???Hivi kweli mtu wa hivi akiandaa report nyingine inaleta maana/mantiki yoyote kweli???Mbaya zaid report yenyewe inahusu tuhuma za ufisadi kama ila ya Jairo. Hakika sio bure "Tanzanians must be crazy"!!Hivi kuna ugumu gani kukataa mtu huyu asishike kitengo nyeti kama hicho hasa baada ya kuonekana hana uaminifu na anafumbia macho ukiukwaji mkubwa wa sheria za fedha badala ya kuzisimamia na kuzilinda kama alivyoapa????Kama hii ndiyo tabia yake, kwanini tuendelee kumuamini kiasi hiki hata kumwacha aendelee kufanya ukaguzi maalum sehemu nyingine??Ni nini kilimsukuma kulinda waharifu na kufumbia macho ukiukwaju mkubwa wa sheria na taratibu za fedha kwa Jairo??Je tuna uhakika gani kama hatorudia tena UDA?? Kimsingi alitutia hasara kwa makusudi kwa kutokuwajibika ipasavyo na hivyo kupelekea Bunge kuteua kamati maalum na kufanya kazi iliyopaswa kufanywa na CAG, Kimsingi kwa gharama ya Kodi za Wanzanchi. Kwanini mtu huyu aendelee kutumikia umma hadi leo????WANAJF NAMLETA KWENU MTU HUYU. Nini kifanyike juu yake wakati huu anasubiri adhabu kama Bunge lilivyoishauri Serikali??Mi naona hana sifa ya kushika mafile ya Serikali.........wewe waonaje??
   
 2. a

  adobe JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2011
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 293
  Trophy Points: 180
  We acha wivu wa kijinga.makosa mangapi yametendwa na viongoz tena ya dhahiri na yenye thamani kubwa hakuna kinachotokea sembuse ripoti
   
 3. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Unataka atende makosa mangapi ndio uone kunahaja ya kumwajibishi????Je unajua katenda mangapi ya hovyo hadi leo kwa tabia hiyo aloionyesha???Zipo kazi nyingi ambazo mtu mwongo mwongo na mpotoshaji anaweza akafanya, sio lazma afanye hii ya umma hasa kwa nafasi nyeti ambayo inahitaji mtu makini na asiye mpotoshaji. Kwani Balali, Karamaga, Lowasa, Mzee Mwinyi,Simba, Msabaha etc walifanya makosa mangapi kabla ya wao kuwajibishwa/kujiwajibisha??? ???kwanini inakushangaza kwa CAG??what is so special??.

  Nadhan hujajua dhana nzima ya utawala bora na uwajibikaji inafanyaje kazi, hatuhesabu idadi ya makosa ili kumwajibisha mtu/mtu kujiwajibisha. Pia taratibu chagua maneno ya kutumia unapowasiliana na Public! Maneno kama wivu wa kijinga sidhan kama yanavumilika sana kwenye public communication. Hata kama ni baba yako, hana sifa za kuaminiwa ni mpotoshaji. Haya sio maneno yangu mbona nimekwambia yapo kwenye ripoti za Bunge iweje unaona mm na sio bunge kuwa linamwonea wivu wa kijinga??? After all uli take any trouble kusoma ripoti ya kamati maalum ya Bunge kabla ya Kuargue case??? Nchi haiwezi kuendeshwa kwa utaratibu unaotueleza wewe wa kufumbia macho watumishi wapotoshaji??Usijifungie tu hapa nyumbani, nenda hadi kwenye Duru za siasa za kimataifa then utajua kwanini CAG hana sifa ya kufanya kazi for the public interests. Kimsingi ukishashindwa kudefend public interest at least once huna sifa za kuaminiwa tena na ndio maana JK na utawala wake tunaona wamepoteza sifa za kuutumikia Umma. Ila haikatazwi kama CCM inaona bado inamwitaji, wampe kazi za chama lakin hizi za kulipwa mshahara kutokana na kodi zetu sisi anaotudanganya ni BIG NO!!
   
 4. Shakazulu

  Shakazulu JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2011
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 940
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mentality kama hii ndio imeifikisha nchi mahali ilipo hivi sasa. Bado tuna safari ndefu sana.
   
 5. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #5
  Dec 30, 2011
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  kwani Kuna serikali TZ???!!!
   
 6. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Huyo bwana/dada ukimchunguza utagundua ni zao la wezi wa nchi hii, maana haiingii akilin kwa mtu mwenye uzalendo kuwa na mtazamo wa aina hiyo.
   
Loading...