Kwanini Bunge (Ndugai) Alizima swali la mauwaji ya Kigoma toka kwa mbunge wa CCM? Yawezekana Zitto yuko sahihi polisi na serikali lao moja

dosama

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
912
957
kigoma+pic.jpg

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango na Naibu wake Dk Ashatu Kijaji wakifuatilia michango ya wabunge kuhusu mpango wa maendeleo wa Taifa na mwongozo wa maandalizi ya mpango wa bajeti ya mwaka 2019/20 jijini Dodoma. Picha na Ericky Boniphace

Kwa ufupi
Jana Jumanne Novemba 6, 2018, Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Josephine Genzabuke ameibua sakata la vifo vya wananchi katika mkoa wa Kigoma, lakini Spika wa Bunge, Job Ndugai amezuia swali lake.

-------------

Dodoma. Sakata la vifo vya wananchi na polisi mkoani Kigoma vilivyosababishwa na mgogoro wa ardhi hivi karibuni limeibukia bungeni, ikiwa ni siku chache baada ya Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe kukamatwa na kisha kushtakiwa.

Zitto alikamatwa wiki iliyopita na kushtakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, baada ya mkutano wake na wanahabari kuzungumzia suala hilo.

Wiki chache zilizopita, polisi walikiri kutokea kwa mapigano yaliyosababisha vifo vya watu wawili na askari wawili waliokwenda kwa ajili ya kulinda amani huko Uvinza.

Jana, mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Josephine Genzabuke ndiye aliyeliibua bungeni akihoji ni kwa nini Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) wamekuwa wakiua na kuwatesa wananchi ambao Rais John Magufuli aliwataka kukaa eneo la Kagerankanda bila ya kuongeza mipaka wakati Serikali ikiwatafutia maeneo mengine.

Baada ya majibu ya Serikali kutoka kwa Naibu Waziri wa Malisili na Utalii, Japhet Hasunga, mbunge Genzabuke alisimama kwa kuuliza swali la nyongeza lililoonekana kumkera Spika Job Ndugai. Genzabuke alihoji,

“Hawa TFS wanaua watu, wanawakata mikono na kuwatesa, kwa nini wanafanya hivyo wakati Rais aliagiza wasibuguziwe.”
Katika swali lake la nyongeza, mbunge huyo alihoji kama TFS wanapingana na agizo la Rais lililotaka wananchi wa maeneo ya Kagerankanda waendelee kulima bila kuongeza maeneo.

Hata hivyo, Spika Ndugai alimzuia kuendelea na swali hilo akisema mambo anayozungumza ni mazito na kumtaka akae chini. Licha ya mbunge huyo kutaka kuendelea kujenga swali lake, lakini aliitwa mbunge mwingine.

Baadaye Ndugai alisimama na kutoa ufafanuzi kwa kukemea maswali aliyosema ni mazito ambayo yalipaswa kupelekwa kwa Waziri Mkuu na si kuulizwa kama ya nyongeza bungeni.

Baada ya kipindi cha maswali na majibu, Mbunge wa Mbozi (Chadema), Pascal Haonga aliomba mwongozo akitaka kuhoji ni kwa nini Spika alimzuia mbunge huyo kuuliza swali la nyongeza.

Spika alimkatiza akisema jambo hilo alishaliondoa kwenye mjadala, hivyo halikuwa na ulazima tena wa kuulizwa mbele ya Bunge.

Awali, katika majibu ya swali la msingi, Naibu Waziri Hasunga alikiri kuwa Rais Magufuli aliagiza ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Kigoma kuwapimia wananchi eneo hilo.

Hasunga alisema jumla ya hekta 10,012.61 zilitengwa kwa ajili ya kilimo kwa wananchi wa maeneo hayo na kijiji cha Mvinza kilipewa hekta 2,174, Kagerankanda 2,496 na eneo lingine la hekta 5,342.61 lilitengwa kwa ajili ya wananchi wengine.
 
Suala lipo kwenye uchunguzi hivi so vema serikali au bunge kuingilia uchaguzi
 
yaibukia bungeni

kigoma+pic.jpg

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango na Naibu wake Dk Ashatu Kijaji wakifuatilia michango ya wabunge kuhusu mpango wa maendeleo wa Taifa na mwongozo wa maandalizi ya mpango wa bajeti ya mwaka 2019/20 jijini Dodoma. Picha na Ericky Boniphace
Kwa ufupi
Jana Jumanne Novemba 6, 2018, Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Josephine Genzabuke ameibua sakata la vifo vya wananchi katika mkoa wa Kigoma, lakini Spika wa Bunge, Job Ndugai amezuia swali lake.
By Habel Chidawali, Mwananchihchidawali@mwananchi.co.tz
Dodoma. Sakata la vifo vya wananchi na polisi mkoani Kigoma vilivyosababishwa na mgogoro wa ardhi hivi karibuni limeibukia bungeni, ikiwa ni siku chache baada ya Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe kukamatwa na kisha kushtakiwa.
Zitto alikamatwa wiki iliyopita na kushtakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, baada ya mkutano wake na wanahabari kuzungumzia suala hilo.
Wiki chache zilizopita, polisi walikiri kutokea kwa mapigano yaliyosababisha vifo vya watu wawili na askari wawili waliokwenda kwa ajili ya kulinda amani huko Uvinza.
Jana, mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Josephine Genzabuke ndiye aliyeliibua bungeni akihoji ni kwa nini Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) wamekuwa wakiua na kuwatesa wananchi ambao Rais John Magufuli aliwataka kukaa eneo la Kagerankanda bila ya kuongeza mipaka wakati Serikali ikiwatafutia maeneo mengine.
Baada ya majibu ya Serikali kutoka kwa Naibu Waziri wa Malisili na Utalii, Japhet Hasunga, mbunge Genzabuke alisimama kwa kuuliza swali la nyongeza lililoonekana kumkera Spika Job Ndugai. Genzabuke alihoji,
“Hawa TFS wanaua watu, wanawakata mikono na kuwatesa, kwa nini wanafanya hivyo wakati Rais aliagiza wasibuguziwe.”
Katika swali lake la nyongeza, mbunge huyo alihoji kama TFS wanapingana na agizo la Rais lililotaka wananchi wa maeneo ya Kagerankanda waendelee kulima bila kuongeza maeneo.
Hata hivyo, Spika Ndugai alimzuia kuendelea na swali hilo akisema mambo anayozungumza ni mazito na kumtaka akae chini. Licha ya mbunge huyo kutaka kuendelea kujenga swali lake, lakini aliitwa mbunge mwingine.
Baadaye Ndugai alisimama na kutoa ufafanuzi kwa kukemea maswali aliyosema ni mazito ambayo yalipaswa kupelekwa kwa Waziri Mkuu na si kuulizwa kama ya nyongeza bungeni.
Baada ya kipindi cha maswali na majibu, Mbunge wa Mbozi (Chadema), Pascal Haonga aliomba mwongozo akitaka kuhoji ni kwa nini Spika alimzuia mbunge huyo kuuliza swali la nyongeza.
Spika alimkatiza akisema jambo hilo alishaliondoa kwenye mjadala, hivyo halikuwa na ulazima tena wa kuulizwa mbele ya Bunge.
Awali, katika majibu ya swali la msingi, Naibu Waziri Hasunga alikiri kuwa Rais Magufuli aliagiza ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Kigoma kuwapimia wananchi eneo hilo.
Hasunga alisema jumla ya hekta 10,012.61 zilitengwa kwa ajili ya kilimo kwa wananchi wa maeneo hayo na kijiji cha Mvinza kilipewa hekta 2,174, Kagerankanda 2,496 na eneo lingine la hekta 5,342.61 lilitengwa kwa ajili ya wananchi wengine.
Ukweli hautakiwi kbs ktk nchi ya jiwe,na wanaosimamishwa km viongozi hawatakiwi kuruhusu negativity kwake,Ndugai anatekeleza
 
Hakulipokea swali kwa kuwa hakupokea maelekezo ya kulipokea hilo swali kutoka mzizi uliojichimbia chini zaidi
 
Ukiona suali limezuiwa jua hilo ndilo suali linalohitaji majibu zaidi tena na ufafanuzi mkubwa na kuchukuliwa hatua kwa haraka zaidi
 
Back
Top Bottom