Kwanini bunge lisiwaandikie Benki ya Dunia kupinga hoja za Mbunge Zitto badala ya "kutamani" kuchukua njia ya mkato?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,616
141,447
Bahati nzuri Bunge letu limesheheni wabobezi na ngumbaro wachache, sasa kwanini hoja za Zitto zisijibiwe kwa hoja?

Zitto ameiandikia Benki ya Dunia katika nafasi yake kama Mbunge na siyo kiongozi wa chama. Hivyo Bunge lina nafasi nzuri ya kumkanusha Zitto kwa kuiandikia WB ukweli ulivyo badala ya kumshambulia Zitto kama mtu binafsi.

Niwape changamoto hii mzee Chenge na Dr Tulia: tumieni weledi na kuweka siasa pembeni ili jambo hili liishe.

Maendeleo hayana vyama!
 
Hoja murua ina mashiko.....Kwa nini hawakutaka kuzijibu hoja za Lissu na badala yake wakakitaka kichwa chake niletwe mezani kama kile cha Yohana Mbatizaji.

Ni muendelezo tu wa awamu ya kushindwa kujibu hoja !!

CCM inasema Kuzipangua hoja zinazomulika ukweli si kazi ya kitoto chief....Why don't u use the 2nd option inayoonekana kuwa nyepesi less risk?
 
Hawana hoja ya msingi ya kuhalalisha upatikanaji wa mkopo huo.

Serikali ya Meko inafanya vizuri kwenye matumizi ya nguvu na inafeli panapihitajika weledi.

Hakuna mbunge wa CCM mwenye uwezo wa kujenga hoja. Wote ni waropokaji tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hoja za Zito huwa hazijibiwi kif*la. Lile jiwe likitoa hoja lazima muweke kikao na mjilipe posho kabisa ili angalau mjaribu kuzijibu
 
Eti wanadai ni sisi tu wa JF tunaojua pini ya Bashite kwenda duniani. Huko kitaa hawayajui.
Hao ndiyo aina ya watu wanaodhani kwamba wanaijua sana dunia. Wanachojua wenyewe ni kuwa asubuhi au jioni wanapo simama basi pale kinaishia kivuli chao hapo ndipo zilipo kingo za dunia.

Ni aina ya watu wanaodhani kwamba kila awashae taa au tochi usiku wakati wa kutembea basi ana matatizo ya kuona, hawafikirii kwamba mara nyingine muwasha taa hufanye vile wasii ona wasije wakamkumba.

Wanaamini kuwa wamejificha, hawajui zama hizi maisha yetu ni kama tunaishi kwenye nyumba ya vioo huku taa zikiwaka.
 
Huo ndio ukweli wenyewe!
Siku hizi huko vijijini usiku watu wanakusanyika wanaangalia taarifa ya habari,kuna kijiji kimoja kinaitwa Mwisi,nilishangaa nilipoenda nikakuta watu wanagonga kahawa huku wakicheki BBC dira ya dunia,nilipouliza nikaambiwa mbona huo utaratibu wanao muda mrefu,huwa wanaanza na chanell ten saa 1,saa 2 wanaweka azam news na saa 3 wanamalizia na Star tv BBC dira ya dunia!
Sasa hivi mambo yamebadilika!
 
Back
Top Bottom