Kwanini bunge letu lisivunjwe katika mabunge mawili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini bunge letu lisivunjwe katika mabunge mawili?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Godwine, May 16, 2010.

 1. G

  Godwine JF-Expert Member

  #1
  May 16, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Nadhani imefika wakati wa kuligawa Bunge letu katika sehemu mbili ili kuongeza ufanisi na kupunguza madhaifu yanayojitokeza kwa sasa kwani bunge moja linakuwa limeshehena kazi nyingi kupita uwezo wa mipango yake . nionavyo mimi tunaweza kuwa na mabunge mawili ambayo kila moja linaweza kuwa na wawakilishi kama 120 na kuwa na majukumu yake kuliko kuendelea kuwa na bunge moja ambalo zaidi ya asilimia 90% ya wabunge wake wanakuwa wamelala wakati miswada ikiwa inaendelea. tukiwa na mabunge mawili yenye wajumbe wachache inaweza kufanya wabunge wengi kuwa wafuatiliaji na kuongeza ufanisi na usimamizi na ata ufuatiliaji wa mikataba inayoliumiza taifa letu.
   
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  May 16, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Heshima mbele mkuu Godwine. Mkuu ukiangalia nchi karibia zote zenye mabunge mawili una kuta hao wana fuata mfumo wa federal government. Kwa maana serikali kuu ina mamlaka yake na serikali za majimbo nazo zina mamlaka yake yanayo jitegemea. Maana ya kuwa na mabunge kwenye federal states ni hivi. Labda nitoe mfano wa Marekani.

  1)Bunge moja lina fuata uwakilishi wa watu. Kwamba mbunge mmoja ana wakilisha watu wa idadi fulani. Kwa Marekani hii ni Congress ambao wawakilishi wao wana toka kwenye constituencies na kila Constituency ina wakilisha watu wa idadi fulani. Hii ina maana majimbo yenye watu wengi zaidi ina toa wawakilishi wengi zaidi.

  2)Bunge la pili ni la majimbo. Kwa maana haijalishi ukubwa wa jimbo lakini kila jimbo lina toa idadi fulani ya wabunge. Kwa Marekani hii ni senate anbalo kila jimbo lina toa maseneta wawili au watatu kama sikosei. Hii ina toa balance kwa Congress kwa maana hata majimbo madogo inapo kuja kwenye senate wana nguvu na uwakilishi sawa na majimbo makubwa in theory.

  Sasa kwa nchi kama ya kwetu kuwa na mabunge mawili yanayo fuata practicality ina maana mikoa nayo lazima iwe na nguvu na chaguzi inayo jitegemea. Kwa maana mkuu wa mkoa ana chaguliwa na wananchi na si raisi na serikali ya mkoa ina kuwa na mamlaka ambayo haitegemei serikali kuu. Sasa hivi serikali za mikoa zinafuata tu maagizo ya serikalo kuu.

  Just a foot note: Kwa Tanzania chama kinacho unga mkono serikali ya majimbo ni Chadema kama ilivyo ainishwa kwenye ilani yao mwaka 2005 na kupiganiwa na mwenyekiti wao Freeman Mbowe.
   
 3. G

  Godwine JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2012
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Miaka miwili toka kutolewa wazo la kuwa na Mabunge mawili CCM kupitia kikao chake cha chama CC na NEC wameamua kulifanyia kazi, ni vema wameliona hili lakini kikubwa ni waweke mfumo madhubuti ya upatikanaji wa mabunge yenye nguvu na si mihuri ya watawala
   
 4. G

  Godwine JF-Expert Member

  #4
  Jan 15, 2013
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  hatimaye mawazo yamefika kwenye katiba sasa
   
Loading...