Kwanini binadamu yeyote mwenye roho na matendo mema kifo humpata mapema?

jitombashisho

JF-Expert Member
Jun 11, 2020
519
1,000
Ulishafanya utafiti kwako na kama bado nashauri ufanye.

Ipo hivi watu wenye roho na matendo mema huwa ni vigumu mno kuzidi umri wa 50+. Wengi wao hufariki chini ya umri huo na kawaida vifo vyao huacha simanzi kuu!

"...baba wa watu alikuwa mwema ama kijana wa watu ndiyo kwanza ameanza maisha ama binti wa watu ndiyo ilikuwa mimba yake ya kwanza".... ni baadhi ya maneno yenye kusononeka utayoyasikia kutoka katika hadhira inayoomboleza misiba mingi ya watu wema.

Binafsi huwa najiuliza sana kwa kifo huwapata mapema watu wenye tabia za namna ile?
 

t blj

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
3,350
2,000
The good die young, 2pac Shakur, nilipata shida sana kuusilikilza wimbo huu siku aliyouwawa 2Pac, ni kama alikuwa anajiimbia yeye, 26 years only hata 30 hakufika.
 

Sang'udi

JF-Expert Member
May 16, 2016
2,991
2,000
Kila mmoja wetu anapozaliwa huwa na mission anayopaswa kui-accomplish.

Wema wengi hu-accomplish missions zao mapema na kurudi kwa Mungu. Wengi wa wasiyo wema hudumu maana Mungu huendelea kuwapa nafasi ya ku-accomplish missions zao.

RIP JPM, ulienda mapema sana tukiwa bado tunakuhitaji.
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
10,756
2,000
Pana nadharia nyingi kuhusiana na vifo. Katika zote nadharia hii inasimama:


Inawabeba wakwenda zao wote na bila exception.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
10,756
2,000
Kufa hakunaga mapema wala kuwahi

Mwenye kifo chake ndio anajua siri hii

Mkuu kwa mukthadha huu:


Kufa mapema kipo.
 

Haki na maendeleo

Senior Member
Jun 15, 2021
114
250
Unampimaje mtu kuwa ni mwema??? YESU aliwahi kuitwa mwema akakataa akasema Mungu pekee ndiye mwema, hivyo kusema kwamba huyu mtu ni mwema huna kipimo maalum kinachoonyesha wema wa mtu, mtu anaweza kuongea vizri lakini moyoni mwake ni mbaya kuliko unavyofikiri, au akiwa gizani hujui anayoyafanya!! Kikubwa kuishi ni kristo kufa ni faida!! Swala la kifo mda ukifika umefika huwezi kuzuia, wanaomcha Mungu miaka wanaishi mda mrefu kuliko unavyofikiria ukiona wamekufa mapema ujue kuna jambo limesababisha, nzr kwa maana ya kumaliza kazi yao au umemkosea Mungu inakuwa ni njia moja wapo ya adhabu yako!!( mwenye kuuujua ukweli ni Mungu tu)
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom