Kwanini binadamu tunapenda kureact katika mambo hasi kuliko mambo chanya?

CHAMVIGA

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
7,687
2,238
Ukifutalia kwa karibu utagundua wafanyakazi wa ndani kama housegirl wanajitahidi sana katika kuwajibika kwa mujibu wa majukumu wanayopangiwa na mabosi wao kama kuangalia watoto,kuwapikia na kuwapeleka shule n.k.

Chakusikitisha wanapokosea kwa bahati mbaya kama kucheleesha chakula au kuwaandibu watoto wa mabosi wao hukumbana na wakati mgumu sana kutoka kwa waajiri wao, ni kwanini huwa mabosi wanasahau wema wote wa wafanyakazi wao na kuwakalipia ima kuwapiga vibaya kwa kosa moja tu?

Mtoto anafanya mazuri mengi lakini akikosea mara moja tu wazazi husahau mazuri yote na kuambulia kipigo kutoka kwa wazazi au walimu wake?
KWANINI REACTION HIZI HAZIJITOKEZI WAKATI MTU AKITENDA MAZURI ILA HIJITOKEZA AKISHAFANYA MABAYA TU?
 
Ni kweli takribani muda mrefu waajiri huwa hawatendei haki wafanyakazi wa ndani sababu kubwa ni kutofata misingi ya dini inavyosema mhudumie mtumwa wako kam unavyojihudumia ww mwenyewe
 
Ukifutalia kwa karibu utagundua wafanyakazi wa ndani kama housegirl wanajitahidi sana katika kuwajibika kwa mujibu wa majukumu wanayopangiwa na mabosi wao kama kuangalia watoto,kuwapikia na kuwapeleka shule n.k.

Chakusikitisha wanapokosea kwa bahati mbaya kama kucheleesha chakula au kuwaandibu watoto wa mabosi wao hukumbana na wakati mgumu sana kutoka kwa waajiri wao, ni kwanini huwa mabosi wanasahau wema wote wa wafanyakazi wao na kuwakalipia ima kuwapiga vibaya kwa kosa moja tu?

Mtoto anafanya mazuri mengi lakini akikosea mara moja tu wazazi husahau mazuri yote na kuambulia kipigo kutoka kwa wazazi au walimu wake?
KWANINI REACTION HIZI HAZIJITOKEZI WAKATI MTU AKITENDA MAZURI ILA HIJITOKEZA AKISHAFANYA MABAYA TU?

Ndio maana wengine wanatoa 2weeks wajieleze kwa nini wasifukzwe kazi ,ni kweli kabisa mkuu watu hawana subra
 
Jamii ndivyo ilivyo....
Fanya mazuri mengi ila ukikosea step kidogo tu..ni kama wanasahau mazuri yako yote.
Sehemu pekee ambayo mazuri yako yatAkumbukwa ni kwenye msiba wako wakati wakisoma wasifu wa marehemu.
Hata kwenye mpira goal keeper ataokoa mipira mingi kweli ila mmoja au miwili iliyompita ndio utakumbukwa na kumhukumu.
 
Hapa kwetu mahouse girl hawana haki na ndio maana wengine hufikia hata hatua ya kuchapwa na maboss wao kitu ambacho si sawa. Unajua ukitaka kuujua umuhimu wa house girl subiri aondoke kama mwezi hivi . Halafu kuna watu huwa hawana shukrani hata uwafanyie nini mahouse girl wanafanya kazi nyingi sana na mshahara wenyewe wanolipwa ni mdogo.

Najua inauma unapokuta hg amekosea lkn ukiweza kuvaa kiatu chake utaelewa amekosea kwa sababu ya uchovu na udhaifu wa kibinadmu. Hebu oneni hg asafishe nyuma, afue nguo , aaandae chakula cha familia na hapo hapo atake care mtoto mbona mambo haya ni mengi sana. Tatizo la hapa kwetu mnyonge hana haki sheria zipo lkn zinasimamiwa na wenye nazo na hao hao baadhi yao utakuta majumbani mwao wanafanya manyanyaso sasa utaenda wapi.
 
Tatizo kubwa ni ukosefu wa upendo,kama una upendo utampenda na kumjali kama mtoto wako kwahiyo hutoweza kumfanyia mabaya yoyote kama ambavyo baadhi ya watu wanafanya kwenye jamii yetu kama kuwapiga,kuwanyima chakula,kuwaunguza moto,baba/watoto wa mwenye nyumba kuwapa ujauzito na kuwafukuza bila hata kuwasikiliza,kuwanyima mishahara yao na maovu ya kila aina lakini hayo yote ni sababu watu tumekosa upendo
 
Kwenye upendo kuna amani kweli ndugu yangu.
 
Hapa kwetu mahouse girl hawana haki na ndio maana wengine hufikia hata hatua ya kuchapwa na maboss wao kitu ambacho si sawa. Unajua ukitaka kuujua umuhimu wa house girl subiri aondoke kama mwezi hivi . Halafu kuna watu huwa hawana shukrani hata uwafanyie nini mahouse girl wanafanya kazi nyingi sana na mshahara wenyewe wanolipwa ni mdogo.

Najua inauma unapokuta hg amekosea lkn ukiweza kuvaa kiatu chake utaelewa amekosea kwa sababu ya uchovu na udhaifu wa kibinadmu. Hebu oneni hg asafishe nyuma, afue nguo , aaandae chakula cha familia na hapo hapo atake care mtoto mbona mambo haya ni mengi sana. Tatizo la hapa kwetu mnyonge hana haki sheria zipo lkn zinasimamiwa na wenye nazo na hao hao baadhi yao utakuta majumbani mwao wanafanya manyanyaso sasa utaenda wapi.

Ni kweli kabisa ndugu ila tatizo hili lipo worldwide sema tu huku pande za kwetu ndio limekuwa kubwa.
 
Jamii ndivyo ilivyo....
Fanya mazuri mengi ila ukikosea step kidogo tu..ni kama wanasahau mazuri yako yote.
Sehemu pekee ambayo mazuri yako yatAkumbukwa ni kwenye msiba wako wakati wakisoma wasifu wa marehemu.
Hata kwenye mpira goal keeper ataokoa mipira mingi kweli ila mmoja au miwili iliyompita ndio utakumbukwa na kumhukumu.

Hata avatar yangu inalizungumza hili mkuu.
 
Lakini naomba tupanue mawazo yetu zaidi katika kulipambanua jambo hili tusiishie kwa mahousegirl pekee japokuwa mimi nimewatumia kama casestudy yangu. Jambo la kureact katika matukio hasi ni pana sana na karibu linaingia katika kila tukio la kimaisha kuliko vile ambavyo mtu atareact katika jambo jema. Mfano mzuri tu ni huyu Kapuya na skendo yake ya binti hivi ni kwanini watanzania tumelivalia njuga sana kuliko hata mema ya Kapuya aliyoyafanya? Hapa ondoa sababu za kisiasa.
 
aiseeee..,haya ni madhara ya ki2 kinachouzwa na watoto wa kapuya.daah!!!hv kumbe jamii forum imesheheni watu wakila namna enh?Sasa oneni huyu teja!!!eti "weka picha"Eti bandugu,kuna haja ya picha hapa?

Atakuwa amecoment huku kasinzia huyu au analeta jokes.
 
Naona wachangiaji wengi wanachangia in a parochial manner confining to housegirls and boys only ilhali nadhani mada ni pana na mleta mada ametumia housegirl kama mfano tu.
Kifupi ni kwamba binadamu anapenda kuona mazuri na hutarajia mazuri most of the time na ndio maana linapoibuka baya anakuwa upset kwani ni kinyume na matarajio na matamanio yake. Ni busara tu inataka tujue kuwa mabaya huambatana na mazuri yanapokuja. "Wish for good but expect bad as well".
 
Ni kweli kabisa ndugu ila tatizo hili lipo worldwide sema tu huku pande za kwetu ndio limekuwa kubwa.
Inawezekana lkn bado nashindwa kuamini kama lipo worldwide kwani nchi zingine hakuna uonevu wa namna hii na ikigundulika unachukuliwa hatua kali. Zipo nchi sheria inafanya kazi mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom