Kwanini bima ya afya hasa NHIF haitumiki kwa wagonjwa wa macho na jino?

escrow

JF-Expert Member
Sep 27, 2016
371
321
Wakuu kama maada ilivyojieleza hapo juu, naomba kujua sababu kwa nini wagonjwa wa macho hasa huduma ya miwani na wale wa meno hawatibiwi kwa bima?

Ni kwamba mara ya kwanza nilienda kutibiwa macho nikiwa na BIMA lakini sikuweza kupata huduma baada ya kuambiwa miwani najitegemea kwa malipo nje ya Bima.

Hivi karibuni nimeenda tena na kadi NHIF ili nihudumiwe jino lilikuwa linauma lakini ikawa tofauti na huduma nikaambia jino halitumii Bima.

Naomba anayejua sababu anijuze kwa ufasaha.
Shukrani sana!!
 
Kama sijakosea bima kuna baadhi ya matibabu ambayo hawaruhusu kufanywa na bima ,mfano Matibabu ya meno ,Miwani ,na oppression za urembo mfano mtu anayetaka kuongeza makalio nk, hii ni kwa sababu haya matibabu hayana kiwango maalum ya kiasi kitakachotakiwa kulipwa mfano mtu anaweza kwenda kutibiwa menu akaomba kuwekewa meno ya dhahabu yenye gharama ya zaidi 2,000,000 na kuendelea .
Asante mkuu!!
 
Wakuu kama maada ilivyojieleza hapo juu, naomba kujua sababu kwa nn wagonjwa wa macho hasa huduma ya miwani na wale wa meno hawatibiwi kwa bima?
Ni kwamba mara ya kwanza nilienda kutibiwa macho nikiwa na BIMA lakini sikuweza kupata huduma baada ya kuambiwa miwani najitegemea kwa malipo nje ya Bima.
Hivi karibuni nimeenda tena na kadi NHIF ili nihudumiwe jino lilikuwa linauma lakini ikawa tofauti na huduma nikaambia jino halitumii Bima.
Naomba anayejua sababu anijuze kwa ufasaha.
Shukrani sana!!
Kuhusu miwani bima wanalipa ila kwa wanachama wachangiaji tu na kuna kiwango.

Meno unatibiwa. Nimetibiwa Kairuki mwaka jana tu. Labda hosp uliyokwenda wao ndio wana sharti la kutotibu baadhi ya matatizo kwa bima.

Hii suala niliwahi kuliona hosp flani binafsi. Wanapokea bima ya NHIF ila baadhi ya matibabu wanakataa sababu eti bima wametenga kiwango kidogo kulilo wanachochaji wao.
 
Shukrani sana mkuu
 
Nakumbuka nishanunua miwani kwa bima. Lakini kuna amount wameweka. Ikizidi hapo ile iliyozidi unajazia mwenyewe. Nimechukua miwani mara 2 ccbrt. Na wao nhif wakanipigia simu kuconfirm kama nilipata hiyo huduma. Ila sijui kama utaratibu umebadilika.
 
Shukrani sana mkuu!
 
Hivi kwa sisi ambao ni wananchi wa kawaida tuliojiajiri tunawezaje kupata bima ya nhif?
 
Bima unapata ila ni gharama kubwa!
NHIF 1mil....
Nzuri ni ile ya CHF inakuwa na gharama nafuu
 
Kama sijakosea bima kuna baadhi ya matibabu ambayo hawaruhusu kufanywa na bima ,mfano Matibabu ya meno ,Miwani ,na oppression za urembo mfano mtu anayetaka kuongeza makalio nk, hii ni kwa sababu haya matibabu hayana kiwango maalum ya kiasi kitakachotakiwa kulipwa mfano mtu anaweza kwenda kutibiwa menu akaomba kuwekewa meno ya dhahabu yenye gharama ya zaidi 2,000,000 na kuendelea .
Sizan kama hiyo ndo sababu, ×ray, ct scan na MRI unadhani gharama ni sawa !!?
 
Meno,macho utatibiwa ila si kwa vituo vya afya ,zahanat bali kwa hospitali zenye hadhi na wataalamu wa huduma hizo wanaotambuliwa
 
Kama sijakosea bima kuna baadhi ya matibabu ambayo hawaruhusu kufanywa na bima ,mfano Matibabu ya meno ,Miwani ,na oppression za urembo mfano mtu anayetaka kuongeza makalio nk, hii ni kwa sababu haya matibabu hayana kiwango maalum ya kiasi kitakachotakiwa kulipwa mfano mtu anaweza kwenda kutibiwa menu akaomba kuwekewa meno ya dhahabu yenye gharama ya zaidi 2,000,000 na kuendelea .
Mbona meno wanatibu Mimi nilitumia kutibiwa Arusha . Tena pesa ilikuwa kubwa nazani bila Bima ningeshindwa
 
Hivi kwa sisi ambao ni wananchi wa kawaida tuliojiajiri tunawezaje kupata bima ya nhif?
Jiungeni kwenye vikundi vya ujasiriamali (KIKOA) mtapata bima kwa gharama nafuu nafuu sana kwa mwaka (50400) kwa mwaka

Alternatively ,lipa 1.5 M kwa mwaka kwa package ya watu sita
 
Hivi kwa sisi ambao ni wananchi wa kawaida tuliojiajiri tunawezaje kupata bima ya nhif?

Unaweza kupata na siku hizi kuna vifurushi kulingana na uhitaji. Unaweza kupata kwa kiwango kuanzia shilingi 190,000/=, laki tatu na kwenda juu.

Wasiliana na ofisi ya NHIF iliyo karibu yako au mtandao wao kwa maelezo zaidi.
 
Back
Top Bottom