Kwanini Bill ya umeme ni kubwa kuliko matumizi yetu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Bill ya umeme ni kubwa kuliko matumizi yetu?

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Apollo, Sep 15, 2012.

 1. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,356
  Trophy Points: 280
  Hapa ninapokaa tunatumia unit 18 kwa siku tano. Hivyo kwa mwezi tunaweza tukatumia zaidi 25,000 kwa mwezi tu. Cha kushangaza hatuna vitu vya kutumia umeme mfano heater, pasi tunatumia mara chache maana nguo zinakunjwa, taa tunatumia powersavers, TV hatuangalii sana na friji tunaitumia ila umeme ukiwa mdogo tunaizima.

  Zamani kuna nyumba tulikuwa tunakaa, tulikuwa tunatumia Sh 10000 kwa mwezi tena kwa vitu hivihivi tulivyonavyo bila kubadilisha matumizi.

  Je kuna mita za luku zinatumia bei kubwa? Au tumewekewa mita ya kibiashara zaidi? Kuna watu wamesema (mafundi vishoka) kuna kifaa cha ku-control umeme hakikuwekwa na Tanesco. Je ni kweli umeme unapotea njiani au? Bado sijaelewa kwanini bill imeongezeka.
   
 2. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,937
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Nijuavyo mimi ni gharama za umeme ziliongezeka kinyemela na watu wengi hawajui...kuna kipindi Tanesco walitaka kupunguza bei lkn haikuwezekana kwa sababu wanafanya risechi ya matumiz na bei. Kuhus unit kwenda san hiyo sijui lkn labd kun tatiz la kiufund
   
 3. Donn

  Donn JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,450
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Mm mpaka nimeondoa huo umeme wao. Nimefunga sola ya nguvu. Ndani ya mwaka mmoja naletewa bili milioni9 utasema ninakiwanda. Chaajabu nimeenda kucheki mtandaoni kwao nimekuta bili kwa mwezi 4000, 5000 akadai eti hapo zitakuwa na makosa ndomaana wameleta bili kubwa. Hapo hapo akapunguza bila kupiga mahesabu mpaka Milioni 5. Sasa huu kama si wizi ni nini?
   
 4. G

  Grim Reaper Member

  #4
  Sep 15, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Fund mmoja wa Tanesco alisema sometimes kunakuwa na errors ktk kukupa mita instead ya kukpa ya home use wanakupa for industrial use so ths can b the reason
   
 5. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,356
  Trophy Points: 280
  Donn pole sana ila safi kwa uamuzi mzuri wa kuepukana na usumbufu wao kwa kuweka Solar, Ila tuliyonayo ni Mita ya luku, sasa sijajua kuna mita za kibiashara na mita za matumizi ya kawaida au? Maana hii inaonekana ya kibiashara zaidi.
   
 6. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #6
  Sep 15, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,356
  Trophy Points: 280
  Asante mkuu, na hichi ndicho nilichokuwa nashindwa kuelewa, sasa naona wanataka kutukomesha? MITA YA KIWANDA NYUMBANI KWA MTU? Looooh!
   
 7. Donn

  Donn JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,450
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Dah.. Kama ni luku hapo ishue, alafu wanakuwa watata sana ukiongelea kuhusu vifaa vyao.
   
 8. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,651
  Likes Received: 8,207
  Trophy Points: 280
  Mh..this one imenivutia..
  Hivi ni kweli kuna luku za home use na za biashara??!
   
 9. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #9
  Sep 15, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,119
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  25,000 sio nyingi ndo bei halisi ya umeme hiyo.
   
 10. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #10
  Sep 15, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,356
  Trophy Points: 280
  Hapo ndio mimi najiuliza, wanasema za kibiashara ni zile za mfano viwandani, madukani, n.k Sasa sijajua ni kweli
   
 11. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #11
  Sep 15, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,356
  Trophy Points: 280
  Mhh, sasa kwa vifaa tunavyotumia ndio tunakuwa na mashaka mkuu.
   
 12. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #12
  Sep 15, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,119
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Za viwandani zina muundo tofatuti ninavyokumbuka ungekuwa na ya kiwandani ungejua, ni kwa ajili ya kupitisha umeme mwingi zaidi. Pia gharama za ziada zinaingia pale matumizi yanapokuwa mengi (kwa nyumba sio rahisi kufika huko), check website ya tanesco wamelist bei.
   
 13. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #13
  Sep 15, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,119
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Checki risiti zako, unatumia kWh ngapi kwa mwezi?
   
 14. Donn

  Donn JF-Expert Member

  #14
  Sep 15, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,450
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Ila za viwanda huwa 4 Ways au 3ways. Inategemea na ukubwa wa matumizi. Kwa kawaida za majumbani ni 2way.
   
 15. Paje

  Paje JF-Expert Member

  #15
  Sep 15, 2012
  Joined: Apr 24, 2010
  Messages: 1,198
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  unit moja ni sh. 160 kwa sasa. kuna flat rate sio kama zamani. hivyo kama mnatumia unit 18 bei yake ni 18x160 ambayo ni 2880 kwa wiki na kwa mwezi ni 2880x4 ambayo ni chini ya elfu 12. na sio kweli kuwa itakuwa ni zaidi ya elfu 25. kama ulivyosema wewe.
  matumizi yako ndio hayo ila inakubidi ulipie na kodi ya vat na service charge. ambayo hayo sio matumizi yako. service charge ni kama buku 4 hivi kwa mwezi. na vat ni asilimia 18 .
  bado unalipa rahisi mno ukilinganisha na mimi
   
 16. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #16
  Sep 16, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,356
  Trophy Points: 280
  mhh. Asante kwa kunipa maelekezo. Itabidi nifuatilie hili mapema.
   
 17. Sauli

  Sauli JF-Expert Member

  #17
  Sep 16, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 230
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 45
  aise me hapa home, frdj 1, bulb energy saver, mashne za kupoza na kuchemsha maj mbili, mayb na pump ya maj bt kwa mwez zaidi ya laki, yan tunatumia units kama 300 hv, cjui kama 2natendewa haki,
   
 18. W

  Wandugu Masanja JF-Expert Member

  #18
  Sep 16, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 1,535
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  aisee mbona mnalipa hela ndogo na mnapiga kelele
  Hivi ninavyolipa ni 120 000 kwa mwezi na matumizi ni kama hivi nina fridge moja freezer moja tv pasi computer, machine ndogo ndogo kama tatu na pump ya maji pia water heater na cooker
   
 19. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #19
  Sep 16, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  hivi ukubwa au udogo wa bill unaupimaje?
  Jaribu kuelewa mada
   
 20. W

  Wandugu Masanja JF-Expert Member

  #20
  Sep 16, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 1,535
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  naomba kukuuliza wewe umefahamu vipi?
  Tatizo hatuna umeme wa uhakika kwenye power drop na meter za kubahatisha kama una kifaa jaribu chunguza wakati umeme mdogo angalia meter yako na umeme unapobadilika angalia tena
   
Loading...