Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,013
- 144,371
Wadau, hivi kuna ugumu gani sisi kama nchi tukawa na sera ya kuruhusu makampuni binafsi kusambaza na kuuza umeme kwa wateja badala ya makampuni haya kuruhusiwa kuzalisha umeme tu na kisha kulazimika kuwauzia TANESCO ambao ndio wenye haki pekee ya kusambaza na kuuza umeme hapa nchi?
Faida ya kuwa na sera ya aina hii ni kama hizi zifuatazo:
1.Makampuni binafsi yakiuza umeme moja kwa moja kwa wananchi, bei bila shaka itashuka.
2.Tutakuwa tume-create ushindani hivyo mbali na bei kushuka, ubora wa huduma pia utaongezeka.
3.Serikalii itapata mapato kutoka katika makampuni binafsi yatayokuwa yakilipa kodi serikali.
4.Makampuni binafsi, kupitia sera hiyo, yanaweza pia kuwekaza katika eneo moja tu la kujenga miundombinu ya kusafirisha umeme na makampuni mengine yakatumia miundombinu hiyo na hivyo tunaweza kuondokana na tatizo la kukatika umeme kutokana na uchakavu wa miundombinu ya TANESCO.
5.Ajira zitazalishwa kupitia makampuni haya binafsi yanayoweza ku-opparate kwa ngazi ya wilaya, mkoa, kanda na hata ngazi ya kitaifa kutegemeana na uwezo na mtaji wa kampuni husika.
6. TANESCO itapunguziwa mzigo wa kuhudumia nchi nzima na hivyo inaweza kujiendesha kwa faida tofauti na ilivyo sasa.
7. Serikalini itaondokana na mzigo wa kuibeba TANESCO na kuokoa fedha nyingi za umma zinazoelekezwa katika kusaidia TANESCO.
8.TANESCO inaweza kutumia miundombinu yake kibiashara kwa makampuni mapya yanayoweza kutumia miundombinu ya TANESCO kwa malipo ya kibiashara.
9.Serikali inaweza pia kufanya biashara ya kuuza kwa makampuni binafsi ya kusambaza umeme kutoka katika vyanzo vyake vya kuzalisha umeme mfano Stieglers Gorge ikikamilika.
Tofauti na hapo, ni bora lile wazo la kuivunja TANESCO na kuwa na makampuni matatu ya kuzalisha,kusambaza na kuuza umeme likafanyiwa kazi kuondoa hii monopoly ya TANESCO katika hii biashara ya kuzalisha na kusambaza umeme.