Kwanini biashara nyingi ndogo hufa? Baadhi ya sababu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini biashara nyingi ndogo hufa? Baadhi ya sababu...

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by CHASHA FARMING, Jan 15, 2012.

 1. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #1
  Jan 15, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  Kufa kwa biashara nyingi ndogo ndogo na za kati


  MOJA YA SABABU ZA BIASHARA NYINGI KUFA NI HIZI

  a. Mtaji Mdogo

  Hili ni Tatizo kubwa kwa watu wengi sana, nasi hapa bongo pekee, bali ni nchi nyingi, Mitaji mara nyingi inakuwa midogo kuwezesha kampuni kufanya kazi mpaka pale itakapo weza kusimama yenyewe, Mitaji hukatika njiani hivyo kufanya mwenye biashara kufunga biashara yake, bila mtaji wa kutosha huwezi simama

  b. Kuweka biashara eneo ambalo silo

  Tunapoanzisha biashara mara nyingi tumekuwa tukiziweka mahali ambapo sipo, hii ni moja ya sababu za biashara nyingi ndogo kufa mapema, huwa hakuna utafiti wa kutosha wa ni wapi uweke ofisi ya biashara yako. MFANO

  UNAWEKASTATIONARY MAHALI PASIPO KUWA NA MASHULE WALA OFISI ZILIZO BIZE
  , hapa huwezi fanikiwa na ni lazima biashara ife. Kutafuta eneo linalofaa ni muhimu sana.


  c. Kutokuwa na Mpango kazi wa biashara yako/Mchanganuo

  Hii ni tatizo kubwa sana kwetu Tanzania, Utakuta mtu anaanzisha biashara ya Baa basi muulize nini mpango wake, je anataka kuwa wapi miaka mitano ijayo hakuna.

  TUNAAMKA ASUBUHI NA KUANZISHA BIASHARA MCHANA, HAKUNA CHA MPANGO KAZI WALA NINI, najiulizaga sana ninapo kuta mtu ana biashara nne sehemu moja UTAKUTA MTU ANAMILKI Hoteli, Toyo, Saluni na Kibanda cha kuchajisha simu.

  Huyu mtu sidhani anaweza jibu kwamba baada ya miaka 5 unataka kuwa wapi.

  d. Kuwa na Uongozi mbaya/Bad management

  Hili nalo ni sugu sana kwetu na ndio linalo tumaliza sisi Watanzania na ni swala ambalo limekuwa ni la kawaida na halipewi ufumbuzi
  Tumekuwa tukianzisha biashara bila kujipanga katika safu ya uongozi, tunaanzisha biashara na kuweka watu wa ajabu katika kusimamia, TUNAWEKA WAKE ZETU KUWA MAMENEJA, TUNAWEKA WACHUMBA WETU KUWA MAMENEJA, TUNAWEKA MASHEMEJI KUONGOZA BIASHARA ZETU, TUNAWEKA BABA ZETU/MAMA ZETU/ DADA ZETU/KAKA ZETU/WADOGO ZETU/WAJOMBA ZETU NA KADHALIKA.

  Mimi sina ugomvi na kuweka hata mke/ shemeji/dada/kaka/baba/mama kuwa watawala katika biashara, swali ni Je, wana ujuzi wa kuongoza biashara zako? Umewapa semina?
  - Huwezi piga hatua kwa kuweka watu wasio kuwa na uelewa wa biashara,


  e. Kupanua biashara harakaharaka/Expanding quicly

  Tunaanzisha biashara leo kesho tusha panuabiashara bila kujali madhara yake ni yapi.

  f. Tatizo la masoko/ kutangaza biashara yako
  Hili huenda likawa na tatizo namba moja kabisa linalo sababisha biashara nyingi sana ndogo zife.
  Masoko ni kitu cha muhimu sana katika biashara, bila wanunuzi hujafanya biashara/ wateja ndo watu watakao nyanyua biashara yako,wateja ndo partner namba moja katika biashara.

  TUMEKUWA TUKIANZISHA BIASHARA BILA KUJUA TUTAMUUZIA NANI
  1. Unaanza kufuga kuku bila kujua utamuuzia nani
  2. Unaanzisha ufugaji wang'ombe wa maziwa bila kuwa na soko
  3. Mtu anafungua hoteli bila kujua ni wakina nani watakula humo
  4. Unaanza kulima Mahindi, maharage na kadhalika bila kujua utamuuzia nani.
  Hili ndio Kosa kubwa sana tunalo fanya watanzania, Tunaashumu watanunua tu, Tunaanza kufuga kuku tukiamini kuna soko bila hata kufanya utafiti, TUNAASHUMU WATEJA WATAPATIKANA TU,
  INASIKITISHA SANA MTU KUJITOKEZA HUMU NA KUSEMA ANA MAYAI YA KISASA ANAUZA, WEWE ULIANZA VIPI KUFUGA KUKU BILA KUJUA UTAMUUZIA NANI MAYAI?

  Hili Tatizo husababisha wanunuzi kuwa wapanga bei, Cheki kwenye kilimo wapanga bei ni wanunuzi, ndo wanapanga bei kwa sababu ulilima bila kujua utamuuzia nani.

  Hii huwa kama MONOPSON, TABIA ZA MONOPSON NI KWAMBA YEYE NDO HUWA ANAPANGA BEI NA SI MZALISHAJI.

  g. Kushindwa kuendana na mabadiliko ya soko

  Tumekuwa tukianzisha biashara lakini tunashindwa kuendana na speed ya soko na mabadiliko ya soko,
  MFANO: soko linapo badilika bila ya wewe nawe kubadilika matokeo yake ni kushindwa.

  h. Kushindwa kupunguza ghalama za uendeshaji

  Hili nalo huwa ni tatizo kubwa sana kwetu watanzania, gharama za uendeshaji zinaposhindwa kupunguzwa kinachofuatia ni biashara kukushinda.

  TUMEKUWA TUKIFANYA VITU KIMASIFA SANA MFANO:
  Mtu anaazisha Hoteli, anashindana na wenzake kuweka kila kitu mara DSTV, MARA TV MARA, HIKI MASHINE YA JUICE
  Unapoanzisha biashara unatakiwa ujiangalie wewe kama wewe usianzishe kushindana na migahawa mikubwa wakati wewe huna huo uwezo, anza na kuweka juice kwenye galoni, anza na screen pekee unakuwa unawawekea wateja mikandaa theni ukipanua mtaji ndo uangalie mambo ya DSTV.

  Ni lazima gharama zisizo kuwa za lazima sipunguzwe, utakuta mtu na hoteli yake au kibanda cha kunyolea watu na anatumia genereta, utakuta genireta iko on na hakuna mteja hata mmoja, wafanyakazi wanaishia kutazama TV,


  i. Kuwa dharau washindani wako.

  Tumekuwa tukianzisha biashara bila kwanza kuwasoma tabia washindani wetu, matokea yake washindani wako wakibadilisha muelekeo kidogo tu ni kwamba inabidi tu ufunge biashara yako.

  MFANO: Una mradi wa kufuga ng'ombe na mko wengi wewe bila hata ya kujaribu kuwachunguza wenzako wana mikakati gani kwa siku za usoni unaingia kichwa kichwa.

  Jaribu kuchunguza washindani wako wana mikakati gani? nini wanatarajia kufanya siku za hivi karibuni? jaribu kuwapeleleza sana na usiwadharau.

  J. Kuwategemea wateja wachache.
  Madhara ya kuwategemea wateja wachache ni kwamba baadae wataanza kupanga bei wao na wakishajua wewe huna wateja wengi zaidi ya kuwategemea wao tu itakuwa balaa sana.

  MFANO: Unaanza kufuga kuku ukiulizwa soko liko wapi unasema pale jirani kuna Mtu huwa anakaanga chips so atakuwa akinunua.
  Wateja wachache ni hatari sana katika biashara

  k. Upangaji mbaya wa bei,
  Tumekuwa tukipanga bei bila kuangalia hali halisi ikoje. Kuna madhara ya kupanga bei ya juu sana au ya chini sana katika biashara.
  Mfano: Bei ya juu sana hupunguza mauzo hivyo kuongeza gharama za uzalishaji na tena kuongeza bei ya hiyo bidhaa na mwisho ni kushindwa.

  Bei ndogo nayo hupelekea kampuni kushindwa kukava cost za uzalishaji.

  l. Kuvujika kwa teem ya kampuni/ partners/wabia

  Mara nyingi watu wanapokuwa wanaanzisha biashara huwa partners wawili au hata wa ne ila kadri siku zinavyokwenda baadhi huamua kujiondoa kwa sababu ya maswala mbalimbali, mfano mgawanyo wa faida, na maswala mengine ya kiutawala
  Hii hupelekea kampuni kukosa mwelekeo na hatimaye kufa.

  Katika hii timu huwa kuna watu muhimu sana katika nafasi fulani so inapo sambaratika biashara huyumba sana na kufa

  m. Kutaka kushindana mojo kwa moja na kiongozi wa sekta.

  Hili huwa ni tatizo kwa wafanyabiashara wadogo, mara nyingi mtu huanzisha biashara na kutaka kushindana moja kwa moja na leaders wa sekta.

  MFANO: Chukulia Biashara ya kusindika nafaka, wewe unaazisha packaging ya unga wa mahindi halafu moja kwa moja unataka ushindane na wakina Azania, Mohamed entrprises, hiki ni kitu cha hatari sana kwa sababu wale wana strategies nyingi sana za kimasoko hivyo wanauwezo wa kukuondoa sokoni sekunde,Wana bajeti kubwa sana ya matangazo na usambazaji kiasi kwamba wewe huwezi fuadafu kwao.

  ILI KUPUNGUZA HAYA HAKIKISHA BASI WEWE MJASIRIAMLI UNA KUWA NA HAYA,

  1. Elimu ya biashara/ Uelewa katika Nyanja nzima ya biashara
  2. Elimu ya masoko ni muhimu sana
  3. Uwezo binafisi wa kuongoza biashara yako/Kuisimamia vizuri
  4. Mtaji wa kutosheleza
  5. Mtu wa kujituma/ Fanya kazi kwa bidii, na ikibidi extra hardwork inahitajika

  TEAM YAKO YA KUSIMAMIA BIASHARA INAPASWA ANGALAU WAWE NA UELEWA KATIKA HAYA MAMBO


  1. Elimu kidogo ya maswala ya fedha, wawe na uelewa wa kawaida katika maswala ya fedha
  2. Wawe na Elimu ya maswala ya Uhasibu, unaweza mfundisha mmoja ambae ndo msimamizi wa fedha
  3. Ni vizuri wakawa wana jua sheria kidogo baadhi ya sheria zile muhumu, make bila kujua baadhi ya sheria unaweza jikuta katika matatizo bila kujua
  4. Elimu ya mambo ya utawala ni muhimu, Mpatie meneja wako elimu ya utawala afahamu jinsi ya kuwaongoza wafanyakazi wako
  5. Elimu ya masoko nayo ni muhimu sana.wajue jinsi ya kutafuta masoko
  6. Elimu ya kuuza nayo ni muhimu sana
  7. Elimu ya huduma kwa wateja yaani customer care
   
 2. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #2
  Jan 16, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  Yapu hii ni meipenda sana mkuu,
   
 3. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #3
  Jan 16, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,740
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Asante sana mkuu kwa elimu nzuri uliyoitoa kuhusiana na biashara. Hata mimi nilikuwa nina mawazo kama haya ya kwako. Bila shaka elimu hii itawasaidia wajasiriamali wote wa Tanzania katika biashara zao ili bishara zao zisife.
   
 4. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #4
  Jan 16, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  poa mkuu, kikubwa ni kwamba tuyafanyie kazi na tusiishie kuserve kwenye flash na kwenye computer zetu,

   
 5. SaidAlly

  SaidAlly JF-Expert Member

  #5
  Jan 16, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,806
  Likes Received: 648
  Trophy Points: 280
  Hauna copy (pdf format) utuwekee hapa tui-download? Itatusaidia sana ktk Elimu ya Ujasiliamali.

  Thanks!
   
 6. MGAWARIZIKI

  MGAWARIZIKI JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2012
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 306
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Good! haya sasa wale wanaokulupuka kuanzisha biashara bila mipango.
   
 7. Kitope

  Kitope JF-Expert Member

  #7
  Jan 17, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mjomba! ufafanuzi rahisi ni kwamba wengi wa biashara ndogo ndogo huwa pia wanategemea biashara hiyo hiyo itoe mkate wa kila siku! sasa kwa ukubwa wa faida wanayoipata kwa siku mambo unakuta hayaendani na mahitaji yao. hivyo mtaji unalika taratibu na mwishowe kujikuta mtu upo hoi na biashara imekufa! mambo mengine yanaweza kuchangia lakini kwa hapa kwetu wengi huwa tufanya mahesabu kwa mtindo huu :- bei ya mauzo - bei ya manunuzi = faida.
   
 8. Kitope

  Kitope JF-Expert Member

  #8
  Jan 17, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Au fanya hivi kwa kiswahili safi Gharama - Kipato = faida. inabidi awe fasta kwa sababu mama kaagiza mtoto aje dukani kuchukua ela ya kununulia vitunguu. Hichi ni kitendawili lakini na mtu asipofanya hivyo ataishi vipi?? akaibe?? soo solution ni mtu mwenyewe kuwa makini kwa sababu wapo wengi wanaishi kwa mitaji midogo na hawafungi biashara miaka nenda miaka rudi.
   
 9. M

  Mtafiti77 Member

  #9
  Jun 11, 2015
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimezinduka!
   
 10. mikonomiwili

  mikonomiwili JF-Expert Member

  #10
  Jun 12, 2015
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  wasomi waoga sana kwenye biashara

  utitiri woote huo siunakuogopesha ?
   
Loading...