Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,672
- 40,549
Kwanza namshukuru Dr. Khamisi ambaye kupitia KLH News alinidokeza uwepo wa nyaraka hii. Barrick Gold ni kampuni iliyosajiliwa Canada. Na kimsingi shughuli zao wanazofanya kule Canada zinaongozwa na sheria za nchi hizo ambazo kwa upande wa madini ni mojawapo ya sheria ambazo zimekomaa zaidi na ni mfano kwa nchi nyingi zaidi.
Niliposoma Mkataba wa Buzwagi, jambo moja lilikuwa linanisumbua; kwanini inaonekana kana kwamba Mkataba unaweka mpaka mkubwa katika masuala ya fedha? Sikuweza kujua chanzo cha hisia hizo hadi nilipopata kuiona sheria hii ya madini ya Canada (ambayo ni sehemu ya Sheria yao ya Ardhi). Nilichogundua ni kuwa kwa mtazamo wa Barrick Gold, mkataba wa Buzwagi ni kinyume kabisa na sheria ya madini ya nyumbani kwao!
Utaona kuwa vipengele ambavyo tumevilalamikia hapa kwenye mkataba huo viko kinyume kabisa vipengele kama hivyo kwenye sheria ya madini ya Kanada. Ni wazi kuwa waliowakilisha Barrick kwenye mazungumzo na serikali yetu walikuwa wanaongozwa na "kwenda kinyume" na sheria ya Canada kwani sheria ya Canada inalenga kunufaisha jamii na nchi na pia kuhakikisha kuwa kampuni inanufaika.
Ni kweli kumbe unaweza kuwa na sheria ya win-win bila kufukuza wawekezaji.
TAFADHALI ipitie sheria hii hasa Kifungu cha 65-67 na ulinganishe na sheria yetu au mkataba wetu na Buzwagi. Tukisema tumeibiwa mchana, tunatumia lugha ya kiungwana, TUMELIZWA!
M. M.