Kwanini barabara za jiji hakuna njia za baiskeli?

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,571
15,321
Hawa designer wa huu mradi wa kulipendezesha jiji walitusahau sisi tunatumia baiskeli kama chombo cha usafiri na anasa binafsi.

Nimeona kwa Mabeberu kule licha ya utajiri wao lakini hawajatusahai wapenzi wa baiskeli.

Serikali itukumbuke aisee, maana wengine ndio anasa zetu. Ila nikiona jinsi jamaa wanavyoendesha baiskeli huko Kariakoo na Posta ni kama swala wanaoogelea kwenye bwawa lililojaa mamba. Near miss za kufa mtu.
 
Yaan kasheshe kweli, unatembea pembezoni lkn huko huko pembezen mara boda boda na wao wanataka kupenya yaan ni kero
 
Jana muda kama huu, nlikua na rafiki yangu tunatembea taratibu kulikata pori lenye giza totoro, tunatoka kijiji cha jirani kilabuni kuelekea nyumbani. Tukipiga story za hapa na pale kana kwamba hakuna kesho. Hua ni mwendo wa masaa 3 kutoka kijiji chetu mpaka hicho cha jirani (ila tukilewa sana tunatumia 4 mpaka 5) kufika nyumbani.

Tulikua tunajadiliana kuhusu aliezila zile hela za bunge la ulaya € Millioni 27. Hivi bado hamjamjua tu nyie mnaokaa mijini??? Maana tuna shida nae atupe mkopo wa elf 2, kwaajili ya bakuli 4 pale kilabuni tunazodaiwa???
 
Kwa kweli Wakoloni wafanye mpango wa kurudi Africa. Hatuwezi kujiongoza, hatuwezi kujitawala, hatuwezi kuchaguana, tunauana, tunatafuna mali za umma na misaada, hatuwezi lolote. Hatuwezi.
 
Mkuu wewe unashangaa njia za baiskeli wakati hata sehemu za kushushia abiria kwa daladala hawaweki foleni kila siku tunalia sababu ya hili...morogoro road mfano tu...hata kuchepusha road pembeni kwa ajili ya kushushia abiria walisahau ndo wakumbuke wa baiskeli
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom